Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 8,943
- 25,284
Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Nzega Vijijini Dkt Hamis Kigwangalla ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Afya ya Jamii, apata chanjo yake ya corona, Sputnik Light, kutoka ya Urusi.
Dr. Kigwangalla aliwahi kupinga vikali matumizi ya chanjo katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona mnamo mwaka 2020 lakini alibadili msimamo wake mapema mwaka huu na kuhimiza upatikanaji wa chanjo dhidi ya virusi vya corona kama njia pekee ya kupambana na ugonjwa wa UVIKO-19 unaosababishwa na virusi hivyo vya corona.