Dkt. Magufuli, Rais Bora Afrika kwa mwaka 2019

Dkt. Magufuli, Rais Bora Afrika kwa mwaka 2019

Umeandika porojo tu ambazo kwa sasa hazina mvuto tena wa kuzisikia au kuzisoma mahali popote pale!

Kiufupi tu Watanzania tunataka maisha bora na siyo bla bla, na nyimbo za mapambio zisizoisha za kumsifia na kumtukuza mtu wenu.
 
Mtoa mada upo sawa kwa vigezo vyako. Mimi mtazamo wangu mbali ya mengi mazuri bado ana mitihani
1.Umoja na ustawi wa taifa tumerudi nyuma.ie ukanda,uchama,ukabila
2. Democrasia imedumaa kama sio kufa.
3. Chaguzi zisizokuwa za haki
4. Biashara haramu ya viongozi
5. Nafasi ya Tanzania Kimataifa ushawishi imeshuka.
6. Uwekezaji kwa ujumla umedumaa
7. Sector mama ya kilimo haijatendewa haki.
8. Watanzania wengi hawana furaha
9. Tatizo la ukosefu wa ajira linaongezeka
10. Ajira mpya na maslahi ya watumishi wa umma imegeuka hisani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anamshinda hata George Washington!
Yaani Hitler akasome.
 
Umewahi kufika nchi ngapi za kiafrika???tuanzie hapo
 
Sijasoma post za juu ila kama huyo ni Bora basi tuachie wafungwa wote walioko magerezani wameonewa!!!
 
Team JPM
Amefufua shirika la ndege lililokufa kwa kununua ndege mpya 8 kwa pesa taslimu

Hivi tunaweza kusema ATCL imefufuliwa ama imefikishwa idara ya wagonjwa mahututi yaani Intensive Care Unit na mgonjwa bado yu hoi taabani hajielewi anapumulia mashine, amepigwa nusu kaputi na kulishwa kwa mipira.

Tuwe wakweli ATCL haijafufuliwa bali imekimbizwa kwenye idara ya mahututi na hatujui hatima yake kama litapona kabisa au kutoka na ulemavu wa kila aina utakao sababisha kushindwa kujitegemea.
 
Huenda mimi ndio sijui maana ya ubora. Kama hivyo ulivyotaja ndio vinatoa rais bora, basi mbona marais wengi wa Afrika watakuwa bora? Maana ukiangalia hiyo list yako marais wengi wametekeleza kama sehemu ya majukumu yao. Ni vyema ungesema vitu Magufuli alivyotekeleza, ila suala la ubora ndani ya Afrika achana nalo. Ubora ni zaidi ya hivyo vitu vilivyo kwenye list yako. Ukumbuke na kuweka deni la taifa kwenye kipindi chake, ili tupime vizuri.
Mimi nimeweka ushahidi, Wewe leta vigezo
 
Hivi tunaweza kusema ATCL imefufuliwa ama imefikishwa idara ya wagonjwa mahututi yaani Intensive Care Unit na mgonjwa bado yu hoi taabani hajielewi anapumulia mashine, amepigwa nusu kaputi na kulishwa kwa mipira.

Tuwe wakweli ATCL haijafufuliwa bali imekimbizwa kwenye idara ya mahututi na hatujui hatima yake kama litapona kabisa au kutoka na ulemavu wa kila aina utakao sababisha kushindwa kujitegemea.

Wewe una chuki binafsi na ATCL, kila mtanzania anaona, Wewe tu kipofu
 
M
Umeandika porojo tu ambazo kwa sasa hazina mvuto tena wa kuzisikia au kuzisoma mahali popote pale!

Kiufupi tu Watanzania tunataka maisha bora na siyo bla bla, na nyimbo za mapambio zisizoisha za kumsifia na kumtukuza mtu wenu.
Maisha bora ni kuchapa kazi, bidii yako ndiyo maisha yako, hakuna vya bure.
 
Umemlinganisha na marais wa nchi ngapi za Afrika hadi ukafikia hitimisho hilo kuwa yeye ndie bora kati yao?
 
VAPS,
Awamu ya kwanza (2015-2020) ilikuwa kujenga miundo mbinu, Yaani nyenzo za maendeleo au maendeleo ya vitu, awamu ya pili (2020-2025) ni maendeleo ya watu. Hizi changamoto ndogo zitatatuliwa zote, tumuunge mkono akamalizie kazi.
 
Wewe una chuki binafsi na ATCL, kila mtanzania anaona, Wewe tu kipofu

Mimi pia ni Mtanzania lakini sioni unachodai kuwa "kila Mtanzania anaona". Na nina uhakika 110% kuwa kuna Watanzania wengi sana ambao hawajui chochote kuhusu ATCL, sasa hiyo "kila Mtanzania anaona" ina maana gani?
 
Awamu ya kwanza (2015-2020) ilikuwa kujenga miundo mbinu, Yaani nyenzo za maendeleo au maendeleo ya vitu, awamu ya pili (2020-2025) ni maendeleo ya watu. Hizi changamoto ndogo zitatatuliwa zote, tumuunge mkono akamalizie kazi.

Kama unayaamini haya uliyoyaandika hapa basi utaamini chochote utakachoambiwa na Magufuli. Hata akikuambia baba yako ni punda utaamini pia.
 
VAPS,
Awamu ya kwanza (2015-2020) ilikuwa kujenga miundo mbinu, Yaani nyenzo za maendeleo au maendeleo ya vitu, awamu ya pili (2020-2025) ni maendeleo ya watu. Hizi changamoto ndogo zitatatuliwa zote, tumuunge mkono akamalizie kazi.
Ma miradi kayachukua utafikri jitu halina hakili, hakuna mradi hata mmoja utakaokamilka ndani ya hii miaka mi5! Awamu ijayo ambayo ni ya mwisho inamwoa tena!
 
Kimsingi, kikanuni,kisheria na hata kiroho, Rais wetu amejitahidi sana kutenda haki na ametumia karama zake zote alizopewa na Mungu katika kuliongoza Taifa hili.
Tujiulize sisi ambao anatuongoza, je kama tungekalia kiti chake tungefanyaje kazi kulinganisha na yeye? Je kama Mbowe, Lowasa, Chenge nk wangekuwa kwenye kiti chake Inchi hii ingekuaje sasa?
Yote 20 yaliyoandikwa ni machache sana ukilinganisha na mengi aliyoyafanya ambayo hayakuorodheshwa.
Mihimili mikuu ya uchumi wa Inchi yoyote ni kilimo na viwanda.
Kwa Inchi zinazoendelea, kilimo lazima kitiliwe mkazo sana kikifuatiwa na Viwanda.
Si Viwanda kwanza halafu Kilimo baadaye, mbali Kilimo kwanza halafu Viwanda.
Katika mhimili wa Kilimo ambao ndiyo uti wa mgongo wa Inchi inayoendelea na ambao unagusa idadi kubwa ya Wanainchi, Inchi yetu haijafanya vizuri sana katika kuendeleza kilimo.
Tuaomba Rais wetu akisemee na kukiendeleza kilimo katika muhula wake wa pili ili tuwe na kilimo cha mapinduzi.
Akifanikiwa hili atapata umaarufu mkubwa Duniani kuliko haya anayofanya sasa.
"Industrial revolution"
 
Japo anamapungufu yake mengi tuu, ila ni raisi bora baada ya nyerere ukilinganisha na wenzake watatu waliomtangulia ana maono na atatufikisha mbali
 
Back
Top Bottom