Dkt. Magufuli aibomoa ngome ya Lowassa

Dkt. Magufuli aibomoa ngome ya Lowassa

Kwani lazima watu hao hao wawe viongozi.Je wengine hawawezi.Ni wakati sasa wa kubadilisha MINDSET zetu au tutakwenda kwenye utawala wa kifalme
 
Wewe magofuli hata akatambike hana uwezo wa kuibomoa ngome ya lowassa coz hata ye mwenyewe anasubiri neema ya lowassa ili amrufishe kuwa waziri......Raisi wa awamu ya tano mh.EDWARD LOWASSA
 
Watz tuna imani kubwa sana na magufuli

Watanzania hatuna imani na Magufuli kabisa ni mtaka sifa na dikteta kila kitu anajue yeye tu,kwanza ni mbinafsi mno,aliamua kuipitisha barabara kuu ya Mwanza hadi Bukoba jimboni kwake Chato,aliamurisha michoro ya awali kuachwa na ichorwe michoro mipya ya barabara itakayopitia jimboni kwake baada ya jimbo lake la awali kugawanywa na yeye akaamua barabara ipite liliko jimbo lake jipya.
 
Kuna dikteta kama viongozi wa CHADEMA wanaobadili Katiba ya CHAMAmchana kweupe ili waendelee kuka madarakani
 
View attachment 231365
Kambi ya Waziri Mkuu wa Zamani , Edward Lowassa inayoaminika kuwa ni ya siku nyingi zaidi katika kinyang'anyiro cha kusaka uteuzi wa kugombea urais kupitia CCM , hatimaye imeanza kusambaratika baada ya mmoja kati ya vigogo wake wa kutegemewa kwa mikoa ya Kanda ya ziwa kuanza kuisaliti kimya kimya.

Chanzo hicho cha habaari cha kuaminika kutoka kambi hiyo kigogo huyo ambaye alichangia kwa sehemu kubwa kujenga ngome imara ya LOWASSA katika Kanda ya Ziwa, hivi sasa amegeuka kimyakimya huku ikielezwa kuwa anayeibomoa ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli.

Inasemekana kigogo huyo ambaye pia ni mjumbe wa NEC na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM amekwenda kumshawishi Magufuli kwamba achukue fomu ya kugombea nafasi hiyo ya urais.

Habari zaidi zinasema kuwa Wajumbe wengi hasa wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM hawana imani tena na LOWASSA kutokana na sababu mbalimbali .

Wajumbe hao wamesema sasa hawataangalia nani ana nguvu kiasi gani ila watazingatia zaidi matakwa ya chama kwamba kinamtaka nani agombee urais.

Aidha wajumbe hao wamelaani tabia ya badhi ya Makada wa CCM kuwasingizia wananchi wa maeneo yao kuwa wamewatuma kwenda kwa Lowassa ili kumshawishi atangaze nia ya kugombea urais.

Wajumbe hao wamesema watu hao ni maswahiba wa LOWASSA wa siku nyingi na wanafanya hivyo kwa sababu hiyo na siyo kwamba wametumwa na wananchi wao.

Baadhi ya Makada hao wa CCM na ambao ni maswahiba wa siku nyingi wa LOWASSA ambao wanakwenda kwa LOWASSA kwa madai kuwa wametumwa na Wananchi ni pamoja na Mjumbe wa NEC kutoka Wilaya ya BUSEGA, Dk. RAFAEL CHEGENI na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Serengeti na mjumbe wa NEC.

Chanzo: Gazeti la CHANGAMOTO

Kumbe gazeti la changamoto
 
Kwani lazima watu hao hao wawe viongozi.Je wengine hawawezi.Ni wakati sasa wa kubadilisha MINDSET zetu au tutakwenda kwenye utawala wa kifalme
Watuj tuna mambo mengi ya kufanya, tunamtaka Magufuli ili tusihangaike kuhudhuria mikutano ya kampeni kutafuta nani anafaa.
 
Wapinzan wa lowassa hawalali cku hiz,ama kwel lowassa kiboko yenu aisee,mtawataja wote bado peter msigwa,sugu,wenje,nasari,maana kila kila kukicha wanaleta mpya tu.
 
Kumbe gazeti la changamoto
Ulitaka waandike Tanzania Daima? Hawezi kuandika habari njema kama hii , ni mwiba kwao. AISEE MAGUFULI akichukua fomu najiunga na CCM , nilkkuwasioni umuhimu wa kujiunga na chama cha siasa, sasa nashawishika.
 
Kuna dikteta kama viongozi wa CHADEMA wanaobadili Katiba ya CHAMAmchana kweupe ili waendelee kuka madarakani

Kazi ipo ,uelewa wetu ni mdogo sana na tumekaa kiushabiki tu wa vyama,hapa Chadema inaingiaje?waliozungumziwa ni Magufuli na Lowassa sasa hilo la Chadema limeingiaje hapa,nadhani wewe ndio wale wa ''zidumu fikra za mwenyekiti''na kuitikia zidumu hata pale fikra zake zikiwa za hovyo,tumia akili kufikiri kama wewe kwanza acha porojo za vyama,tujadili watu binafsi wanaoutaka uraisi,bila kujalisha ni Chadema,CCM,au CUF.Wakati mwingine uwe kwanza unasoma kilichoandikwa kwanza kabal ya kuanza kuiota tu Chadema.
 
Wapinzan wa lowassa hawalali cku hiz,ama kwel lowassa kiboko yenu aisee,mtawataja wote bado peter msigwa,sugu,wenje,nasari,maana kila kila kukicha wanaleta mpya tu.
Kwani akina Msigwa ni washirika wa LOWASSA, SLAA anajua?
 
Kazi ipo ,uelewa wetu ni mdogo sana na tumekaa kiushabiki tu wa vyama,hapa Chadema inaingiaje?waliozungumziwa ni Magufuli na Lowassa sasa hilo la Chadema limeingiaje hapa,nadhani wewe ndio wale wa ''zidumu fikra za mwenyekiti''na kuitikia zidumu hata pale fikra zake zikiwa za hovyo,tumia akili kufikiri kama wewe kwanza acha porojo za vyama,tujadili watu binafsi wanaoutaka uraisi,bila kujalisha ni Chadema,CCM,au CUF.Wakati mwingine uwe kwanza unasoma kilichoandikwa kwanza kabal ya kuanza kuiota tu Chadema.
Chadema imeingia baada ya kutajwa neno dikteta ambalo linawanusu sana viongozi wa CHADEMA
 
Kwani lazima watu hao hao wawe viongozi.Je wengine hawawezi.Ni wakati sasa wa kubadilisha MINDSET zetu au tutakwenda kwenye utawala wa kifalme
Hapo sasa ndiyo maana mimi simpendi kabisa lowasa hata kumsikia mwizi yeye,fisadi yeye,visasi yeye halafu watu wanataka awe kiongozi Ebo!
 
Chadema imeingia baada ya kutajwa neno dikteta ambalo linawanusu sana viongozi wa CHADEMA
Chadema kila mtu anafahamu kuwa ni chama cha kidikteta kwa mda mrefu na ndiyo msingi wake haswa.
 
Kwa hiyo ni Rais wa Wachafu Vs Rais wa Wakurupukaji?

Ni Team RICHMOND Vs Team Kabula?
 
Hata mimi naungana na cybercrime, hakuna haja ya kuwataja, nyie jiandaeni mtakutana Oktoba.

Ha ha ha.. Haya tujiandae hiyo Octoba.. Ila ujue tuna faili la kila mtu huko ccm.. Ukiwaondoa wale wazee kama Warioba na Salim waliobakia wote hawafai..
 
Nyumba zetu kwanza, mambo mengine baadaye
 
Watanzania hatuna imani na Magufuli kabisa ni mtaka sifa na dikteta kila kitu anajue yeye tu,kwanza ni mbinafsi mno,aliamua kuipitisha barabara kuu ya Mwanza hadi Bukoba jimboni kwake Chato,aliamurisha michoro ya awali kuachwa na ichorwe michoro mipya ya barabara itakayopitia jimboni kwake baada ya jimbo lake la awali kugawanywa na yeye akaamua barabara ipite liliko jimbo lake jipya.
hapo wala sioni kama ni ubinafsi, kwani wafaidikaji wakuu ni wananchi wanayotumia barabara hiyo, yeye ukimuita mbinafsi kwa kujenga barabara ambayo imewanufaisha wananchi moja kwa moja na sio kuwa ni wa jimbo lake tu, kwani inatumika kwa wakazi wote wa bukoba, na hao wanaokula pesa wao na familia zao tuwaiteje? mala hiyo milioni kumi niliitumia kwa mboga!! huyo lowasa kwa ufisadi wote alioufanya ni tajie hata sehemu moja ambapo wananchi wamefaidika nao? kama sio hadi leo ndio unatutafuna kwenye sekta ya umeme?? hata kama magufuli ana mapungufu yake lakini yamzidi lowasa na ndio tishio kubwa kwa kambi ya lowasa ni huyu. we uwe kambi moja na kina chenge, rostam, kalamagi kuna nini hapo?!!! serikali itakuwa ya genge la MAFIA.
 
Back
Top Bottom