Dkt. Magufuli aibomoa ngome ya Lowassa

Dkt. Magufuli aibomoa ngome ya Lowassa

Attachments

  • 1425377076710.jpg
    1425377076710.jpg
    42 KB · Views: 506
Nyoka wa Makengeza anaweza kuwasaidia CCM maana ndio mpiga dili mwenzao nayekubalika mpaka akatunga katiba.
 
ccm mkilogwa mkampendekeza lowassa achukue fomu ya urais mmeumia.
 
Naomba kuuliza kwanini lowassa anatumia mabilioni kuutaka urais?je atarudishaje fedha zake?
 
Bora wameanza kubomoana wenyewe kwa wenyewe kabla hawajakumbwa na mafuriko ya UKAWA.
 
Wewe mwenyewe mleta mada upo kundi lipi, na je tukusaidieje ili mambo yakunyokee?
 
hapo wala sioni kama ni ubinafsi, kwani wafaidikaji wakuu ni wananchi wanayotumia barabara hiyo, yeye ukimuita mbinafsi kwa kujenga barabara ambayo imewanufaisha wananchi moja kwa moja na sio kuwa ni wa jimbo lake tu, kwani inatumika kwa wakazi wote wa bukoba, na hao wanaokula pesa wao na familia zao tuwaiteje? mala hiyo milioni kumi niliitumia kwa mboga!! huyo lowasa kwa ufisadi wote alioufanya ni tajie hata sehemu moja ambapo wananchi wamefaidika nao? kama sio hadi leo ndio unatutafuna kwenye sekta ya umeme?? hata kama magufuli ana mapungufu yake lakini yamzidi lowasa na ndio tishio kubwa kwa kambi ya lowasa ni huyu. we uwe kambi moja na kina chenge, rostam, kalamagi kuna nini hapo?!!! serikali itakuwa ya genge la MAFIA.

Na wale walioikosa ambao ndio walikusudiwa je haki ipo wapi?hapa tunazungumzia haki ,hakuna aliyebora au na afadhali pamoja na huyo Magufuli wote ni mafisadi tu,hana cha afadhali hata chembe wote ni ndege wa aina moja,halafu watu mnavyochekesha nikuwa kwa mfano kwa kumsema Magufuli basi mtu yupo kambi ya Lowasa au kwa kumsema Lowasa basi mtu yupo kambi ya Membe au Muhongo,kueni bana haya mambo ya kambi sio kila mtu anahusika,mumeanza ujinga wa kuwasema watu ambao wako against na watu mnaowataka kuwa wapo kambi fulani au chama fulani,wengine hatuna vyama wala kambi tunachosema ni kile tunachokiona,nadhani ndugu wewe ni mgeni humu JF,jaribu kupitia nyuzi zangu ndio utajua mimi ni mtu wa sampuli gani.
 
CCM ikisimamisha rais mwingine ya JP Magufuli au S. Sitta, basi ikae tayari kukabidhi mikoba ya Administration kwa Upinzani
 
Watanzania hatuna imani na Magufuli kabisa ni mtaka sifa na dikteta kila kitu anajue yeye tu,kwanza ni mbinafsi mno,aliamua kuipitisha barabara kuu ya Mwanza hadi Bukoba jimboni kwake Chato,aliamurisha michoro ya awali kuachwa na ichorwe michoro mipya ya barabara itakayopitia jimboni kwake baada ya jimbo lake la awali kugawanywa na yeye akaamua barabara ipite liliko jimbo lake jipya.

Magufuli ana akili sana alifupisha njia ya kutoka mwanza hadi bukoba kiasi leo mtu unaweza kwenda bukoba na kurudi mwanza kabla jua halijatua,mpeni nafasi awatumikie watz.
 
Naona wanapingana na ile dhana yao ya kusimamisha mgombea Wa kike
 
ccm mkilogwa mkampendekeza lowassa achukue fomu ya urais mmeumia.

Sisiem walimtosa Lowassa, CDM wamempokea na kumpatia fursa ya kugombea urais kwa mwamvuli wa UKAWA, je, CDM na UKAWA nao wameumia? Naomba jibu lako fasta!
 
Magufuli kuibomomoa ngome ya aliyewahi kuwa bosi wake ni ngumu sana. Kitendo cha kusalitiana ndani ya ccm kitawamaliza kabla ya october kwani watahama wengi au kuendesha uasi wakiwa ndani ya chama. Kumbukeni kuwa hakuna dhambi na adui mbaya kama unafiki. Ni wachache sana walio ndani ya ccm wenye dhamira na mapenzi ya kweli na chama hicho kwani walio wengi walimpenda na kumwamini Lowasa kama rais wao na atakayeweza kuya-balance makundi yanayoasimiana ccm. Wengi watamfuata UKAWA na au watampigia kampeni za chinichini ili ashinde. Ccm ijiandae kushindwa kwani hata mwenyekiti wao alishawatabiria hilo badiliko.
Suala la ufisadi halina mashiko kwa sasa kwani kiukweli liliasisiwa na kulelewa ccm na moja ya nguzo kuu za ccm ya leo kuwa kama wewe siyo fisadi basi ni mpinzani wao. Ccm bomokeni mkajiumbe upya!
 
Back
Top Bottom