MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
Mkuu PascoMkuu, lets be fair, kuna tiba inaitwa 'hypinotisim' haimuhitaji tabibu kuwa na cheti chochote zaidi ya 'convincing power!', hivyo Mwaka is very right na anasaidia wengi!.
Nionavyo mimi Mwaka na Kigwa wanafanana kwa mengi.
Kama ni waganga wa tiba asili kujitangaza wanajitangaza wengi why mwaka tuu?!. Hivi Babu wa Loliondo alikuwa na vyeti?, alisomea wapi zaidi ya kuoteshwa kwenye ndoto?!, alipata wapi vibali?!.
- Wote ni madaktari, tofauti ni Kigwa kasomea, Mwaka hajasomea!, hivyo hapa kuna ka wivu ka mmoja kujisikia zaidi kuliko mwingine!, sasa kitendo cha anayejisikia kupewa rungu, kazi ya kwanza ni kumtwangia mshindani wake!.
- Aliyesemea hana practicing certificate kwa sababu hakufanya intenship, hivyo amebaki daktari jina!, asiyesomea, ana pactice and make money!. Hapa ni wivu tuu wa maendeleo!.
- Wote wanamiliki majumba ya ghorofa, mmoja kigorofa chake ni kimoja, anakimalizia kwa kujinyima sana!, mwingine anazo ghorofa tatu za haja!.
- Wote wanatumia Rangerover sport, mmoja ya kwake ni ya zamani 2006 na CC zake 2.7, mwingine ni ya 2012 cc zake 4.3!, hivyo hapa ni husuda tuu!.
- Wote they are good looking and smart, wanapenda kuvaa vizuri, tatizo ni mmoja ana uwezo wa kuvaa suti za Mwasu, AK's au zile za lile duka pale, JM Mall, Mlimani City, Msasani Mall, na mwingine yeye ni zile suti za yale maduka pale Kinondoni, au Sinza kama Roby One, Hasani Pamba Kali!, hivyo hapa ni wivu tuu wa kipato!.
- Wote wanapenda kutokea kwenye TV, mmoja analipia kutokea kwenye vipindi vyake, mwingine ili kutokea ni mpaka wakati wa vikao vya bunge!, hivyo lengo ni kumzima asitokee sana ndio maana anaulizwa kwa nini anajitangaza!, watu wa tiba asili wote wanaojitangaza hajawaona!, kuna mtu anajitangaza zaidi ya mzee wa DFP?!.
- Wote wanapenda totoz, mmoja kisirisiri, mwenzake kiwazi wazi, hivyo hapa ni husda tuu ya kwa nini apendwe?!.
- Wote wanapenda pesa, mmoja anazo nyingi za kutosha!, mwingine anasubiri za mshahara mwisho wa` mwezi au posho za vikao!. Hivyo hapa ni wivu wa kipato!.
- Wote wanapenda mafanikio na biashara, mmoja biashara yake ni ya kudumu, anapiga pesa mwanzo mwisho!, mwingine biashara yake ni ya msimu, hivyo hana uhakika sasa, kutegemeana na upepo wa kisiasa, hivyo hapa ni wasiwasi tuu wa maisha!.
- Wote wawili wanampenda sana mwanamuziki Diamond Platnumz, kosa ni mmoja kaimbwa na diamond, mwingine hata kutajwa hatatajwa!.
Watanzania lazima tufike mahali tuache wivu wa kike kwa kila mwenye nacho, kila mtu a fight very hard to get rich or just die trying!.
Pasco
Kuna uwezekano ni kweli kwa haya uliyoyasema kuhusu wivu lakini hii haiondoi ukweli kuwa kuna taratibu au sheria zimevunjwa!
Kuna watu naamini walikuwa wanawaonea wivu wale jamaa wa TRA na TPA ambao kwa sasa wana kesi ya kujibu mahakamani. Kuna watu naamini walikuwa wanasema kama ningekuwa fulani wa TRA au TPA ningekuwa pia natanua kama wao huku wengine wakisema kama ningekuwa nina mamlaka ya kuwakamata ningewakamata kwa sababu ya madudu wanayoyafanya.
Matamanio haya hayaondoi ukweli kuwa hawa jamaa wa TPA na TRA walikuwa wanaihujumu serikali ili watajirike na kutanua. Hata DK. Mwaka alikuwa anaihujumu serikali ili avune mapato mengine ambayo yanahitaji modern doctors.
Jaribu kusoma angalizo hili la mdau ambaye ana uelewa katika eneo hili,
Dr. Preta! Mwaka amefanya makosa katika utambulisho wake..
1) Angejinasibisha ni mtaalamu wa Tiba Mbadala kama Mkuu Mzizi Mkavu wa JF
2)Mwaka picha nyingi ninazoziona kwenye mitandao na matangazo amening`iniza stethoscope shingoni... sidhani kama anajua hata kuitumia ? Heart sounds takes years of practice kuzi master ndio maana medicine ni miaka 5 mpaka 6
3)Anapicha nyingine amebeba kitabu cha Obstetrics and Gynecology yeye ni mtaalamu wa tiba mbadala hicho kitabu ni cha nini ? amefika mbali na kujinasibisha ni Mtaalamu wa magonjwa ya kina mama ... jamani! kuwa gynecologist lazima uende Medical school miaka 5 mpaka 6 , ufanye mwaka mmoja wa internship then urudi shule ku specialise miaka 4 tena... mwaka yeye amefanya training ya mwaka mmoja na red-cross china anajiita gynecologist ????
4) Pelvic Exam, kufanya uchuguzi sehemu za siri za kina mama na dada zetu "ONLY A QUALIFIED PHYSICIAN NDIO ANARUHUSIWA JUST INCASE IKATOKEA SEVERE BLEED , A PHYSICIAN WILL KNOW HOW TO INTERVENE " Sidhani Mwaka kama anaweza kushona hata kidonda..
5) Unapofanya pelvic exam kuna some modern equipment's zinatumika again only certified physician ndio anaruhusiwa kuvitumia ... mfano kama mwana mama ana matatizo ya kizazi kumbe she has Carcinoma of the cervix, most of CAX ukigusa tu zina bleed ,, je mwaka ana blood bank pale clinic yake ?!! JE IKATOKEA MGONJWA AMEFARIKI WAKATI MWAKA AKIFANYA PELVIC EXAM UNAJUA ITAKUWA NI MURDER CASE ?! SABABU MWAKA HE WAS NOT TRAINED KUTOA HIYO HUDUMA.
MWISHO
Mimi sina neno na Mwaka! ila tu arudi kwenye misingi yao ya tiba mbadala na asifanye utatibu kama wanavofanya madactari wa modern medicine including kufanya Pelvic exam...
Kuna watu wanacomplain mbona kikombe cha babu watu walitumia ... well babu hakuvaa stethscope , babu hakujiita gynecologist, babu tiba yake ilikuwa ni kiimani zaidi...
hata sisi waislam tuna wataalamu wetu wa tiba za kissuna huwasikii wakijitangaza ni ma gynecologist wala kufanya uchunguzi wa kizazi kama mahospitalini wanavofanya...
Mwaka amshukuru sana Mh.Dr. H. kingwa! sababu ingefika siku mgonjwa akafariki basi mahakamani angehukumiwa kama muuaji sababu si tabibu aliyekuwa trained kufanya yale anayo yafanya ...
Last edited by a moderator: