Nimeguswa sana na tukio la kushikiliwa na vyombo vya dola mtu anayetajwa kama Dr Louis Shika (pichani).
Ukiacha tukio lilivyo, mtu huyo ninamfananisha sana na "SHIKA LUNYALULA KIDOLA" mzaliwa wa kitongoji cha CHAMUGASA kijiji cha KALEMELA wilaya ya BUSEGA, Simiyu.
Shika ninayemfahamu, yeye na ndugu yake JEREMIAH KIDOLA walikuwa wanafunzi wa vyuo vikuu huko USSR (Urusi ya zamani) kwenye miaka ya 1970 & 1980. Nakumbuka kama siyo wote lakini Jeremiah ambaye ni marehemu alisoma udaktari na kuwa miongoni mwa madaktari bingwa wa Bugando Hospt Mza, binafsi ninazaidi ya miaka 39 bila kuonana na Shika, ingawa ilijulika mapema kuwa alioa mke wa kirusi na baadaye kuzama kwenye ulevi wa pombe za kupindukia huko Urusi.
Mwaka juzi nilikutana na mgodo wao Daudi aishiye kijiji cha Mwamanga - Magu. Akanijulisha, kuwa, SHIKA alisharudi Tanzania lakini alidai akili zake hazina utimamu tena, huku akinipa mifano:-
1). Ana zaidi ya miaka 10 tangu arudi nchini lakini kila siku "anadai kusubiri mizigo yake kutoka urusi ifike bandarini, pia alikuwa hajui kwa nini imechelewa kufika" hali ambayo ilidaiwa kumsababishia SONONA kubwa sana.
2). Ilikuwa zaidi ya miaka 12 tangu Baba yao mzee Lunyalula Kidola afariki dunia, lakini hakuwahi kufika msibani licha ya Shika kuwepo Dar es Salaam.
Kifupi, nimeguswa sana na jina la SHIKA pia sura yake kama mtu ninayemfahamu vizuri tangu tukiwa majirani kijijini wakati huo Shika na Jeremiah wakisoma darasa moja kwenye s/m Chamugasa pamoja na dada yangu mkubwa "Magdalena", hivyo, sura hii ndiyo sura pia ya mdogo wake aliyeko kijijini Chamugasa aitwaye Pius, Je, nimemfananisha kwa uhakika au kimakosa?, tuuachie wakati uamue.
2. Said Lugumi ni mzaliwa wa Magu, Busega na Magu siyo kama ni maeneo jirani tu, bali zamani ilikuwa wilaya 1, je, kuna nini nyuma ya Dkt. Louis Shika kupitia uuzwaji wa majengo ya Lugumi?, Ni utapeli?, Ni shida kali au kuna nini hapa?
Naamini vyombo husika viko kazini, tunasubiri majibu.