Dkt. Kigwangalla hebu tujuze haya kuhusu mtoto Getrude Clement

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
1. Je, kabla ya mtoto Getrude Clement kwenda kuhutubia Umoja wa Mataifa ulikuwa unamjua? Wizara yako ilikuwa inamtambua?

2. Je, ulienda kumuaga kabla hajaenda? Ulikuwa unajua anaenda? Au ndio tabia zile zile za kutambua mchango wa mtu baada ya kufa? Wewe umetambua uwezo wake baada ya kurudi!!

3. Je umejua lini kwamba baba yake ni kinyozi na mama yake ni mfanyabishara ndogo ndogo?

4. Sasa kwa nini Foundation yako ndio itamlipia ada ya Form 5 na 6 badala ya Wizara yako?

5. Unasema utampeleka shule ya kisasa kwani mbona kwenye shule ya kata aliyosoma amefikia hapa ulipomkuta? Unadhani kwanini asiendelee shule ya kata? Wengine waendelee huko kwanini?

6. Je, huyu ni mtoto pekee mwenye kipaji? Wizara yako ina utaratibu gani kuwatambua na kuwaendeleza watoto wenye vipaji? Au ndio Foundation yako itafanya?

7. Hujasema lolote kuwapongeza wazazi wala kuwatia moyo wazazi wengine. Huoni mchango wa wazazi?

Tuache kufanya maamuzi kwa matukio. Hakuna sustainability wala matokeo yenye tija. Ndio maana inaweza kuonekana ni maigizo au kutafuta political mileage.

Tunategemea taarifa rasmi inayojitosheleza kutoka Wizara yako na sio post FB au kwenye social media. Watoto wako wengi. Huyu sio wa kwanza au wa mwisho.

Hongera sana Getrude Clement pamoja na Wazazi wako, Walimu wako na wote waliokusaidia kufikia hapa. Mungu akubariki.M
 
Ila sisi watz watu wa ajabu sana hivi mwanaume mzima unahoji matumizi ya hela ya mwanaume mwenzio.pumbafu tafuta hela acha majungu
 
Viongozi wetu siku zote huwa hawana macho....wanaona tu pale wanapooneshwa..
 
  • Thanks
Reactions: 999
1. Je, kabla ya mtoto Getrude Clement kwenda kuhutubia Umoja wa Mataifa ulikuwa unamjua? Wizara yako ilikuwa inamtambua?

2. Je, ulienda kumuaga kabla hajaenda? Ulikuwa unajua anaenda? Au ndio tabia zile zile za kutambua mchango wa mtu baada ya kufa? Wewe umetambua uwezo wake baada ya kurudi!!

3. Je umejua lini kwamba baba yake ni kinyozi na mama yake ni mfanyabishara ndogo ndogo?

4. Sasa kwa nini Foundation yako ndio itamlipia ada ya Form 5 na 6 badala ya Wizara yako?

5. Unasema utampeleka shule ya kisasa kwani mbona kwenye shule ya kata aliyosoma amefikia hapa ulipomkuta? Unadhani kwanini asiendelee shule ya kata? Wengine waendelee huko kwanini?

6. Je, huyu ni mtoto pekee mwenye kipaji? Wizara yako ina utaratibu gani kuwatambua na kuwaendeleza watoto wenye vipaji? Au ndio Foundation yako itafanya?

7. Hujasema lolote kuwapongeza wazazi wala kuwatia moyo wazazi wengine. Huoni mchango wa wazazi?

Tuache kufanya maamuzi kwa matukio. Hakuna sustainability wala matokeo yenye tija. Ndio maana inaweza kuonekana ni maigizo au kutafuta political mileage.

Tunategemea taarifa rasmi inayojitosheleza kutoka Wizara yako na sio post FB au kwenye social media. Watoto wako wengi. Huyu sio wa kwanza au wa mwisho.

Hongera sana Getrude Clement pamoja na Wazazi wako, Walimu wako na wote waliokusaidia kufikia hapa. Mungu akubariki.M
Kuna ubaya gani Kigwangalla kumsomesha huyo binti,sina hakika kama umeachiwa hata akili ya kuvuka barabara...aliyekushikia akili kakuweza.
 
Nakumbuka kifo cha kamanda MAWAZO,

Kinanikumbusha AHADI YA MTOTO WAKE KUSOMESHWA .... Mawazo .... mwalimu Mawazo...

Mtoto wake naye alikumbwa na ahadi ya kusomeshwa mpaka kiwango cha JUU sana
 
Back
Top Bottom