Uchaguzi 2020 Dkt. John Pombe Joseph Magufuli-Tunu itakayodumu kuwahi kutokea Tanzania

Elpaul

JF-Expert Member
Jan 19, 2018
331
250
Poleni na mihangaiko ya hapa na pale ya kutafuta mkate wa kila siku, Tanzania ni moja kati ya nchi iliyojaaliwa tunu kadha wa kadha na Muumba wa mbingu na ardhi, ukiachana na utajiri mkubwa tulionao kama Madini, Mito, Maziwa, Bahari,Mbuga za wanyama, Milima, Mabonde, na mengine mengi, Kuna jambo kubwa tunalojivunia ambalo ni AMANI, hii imekuwa ni kama alama ya taifa letu tukufu, Mungu Muumba azidi kutupa nguvu na roho zenye kuidumisha Amani hii.

Tanzania ni taifa lililotawaliwa na marais watano tofauti tofauti tangu tupate uhuru toka mikonono mwa wakoloni, Kila kiongozi aliyekabidhiwa taifa la Tanzania ni dhahiri alitawala kadri ya uwezo wake huku akijitahidi kuleta mabadiliko ya hapa na pale, Katika awamu ya tano Watanzania tulimpa ridhaa ya kuongoza nchi ndugu John Pombe Joseph Magufuli, Hata hivyo watanzania tuliowengi hatukuwa na uhakika kama ndugu JPM angeweza kuwa na uthubutu wa kujaribu mambo ambayo asilimia kubwa ya watanzania tulikuwa tukihisi ni mambo makubwa na hatuyawezi.

Mtanzania wa kipindi cha Jpm ni mtu ambaye angalau anajiona kumbe na yeye anaweza kuwa na uthubutu katika baadhi ya mambo na akawa chachu ya mabadiliko, katika kipindi cha Jpm tumeshuhudia viongozi katika sekta wakitakiwa kueleza mbele ya kadamnasi ya watanzania ni nini wanachofanya katika nafasi wanazopewa, tumeshuhudia wageni (watu weupe) wakitakiwa kueleza mbele ya watanzania eidha wanafanyaje kazi zao au ni lini watamaliza kutekeleza kazi walizokuwa wamepewa hapa nchini na mengine mengi ambayo tuliowengi tuliyashuhudia.

Watanzania tumeshuhudia Jpm akiuonesha ulimwengu kwamba watanzania ni watu wanaoweza kujitegemea kifikra katika mlipuko wa gonjwa la Covid-19 lililokuwa na kampeni za kuwataka watu kukaa sehemu moja, Jambo ambalo ni gumu kwa asilimia kubwa ya watanzania kwani ili mkono uende kinywani ni lazima watu wazunguke hapa na pale, katika hili janga tumeshuhudia mataifa yaliyoendelea yakitaka kutuuzia barakoa, Yakihimiza kupulizia famigation sehemu zenye msongamano lakini Jpm alipinga vikali kwani ni ujinga uliokuwa hauingii akilini.

Jpm na jopo lake walienda mbali zaidi kwa kupeleka sampuli za wanyama, ndege na matunda katika maabara iliyokuwa ikitumika kutoa matokeo ya Covid-19 Cha kushangaza baadhi ya sampuli hizo zilionekana kuwa na maambukizi ya Covid-19!! Jpm akasimama na watanzania kuendelea na maisha ya kawaida, Ndugu Jpm alishutuka baada ya takwimu kuonesha KENYA kuwa muuzaji kwa kiwango cha juu madini ya Tanzanite.

Licha ya Madini hayo kupatikana Tanzania pekee ulimwenguni!! Baada ya hatua kuchukuliwa chini ya Jpm, Matokeo watanzania tuliowengi tuliyashuhudia, Jpm hakuridhishwa na jinsi watanzania tulivyokuwa tukinufaika na mgao wa wasimamizi wa Migodi yote Tanzania yaani BARRIK. Jpm baada ya kuchukua hatua matokeo tuliyaona....., Yapo mengi tuliyoshuhudia chini ya Jpm na mengine twaweza kuyaongeza hapa..., Naomba kumalizia kwa swali Je, Dr. Jpm ni tunu kutoka kwa Mungu ambayo watanzania tutajivunia siku za usoni???
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,519
2,000
Uhuru wa mawazo, sio uhuru wa kuwaza, na uhuru wa kuwaza, sio uhuru wa mawazo.

Mleta mada sijui kama kaandika anachokiwaza na kukiamini.
 
Ajaye

Member
Sep 25, 2020
38
95

Ni tunu kubwa tena Sana tuu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom