Kutoka Ufaransa: Makamu wa rais Dkt. Mpango akutana na Seneta Ronan Dantec

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,031
23,822
30 Juni 2021
Paris , France

02-12-1536x1051.jpg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Juni 30, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa kundi la maseneta wa kifaransa marafiki wa Tanzania Mheshimiwa RONAN DANTEC M. Ronan Dantec, sénateur de la Loire-Atlantique (Pays de la Loire) - Sénat.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika jengo la Bunge la Seneti Paris Nchini Ufaransa. Seneta Dantec amezungumza na Makamu wa Rais juu ya umuhimu wa kuhifadhi mazingira lengo likiwa ni kupunguza hewa mkaa duniani. Pia ameshauri uwepo wa mfuko wa fidia kwa wale watakaothirika na masuala ya kuhifadhi na kulinda mazingira. Makamu wa Rais Amesema amefurahishwa na namna uhifadhi wa mazingira unavyofanyika nchini ufaransa ikiwemo Mji wa Paris licha ya ukongwe wa mji huo.

Amemuhakikishia Seneta Dantec kwamba Tanzania ipo tayari kushirikiana na Ufaransa katika uhifadhi wa mazingira na kuwakaribisha Maseneta rafiki wa Tanzania katika kutekeleza hilo kwa pamoja. Amesema Tanzania inazingatia uhifadhi wa mazingira lakini kwa kulinda haki za wananchi wakati wa utekelezaji wa uhifadhi huo.

Pia Makamu wa Rais ametembelea maktaba iliopo katika jengo hilo na kujionea historia mbalimbali iliohifadhiwa vizuri ya uongozi mbalimbali uliowahi kutawala Nchi ya Ufaransa. Aidha Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ametembelea ukumbi wa Mikutano ya Bunge la Seneti na kupokea maelezo kutoka kwa Bi. Maryam Zadeh moja ya wahudumu katika Bunge hilo.

Makamu wa Rais yuko Nchini Ufaransa kuhudhuria Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa (Generation Equality Forum) linalofanyika Juni 30 hadi Julai 2 ,2021 lenye lengo la kuchagiza haki za usawa wa kijinsia kama zilivyokubaliwa katika mkutano wa Beijing wa mwaka 199

Source: KONCEPT TV
 
Tafadhali bagamoyo mnapo pata wasaa wa kusogoa na vp uwe unachomekea na ishu ya katiba mpya.

Mwambie watanzania wanaamini katiba mpya ndiyo itakuwa tiba kamili ya uhifadhi endelevu wa wanyama pori.

Kifupi mwambie tunataka katiba mpya
 
Kutokana na hali yake ya Kiafya kuwa ni ya 'tia maji tia maji' tokea augue Mwezi February kwenda March mwaka huu ( 2021 ) tafadhali kabla hajarejea Tanzania ahakikishe amepigwa Chanjo (Jab) ya Corona kutoka katika mojawapo ya Astra Zeneca, Pfizer, Moderna na Johnson and Johnson.
 
Kutokana na hali yake ya Kiafya kuwa ni ya 'tia maji tia maji' tokea augue Mwezi February kwenda March mwaka huu ( 2021 ) tafadhali kabla hajarejea Tanzania ahakikishe amepigwa Chanjo ( Jab ) ya Corona kutoka katika mojawapo ya Astra Zeneca, Pfizer, Moderna na Johnson and Johnson.
Yani usiku huu huko macho hujalala? Mchana kutwa huko humu. Homwek kweli umefanya? Kama taifa tunaenda wapi. Mama anajitahidi sana kutunyooshea njia lakini vijana uchwara kama wewe mnamlet down.

Huo muda wa kutolala mnautoa wapi!

Kamoooonn Lala bwana!
 
Yani usiku huu huko macho hujalala? Mchana kutwa huko humu. Homwek kweli umefanya? Kama taifa tunaenda wapi. Mama anajitahidi sana kutunyooshea njia lakini vijana uchwara kama wewe mnamlet down.

Huo muda wa kutolala mnautoa wapi!

Kamoooonn Lala bwana!
Hahaha daah Kweli.
 
Yani usiku huu huko macho hujalala? Mchana kutwa huko humu. Homwek kweli umefanya? Kama taifa tunaenda wapi. Mama anajitahidi sana kutunyooshea njia lakini vijana uchwara kama wewe mnamlet down.

Huo muda wa kutolala mnautoa wapi!

Kamoooonn Lala bwana!

Kwahiyo mama anataka tulale muda kama huu au unataka jamaa akuite mkalale ili ushuhudie vizuri mlivolala na umpelekee habari mama.
 
Senatorial Election 101

Is the French Senate a retirement club for old politicians?


Senate members, 348 in number to be precise, how they enter the chamber the so called Upper House . And Who are these 162,000 Big voters that have privilege of electing senators on behalf of all French citizens..
Source : France 24

Le Sènat
The French Parliament is made up of two chambers, the National Assembly and the Senate. Members of the two Houses are chosen by two different electoral systems. This ensures that all the diverse components of French society are represented as fairly as possible.​

Examination of bills by both Houses of Parliament makes for better laws and the well proven experience of the Senators improves their content.

The Speaker of the Senate ensures the stability of France’s institutions as he is called upon to replace the President of the Republic in the event of his death or resignation.

Even in France few people have an in depth knowledge of how the Senate works as only local electoral office holders and members of the Assembly of French Citizens Resident Abroad elect the senators. That is to say the 348 Senators are elected by part of the country's local councillors, as well as by representatives of French citizens living abroad.

Discover this full fledged parliamentary assembly : its purpose, its organisation and the place where it sits, the Luxembourg Palace .

The 348 senators are assisted by specialised civil servants and parliamentary aides. In all, 2000 people work here.
Source : Senat.fr Un site au service des citoyens
 
Africa.

Tunafunga safari mpaka ulaya kujadili namna ya kutunza mazingira.

Nini hasa faida ya kuwa na vyuo vinavyotoa kozi na utunzaji mazingira kama mwika etc?

Faida ya wataalam wetu ni nini hasa.

Hivi ni lazima sana tufike Ulaya ndio tuonekane kuwa tupo serious na maendeleo?
 
Tafadhali bagamoyo mnapo pata wasaa wa kusogoa na vp uwe unachomekea na ishu ya katiba mpya.

Mwambie watanzania wanaamini katiba mpya ndiyo itakuwa tiba kamili ya uhifadhi endelevu wa wanyama pori.

Kifupi mwambie tunataka katiba mpya
Saccos ya ufipa mnayo hata katiba ya zamani kweli?.
 
Africa ....

Tunafunga safari mpaka ulaya kujadili namna ya kutunza mazingira.

Nini hasa faida ya kuwa na vyuo vinavyotoa kozi na utunzaji mazingira kama mwika etc??

Faida ya wataalam wetu ni nini hasa.

Hivi ni lazima sana tufike Ulaya ndio tuonekane kuwa tupo serious na maendeleo??

Wazalendo wapenda mazingira wapo wengi hapa Tanzania tuwaenzi
reginald mengi mansion 1

POSTED BY: MAUREEN WARUINGE
MAY 10, 2019

Late Tanzanian billionaire Reginald Mengi’s mega mansion​

Photos of the sprawling mansion belonging to the late Tanzanian billionaire Reginald Mengi have surfaced
 
Africa.

Tunafunga safari mpaka ulaya kujadili namna ya kutunza mazingira.

Nini hasa faida ya kuwa na vyuo vinavyotoa kozi na utunzaji mazingira kama mwika etc?

Faida ya wataalam wetu ni nini hasa.

Hivi ni lazima sana tufike Ulaya ndio tuonekane kuwa tupo serious na maendeleo?
Afrika bado tunatakiwa kutawaliwa au kuwa chini ya Utawala fulani.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom