Dkt. John Pombe Magufuli umelifaa taifa kisiasa na kiuchumi. Sasa ongeza kasi kudhibiti fedha za political vote

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
554
1,000
Dkt. John Pombe Magufuli, ni mwamba imara - umefanya mengi mazuri i.e utawala bora, uwajibikaji, miundombinu nk

Pamoja na hayo nashauri uangazie sana matumizi ya fedha unazotoa kwa ajili ya mfuko wa self help schemes or political vote. Kwa wasiozifahamu ni kuwa Serikali hutoa:-
(a). Fedha za maendeleo ya Jimbo kwa majimbo yote nchini - matumizi ya fedha hizi bado hayako wazi sana na ukaguzi wa matumizi yake hauna standard moja;

(b). Fedha za self help scheme tshs 20,000,000/=. Hizi hutolewa kila mwaka kwa kila Mkuu wa mkoa ili zichangie shughuli mbalimbali zilizoanzishwa na wananchi. Kama ikiwezekana fedha hizi zitolewe kwa maRC watakaozisimamia na kuzitumia vizuri. Wenye makandokando ya matumizi wanyimwe.

(c). Fedha tshs 5,000,000/= kwa kila DC kila mwaka. Hizi zinaonekana ndogo lkn kwa kuwa ni fedha za umma basi matumizi yake yamlikwe ili zifanye kazi tegemewa.

Sisemi kwamba zimetumika vibaya lkn kama tabia za binadamu zinsvyobadilika ni yumkini baadhi yao wakizitumia kununua maandazi, kulipa ada za watoto wao, kufanya matengenezo ya magari ya familia nk nk

Watanzania, hasa wanaccm wanakuunga mkono jitihada zako za kuliongoza taifa na kwa maamuzi magumu ufanyayo Mungu azidi kusimamia na kukuongoza.

Salaam za mwaka mpya wa 2021 mwema kwako na wasaidizi wako.
Mungu ibariki Tanzania!
 
KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
2,352
2,000
Hizo pesa mbona wengi hatuzijui halafu kwa nini zitolewe kwa Marc na maDc
 
Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
554
1,000
Hizo pesa mbona wengi hatuzijui halafu kwa nini zitolewe kwa Marc na maDc
Kama zilivyoitwa "self help scheme" - hutolewa kila mwaka ili zisaidie juhudi za maendeleo zilizoibuliwa na wananchi, au iwapo kuna matukio fulani yaliyotokea i.e shule ikiungua, wanafunzi wasiokuwa na uwezo, ujenzi wa misikiti/makanisa nk
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,401

Kwa jinsi serikali ilivyokuwa na bureacracy, usishangae 20m zikitumika kukagua matumizi ya 20m.
 
fyddell

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
7,217
2,000
Kama zilivyoitwa "self help scheme" - hutolewa kila mwaka ili zisaidie juhudi za maendeleo zilizoibuliwa na wananchi, au iwapo kuna matukio fulani yaliyotokea i.e shule ikiungua, wanafunzi wasiokuwa na uwezo, ujenzi wa misikiti/makanisa nk
Kwahiyo mkuu kwamfano katika mkoa husika hakuna juhudi zozote za maendeleo katika mkoa husika, je hizi fedha huwa zinarudishwa au ndio imetoka hiyo?
Pili he hizi fedha huwa zinatolewa in monthly basis au annual?
 
gTurn

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
486
500
acha upumbafu amelifaa vipi taifa kisiasa? hivi kichwani zimo kweli wewe.? unaijua siasa wewe? acheni ushabiki maandazi ndio maana africa ni kama mazezeta tuu kutokana na fikra zetu..
 
Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
554
1,000
Kwahiyo mkuu kwamfano katika mkoa husika hakuna juhudi zozote za maendeleo katika mkoa husika, je hizi fedha huwa zinarudishwa au ndio imetoka hiyo?
Pili he hizi fedha huwa zinatolewa in monthly basis au annual?
Zinakuwa kwenye bajeti za kila mwaka, hutolewa kwa mkupuo mmoja kupitia votes za kila mkoa

Juhudi za maendeleo zipo, hulka ya binadamu huwa maximization - hata hivyo hii haiwezi kuwa kwa wote
 
Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
554
1,000
acha upumbafu amelifaa vipi taifa kisiasa? hivi kichwani zimo kweli wewe.? unaijua siasa wewe? acheni ushabiki maandazi ndio maana africa ni kama mazezeta tuu kutokana na fikra zetu..
Unakwama sehemu, siasa kokote duniani haina kipimo kimoja kama biblia au kruani - siasa safi ni ile yenye tija kwa taasisi, na watu wake.

Mfano, Mbowe hutumia mbinu na mikakati kibao kubaki ktk nafasi ya uenyekiti wa taifa - uliza Sumaye jinsi wajumbe wake walivyofungiwa sehemu wasipige kura - uliza Zitto alivyotimuliwa eti anakisaliti chama - uliza akina Mdee walivyotimuliwa kisha kurudishwa chamani

Hatuipimi siasa ktk mlalo wa kiutukufu - tunaangalia mambo mengi mazuri yanayofaidisha watu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom