yusuphfrancis
JF-Expert Member
- Oct 26, 2016
- 433
- 361
Ni kweli mkuuUsichokijua ni bora tu kukaa kimya. Una uhakika gani kuwa hizi allegations zako TISS walikuwa hawazifahamu?
Una uhakika gani kuwa TISS hawakushauri lolote kabla ya haya kutokea?
Tanzania tuna bahati ya kuwa na taasisi imara. Hata wewe wakiamua kudeploy resources na kukufikia usiku huu wanakupata.
Usiku mwema!!
Akina Chenge, Ndugai na wengine waliotuingiza mkenge kwa mikataba mibovu wote walipitia JKT
Wametusaidia nini hao zaidi ya kututia hasara?
Uzalendo ni tunda la haki siyo kwata
Usichokijua ni bora tu kukaa kimya. Una uhakika gani kuwa hizi allegations zako TISS walikuwa hawazifahamu?
Una uhakika gani kuwa TISS hawakushauri lolote kabla ya haya kutokea?
Tanzania tuna bahati ya kuwa na taasisi imara. Hata wewe wakiamua kudeploy resources na kukufikia usiku huu wanakupata.
Usiku mwema!!
Nadhan lawama zinapaswa kwenda ubalozi Kwetu south
Na sio hao unaowasema
Sidhan hivyo Ila kama Unataka kuleta ujuaji kwamba unaifahamu kiundani sawa pia
Nyote wawili mnazungumzia kitu kimoja.
Kwanini TISS 'inadeploy resources' kuwafikia Wapinzani wa CCM na wanaomsema JPM wakati inashindwa 'kudeploy resources' kulinda maslahi ya Taifa mpaka ndege inakamatwa Afrika Kusini?
Au unasema TISS walijua wakakaa kimya?
Kwa mara ya tatu tena nakuandikia Mzee wangu Dr Modestus Kipilimba, mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa taifa, TISS.
Natamani sana, Rais Magufuli awe wa kwanza kusoma hii mada kabla yako.
Nimeshindwa kuendelea na kazi niliyokuwa naifanya usiku huu kwenye Computer, moyo wangu umekosa amani kabisa hadi niandike hii mada.
Dr. Kipilimba, unadhani bado unastahili kuongoza Idara nyeti na muhimu Kama hii ya TISS?
Kwanini mikononi mwako serikali ya awamu ya tano inadhalilika sana kimataifa?
Kwanini Idara yako imeruhusu uwepo wa watu Kama Musiba wanaokashifu viongozi wakubwa hadharani?
Sikufundishi kazi, ila nashangaa kwanini hujui kuwa idara kama TISS ndo Roho kamili ya Tanzania.
Kifo cha TISS ni kifo cha Tanzania, kwanini hujifunzi magumashi ya CIA, MI5, Mossad na mashirika mengineyo kama TISS?
Ninaposema magumashi nadhani umeelewa vizuri kabisa, maana nikielezea itahitaji kitabu.
Uimara wa TISS ndo Uimara wa Tanzania, na udhaifu wa TISS ndo udhaifu wa Tanzania.
Tunajua ya kwamba dawa ya Deni ni kulipa, lakini ilikuwaje TISS ikashindwa kubaini kuwa Steyn kafungua shauri mahakamani dhidi ya Tanzania kudai mali yoyote ya nchi ikamatwe?
TISS ingeitaarifu serikali basi, ndege isingeenda SA, na hivyo wangetafuta namna nyingine ya ku-solve tatizo.
Ni aibu kubwa mno nchi kudaiwa na raia mmoja Halafu mali ya nchi kukamatwa kwa Deni nje ya nchi, hii fedheha kubwa.
TISS mngeweza kuepusha hii fedheha. Kama TISS, ilishindwa kubaini njama za kutaifisha mali ya nchi, je itaweza kujua nini kinapangwa Somalia na Alshabab kwa mfano juu ya nchi?
Dr Kipilimba, TISS chini yako ni dhaifu mno, nakushauri u resign tu. TISS chini ya Dr Hansy Kitine na hayati Imran Kombe ilikuwa imara kupindukia.
Nakumbuka Tukio moja (siwezi kulitaja) nilikuja kushtuka mission accomplished muda mrefu kumbe yule jamaa alikuwa TISS na akapotea kama jini.
TISS ya leo imejaa vijana wa UVCCM, wasiojua lolote kuhusu intelligence wala miiko yake. Idara hii imegeuzwa kuwa ya kisiasa ili CCM itimize ndoto zake za alinacha za kutawala milele. Inashangaza sana, yaani Idara haikuweza hata kuzuia maandamano ya kuharibu Diplomasia yetu na SA.
Watumishi wa Idara hii wanatakiwa wawe wafia nchi (wazalendo kweli kweli) siyo wafia CCM au CHADEMA.
CCM itakufa, CHADEMA itakufa, lakiniTanzania ipo tu!
Ok! Say walikuwa, matokeo ndio haya tunayaona????Usichokijua ni bora tu kukaa kimya. Una uhakika gani kuwa hizi allegations zako TISS walikuwa hawazifahamu?
Una uhakika gani kuwa TISS hawakushauri lolote kabla ya haya kutokea?
Tanzania tuna bahati ya kuwa na taasisi imara. Hata wewe wakiamua kudeploy resources na kukufikia usiku huu wanakupata.
Usiku mwema!!
Kuna watu wanamaliza Form 4 na miaka 14 hadi 16 maana yake ni underage. Serikali haiwezi wapeleka hukoHebu waambieni hao walio against Government kwa sababu tu ya kubwanwa maslahi wajitafakari. Uzalendo kwanza. Actually JKT ingerudi tena ianzie form 4 maana kuna kizazi kwa kweli kinatishia amani ya nchi!
Uzalendo hautafutwi JKT bali ni matokeo ya haki katika taifa.Ndo uko sawa kabisa JKT inapaswa kurudi kisawasawa na mimi napendekeza vijana wakae kambini kwa miaka miwili.
Hii wanafanya Israeli na Korea Kusini na baadhi ya nchi zingine.
Hii itasaidia watu kushika moyo na kuonyesha wanaipenda nchi yao na wako tayari kuitumikia "no matter what".
Hata kama kuna kiongozi ambae na kasoro zake lakini linapokuja suala la ndege kuzuiwa nchi nyingine khasa ndege mpya watanzania wanaungana pamoja kutafakari juu ya mstakabali wa mali hiyo ya taifa.
Marekani pamoja na Donald Trump kufanya anayofanya lakini wakaikung'uta Syria kwa mabomu na sasa wanaishughulikia Iran na Korea Kaskazini, hiyo yote ni kwa "maslahi ya taifa" hilo.
Unafahamu hata nchi zilizoendelea likija jambo la "kwa maslahi ya taifa" wanageuka na kuunga mkono, hayo utaona kwenye televisheni, radio na magazaeti.
Masuala kama ya ugaidi na kutishia usalama wa mataifa yao wanaweza wakayaongelea kwa siku kadhaa masaa 24 na ukijaribu kubadilisha chennels habari ni hizohizo mpaka kieleweke mbele ya wananchi.
Viongozi mbalimbali, wasomi na watu wengine wa kada mbalimbali kwenye jamii wataitwa kwa interviews.
Sisi Tanzania kuna kitu kimeharibika ndani ya miaka 20 ilopita na tunapaswa kujitafakari na kujifunza uzalendo na kulinda maslahi ya taifa.
Waandishi hawajaanza leo kuikosoa TISS,; mimi Nafanya marudio tu, magazeti ya Mwanahalisi na Mawio, yalifutwa kwa sababu ya kuikosoa TISS, Azori Gwanda, Ben Saanane, Kanguye nao wamepotezwa na TISS, Tundu Lissu alipigwa risasi na TISS.Ushauri wako haulengi kuondoa chanzo cha tatizo, ubovu wa TISS haujaanzia kwa Dkt. Kipilimba, mbona wakati nchi inafisidiwa kupitia kagoda mpaka escrow hamkusema TISS wanafanya nini?? hii ishu ndogo ya ndege inalingana na aibu ya watu kugawana pesa za nchi kwenye mifuko tena mitaani?? benki ndio zilikuwa kichaka cha kuficha uhalifu na TISS wapo, kuna aibu kubwa kushinda hizo??Kipilimba amerithi TISS mbovu..laumu waliokuwepo kabla yake!
Unazidi kuonyesha umbumbumbu wako humu, pathetic kabisa wewe.Ni kweli mimi hakuna ninalolijua kuhusu TISS sababu mimi sio mtumishi wa idara hiyo.
Afadhari mimi najitambua sijui kuhusu TISS kuliko wewe unajinasibu unajua kuhusu TISS na intelijensia kiujumla huku unaongea usiyoyajua.
Huyo anaekupa hadithi anakulisha matango pori tu, hamna kitu hapo.
Mkuu idara ya usalama wa taifa ikishindwa jambo lolote ujue hakuna tena nchi salamaMkuu shikamoo, nimesoma posti yako inaharufu ya utuuzima na busara fulani hivi zilizopitwa na wakati!!! Eti unatamani rais awe wa kwanza kulisoma hili!!!
Labda hulijui hili " U can't swim against the current". Sio Dr Kipilimba pekee wako mawaziri, makatibu, makamishna, wakurugenzi, mabalozi wanaoshindwa kama nansvyoshindwa Dr.
Nakuonea huruma, looh, endapo kama ungejua!!
Acha mimi niishie hapa, ili nisije nikasema na visivyotakiwa kusemwa.
Wewe m.pumbavu usiejua hata kuandika na wewe ni "think tank" ya TISS?Wewe tafuta pesa kwa njia halali, usibeze Tiss kwa kukuharibia shughuli zako haramu, kama akaunti ina pesa haramu ni wajibu wao kuifunga hata kama kufanya hivyo hakutaboresha uchumi!
Well said!.wanadhani kila anayeshauri humu ni CHADEMA. Wengine wapo nao humo humo ofisini ila hawataki ujinga.Tatizo lenu mna uwezo mdogo mno wa kufikiria ,unajuaje Kama na mimi nimeiva ktk masuala ya intelligence?
Halafu ni wapi nimetukana zaidi ya kushauri?
TISS haiko imara ,ni kichaka cha CCM kufanya upumbavu wao.
Tungekuwa na TISS imara, hata uchumi ungekuwa imara, kwa sababu kazi za Taasisi Kama TISS ni kuhujumu mataifa mengine kwa maslahi ya nchi na siyo kuhujumu vyama vya siasa.
Ningeandika mazito ila namwonea huruma Melo watamtesa bure, hapa mbona nimeshauri tu, nikiweka nondo nzito hadi ikulu watapoteana.
Wewe kula ukalale huna unalojua, Tuachie sisi wanaume tuikosoe serikali.