Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,126
- 20,550
Daktari Philip Isdor Mpango, habari? Prof Chachage Seithy Loth Chachage - alitumia neno ‘Collective Imbecilization’ kueleza uzuzu, ubwege, ufala wa pamoja unaoweza kufanywa na serikali Hili jaribio la kuwapumbaza watu mamilioni kwa mpigo.
Ni kama vile kuwakusanya watu milioni 50, ukawaweka ndani ya ukumbi mmoja kwa ukubwa huo Ukafunga madirisha na milango, ukawanyunyizia dawa ya uzuzu, ubwege na ufala, ikawakolea, ukawaachia waende Duniani waendelee shughuli zao.
Haiwezekani, isipokuwa inawezekana watu wakapumbazwa kwa pamoja, wakafanywa mazuzu kwa pamoja, wakageuzwa mabwege kwa pamoja Hata kama watu hao hawajioni ndani ya ukumbi huo na hawasikii harufu ya dawa ya ajabu wanayopuliziwa na kuwafanya kuwa mabwege na mazuzu.
Ipo mifumo imetumika, kutufanya sote tuwe mazuzu kama ambavyo alieleza Chachage alipokuwa akizungumzia “collective imbecilization” Kwamba Makamu wa Rais ni special force au secret service? Kwamba Makamu wa Rais unatumwa kazi za siri za serikali?
Ukajificha usijulikane ulipo? Daktari Mpango, hivi ni kwanini unawaona watanzania wote ni mazuzu? Tunakubaliana kwamba, mazuzu yapo, lakini siyo wote ni mazuzu. Dkt. Mpango, usilalamikie mitandao ya kijamii. Lawama peleka ofisi ya Makamu wa Rais.
Watanzania wanayo haki ya kuhoji alipo Makamu wa Rais, wao ndio wanaomlipa mshara na ameapa kuwatumikia.
Dkt. Mpango, unashukuru kuombewa na watu gani? Wanakuombea wapi na vipi wakati unasema ulikuwa katika shughuli maalum na siyo ugonjwa? Watanzania hawajui ulipokuwa ukipokea matibabu Korea Kusini.
Ni wapekuzi wachache tulifahamu hadi jina la hospitali uliyofanyiwa upasuaji. Ulikaa kimya umetumwa kazi ya kijasusi, mwezi mmoja baadae, uibukie kanisani halafu ukapokelewe Ikulu na Rais?
Aah! Akili gani hii Daktari? Ni mara ya pili hii, unazusha taharuki ukiwa katika matibabu, baadae unatoka kuzungumza na umma, unawasuta,huna haya wala moyo wa shukhran. Kuna kusema ulikuwa mgonjwa? Na kwanini unawafokea watu waliokuwa wanauliza makamu wa Rais yupo wapi?
Unasema ulikuwa unaona kila kitu ukiwa mafichoni, ukanyuti. Sasa kwanini unawasuta leo watu wanaokupenda na walikuwa wanauliza ulipo?
Kwamba hawakuwa na haki ya kuuliza Makamu wa Rais alipo? Hii ni tabia mbaya na haitakiwi kuwa desturi kwa watawala kuwapumbaza watanzania. Tunakataa.
Watanzania ndiyo mabosi wenu viongozi/watawala. Unapotea, mwezi haujulikani ulipo. Waajiri wako tunaanza kukutafuta, umejificha sehemu (tunajua hospitali), unatuchora tu? Unaona upo sawa? Ok! Baada ya mwezi mzima, unapatikana, unaibuka kanisani na Ikulu, kutufokea.
Unatufokea watu tunakununulia kila kitu ambacho unakula na kuvaa? Daktari Mpango, Rais ni bosi wako, sisi, watanzania ni waajiri wako, sisi ndiyo mabosi wako, pia mabosi wa Rais. Unawajibika kwa Rais, unatumikia wananchi.
Daktari, SIJAPENDA.
MM