Dkt. Kimei na Spika Ndugai, watoto wenu mliwasomesha ufundi simu?

Mhe. Kimei, Mbunge wa Vunjo, amekosoa vikali mazoea ya kutukuza elimu ya "ma degree na ma PhD," akidai yanapotezea watoto muda.

Hoja iliyoungwa mkono kwa nguvu na Spika Ndugai aliyelitaka bunge limsikilize Kimei kwa makini, na akamwongezea muda arudie na asisitize hoja yake.

Badala yake watoto wasomee "ujuzi" kama vile ufundi simu na umakenika, wanasema Kimei na Ndugai.

Najua mtoto mmoja wa Ndugai alimleta bungeni akasema anasomea udaktari China. Wa Kimei sijui.

Ningependa kujua, watoto wao waliwasomesha ufundi simu?

Au mnataka tu kuingiza mikenge watoto wa watu ili wawatengenezee watoto wenu system charge za simu zao?

Ili wabaki kuwa wao lazima watengeneze kundi la watu wa chini
IMG_3738.jpg
 
Una degree ya Mining Engineering basi unarudi kuwa mhadhiri na hata hujapitia kozi ya ualimu. Hivyo 'Pedagogy skills unazitoa wapi?
Niliwahi kuhoji suala kama hili;

 
Vyuo vya ufundi viwe vingi kila mkoa yaani tutatengeneza bonge la taifa kama china kutakuwa na wajuzi wengi na ushindani mkubwa na ugundunduzi wa vitu mbalimbali baada ya miaka 20 tutawapiku wachina sana tu
 
Ndo maana wanataka mitaala ibadilishwe.
Yaaani mtoto akitoka form 4 au 6 au chuo.
Awe na ujuzi wa ziada.
Hata akikosa ajira ujuzi wake anao utamsaidia.
Ujuzi utamsaidia vp wakati hakuna ajira/pesa mitaani? Kama hakuna pesa mtaani hata kama mtoto ana ujuzi wa umeme atafanya wiring nyumba ya nani wakati watu hawajengi? Hata kama wapo wachache wanaojenga hao mafundi umeme au welding wapo wangapi hapo mtaani? Mwenye shibe hawezi kumkumbuka mwenye njaa hata siku moja mkuu.
 
Watoto wenu wakasome ufundi simu ili waweze kupata matonge kwa sababu baba zenu hawana pesa. Watoto wa Kimei na Ndugai wao wataenda kusomea usimamizi wa fedha kwa sababu baba zao wanazo nyingi Sana.
Kwa kiingereza wanasema "it's survival of the fittest" mwenye nacho atazidi kuongezewa
 
Wao wanawapeleka ufundi watoto wao? Au wanataka na vizazi vyao ndiyo wabaki kutawala milele!
 
Alikuwa na point. What is the use 7 yrs Primary School+6 yrs Secondary School+ 2-5 yrs tertiary education. Na chuoni mtu anasoma BA Caltural Heritage, B.A Tourism, BA. Linguistics and the likes. Anakuja mtaani hakuna ajira anaishia kuwa boda BODA, kondakta wa basi.

Matumizi mabaya ya muda na rasilimali akili.

Maoni yangu:
1. Mfumo wa elimu urekebishwe miaka ipunguzwe i.e primary school 5 yrs secondary 3 to 4 yrs, e.t.c
2. Mkazo uwe kwenye vyuo vya kati. Basically middle income economy kwa kiasi kikubwa inaendesha na mafundi mchundo na mafundi sanity.
Naunga mkono hili
 
Wa-tanzania naomba sana wamsikilize Mh. Kimei anajua nachokiongea, huyu hajawahi kuwa mwanasiasa. Ana practical ya kila anachokisema. Bora watu watoe hoja kuwa hawamwelewi ili atoe ufafanuzi zaidi, lakini siyo kumpinga. Naomba sana kwenye Bunge hili hii miaka mitano, tumsikilize kwa makini sana huyu mtu kila anachoongea
Sio lazima mkuu.
 
FUNDI HAJAWAHI KUKOSA KAZI.
Ujuzi utamsaidia vp wakati hakuna ajira/pesa mitaani? Kama hakuna pesa mtaani hata kama mtoto ana ujuzi wa umeme atafanya wiring nyumba ya nani wakati watu hawajengi? Hata kama wapo wachache wanaojenga hao mafundi umeme au welding wapo wangapi hapo mtaani? Mwenye shibe hawezi kumkumbuka mwenye njaa hata siku moja mkuu.
 
Lazima tufanye root cause analysis. Mfumo wa elimu yetu ni mbovu. Tuanzie hapo.

Mbona yeye ni Dr. Kimei na amefanikiwa? Elimu yetu iwe inafundisha life skills na independent thinking. Graduate anafanya interview - akiulizwa swali utadhani ni text book! Kukaririshwa na kupasi mtihani siyo elimu.

Una degree ya Mining Engineering basi unarudi kuwa mhadhiri na hata hujapitia kozi ya ualimu. Hivyo 'Pedagogy skills unazitoa wapi?
Nijuavyo kuna tofauti kati "teacher" na "instructor"!

Huyo mtu wa mining anakua instructor na sio teacher.
 
Back
Top Bottom