Mala ya kwanza kumfahamu Dr huyu ni mwaka1977- 1979 mwishoni tulikuwa nae Mbeya M.TC,akisoma course ya Clinical Oficer (C.O) zamani waliitwa Medical Assistant, Kule chuoni Mbeya alikuwa anaitwa
Lunyalula Kidola na alikuwa Rais wa chuo.
Baada ya kumaliza kozi kilamtu alitawanyika kivyake kwenda kujiunga na JKT na baadae kuajiliwa kazini.
Baada ya kumaliza tu tulikutana nae Dar mitaa ya Uhuru akiulizia bei ya godoro mikononi alikuwa ameshikilia bahasha nadhani ndani kulikuwa na vyeti akaniambia anaenda wizarani kushughurikia scholarship yake anakwenda URUSI.
Baadae nilisikia alienda kusoma Urusi degree ya Medicine. Hatukuonana tena hadi miaka ya 2000 nilianza kukutana nae mitaa ya Dar,kila tukionana nae alikuwa ananiambia mambo ya kuwa na hela nyingi na biashara lakini nilianza kumtilia mashaka kwani mambo aliyokuwa ananiambia hayakuwa yanafanana na muonekano wake,fedha nyingi alizosema alikuwa nazo zilikuwa hazifanani na yeye , basi kila alipojitahidi kuniongelesha nilikuwa ninampuuza.
Pia alikuwa amekatika vidole na meno mengine alikuwa hana vitu vyote hivi vilikuwa vinanipa mashaka.
Tukaacha kuonana nae hadi hapo jana nilipomwona kwenye mitandao na leo kwenye magazeti.
Kifupi huyu jamaa alienda kusoma Urusi kozi ya udakitari sina uhakika kama alimaliza maana kila ukimwuliza mambo mengi alikuwa anafichaficha, mfano anafanya kazi wapi hasemi mala lectural Aghakan University ukienda huko humkuti n,k. Kuna jamaa anamfahamu zaidi anaitwa Dr, Edward Maswanya yuko pala NIMRI.
Kabila lake ni msukuma.