Dkt. Mpango uwakemee na Viongozi wa Kanisa Katoliki pale ambapo unaenda kusali wasiwe wanazuia waumini kutoka mpaka wewe unapo ondoka kwenye viwanja

Milonji

Senior Member
May 26, 2022
153
494
Taifa la Mungu ninawasalimu wote.

Jana vyombo vya habari viliripoti taarifa hii ya maelekezo kutoka kwa Makamu wa Raisi Dk. Mpango.

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mango akiwa ziarani Mwanza amesema hataki kusikia tena Barabara zikifungwa kwa masaa mengi ili apite, huku akisema dakika 10 zinatosha ili Wananchi waendelee na shughuli zao. Kwa hilo ninamuunga Mkono 100%.

Ninakuomba Mh. uwakemee na Viongozi wa Kanisa Katoliki pale ambapo unaenda kusali wasiwe wanazuia waumini kutoka mpaka wewe unapo ondoka kwenye viwanja vya Kanisa.

Hali hii imekuwa kero sana na makwazo kwa waumini wenzako. Hata mimi binafsi nikikuta tupo wote kwenye hiyo Misa mzuka wa Kusali huwa unaisha kabisa.

Mh. Mpango, kuna siku tumezuiwa kutoka eneo la Kanisa (geti la nje) kwa zaidi ya saa moja na nusu kwa maelekezo ya kwamba tusubiri kwanza hadi utoke na sisi ndiyo tutoke.

Aisee, yaani Misa imeisha tukaambiwa hakuna kutoka kwa sababu umeenda kuwasalimia Mapadre na baadae ukaenda kuwasalimia Masista huku sisi tunakusubiri na Misa imeisha na Misa nyingine imekwisha anza. Lakini hatukutakiwa kutoka mpaka wewe uondoke.

Ulipo rudi na kuondoka tukajikuta waumini wa Misa mbili tunatoka wote kwa pamoja.

Kuna siku nakaribia Kanisani naona na Msafara wako unaingia Kanisani. Ili usinikwaze nikaamua kuchukua Bodaboda na kwenda Kusali Parokia nyingine iliyo karibu japo kwa kuchelewa.

Ndugu zangu, baada ya kusikia kauli yake Juzi nikakumbuka kwazo hili na nimeandika hapa kiwakilisha Waumini wengine ambao wamekuwa wakikerwa na Jambo hili pia nina amini Ujumbe huu umemfikia

Wenu Chaliko.
 
Nasikia Mzee anasali sana. Security wamemkataza apunguze idadi yA sala zake za asubuhi lakini kagoma
 
Inaboa sana, binafsi huwa nikijua kiongozi fulani wa juu anasali kanisa ambalo nilipaswa kusali, huwa nabadili maamuzi fasta maana sipendi kunyanyasika mbele za Madhabahu, mara mtaambiwa hapa msikae, mara mtaambiwa ndani kumejaa mnatengewa kaeneo ka kukaa huko nje kama mateka
 
Taifa la Mungu ninawasalimu wote.

Jana vyombo vya habari viliripoti taarifa hii ya maelekezo kutoka kwa Makamu wa Raisi Dk. Mpango.

"Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mango akiwa ziarani Mwanza amesema hataki kusikia tena Barabara zikifungwa kwa masaa mengi ili apite, huku akisema dakika 10 zinatosha ili Wananchi waendelee na shughuli zao."

Kwa hilo ninamuunga Mkono 100%.

Ninakuomba Mh. uwakemee na Viongozi wa Kanisa Katoliki pale ambapo unaenda Kusali wasiwe wanazuia waumini kutoka mpaka wewe unapo ondoka kwenye viwanja vya Kanisa.

Hali hii imekuwa kero sana sana na makwazo kwa waumini wenzako. Hata mimi binafsi nikikuta tupo wote kwenye hiyo Misa mzuka wa Kusali huwa unaisha kabisa.

Mh. Mpango, kuna siku tumezuiwa kutoka Eneo la Kanisa (Geti la Nje) kwa zaidi ya Saa Moja na Nusu kwa maelekezo ya kwamba tusubiri kwanza hadi utoke na sisi ndiyo tutoke.

Aisee, yaani Misa imeisha tukaambiwa hakuna kutoka kwa sababu umeenda kuwasalimia Mapadre na baadae ukaenda kuwasalimia Masista huku sisi tunakusubiri na Misa imeisha na Misa nyingine imekwisha anza. Lakini hatukutakiwa kutoka mpaka wewe uondoke.

Ulipo rudi na kuondoka tukajikuta waumini wa Misa mbili tunatoka wote kwa pamoja.

Kuna siku nakaribia Kanisani naona na Msafara wako unaingia Kanisani. Ili usinikwaze nikaamua kuchukua Bodaboda na kwenda Kusali Parokia nyingine iliyo karibu japo kwa kuchelewa.

Ndugu zangu, baada ya kusikia kauli yake Juzi nikakumbuka kwazo hili na nimeandika hapa kiwakilisha Waumini wengine ambao wamekuwa wakikerwa na Jambo hili pia nina amini Ujumbe huu umemfikia

Wenu Chaliko.
😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom