Dkt. Gwajima D
JF-Expert Member
- Nov 28, 2015
- 602
- 3,982
BINTI ALIYEDAI ANAISHI NA NYOKA AJISALIMISHA KWA WAZIRI DKT. GWAJIMA
Aomba radhi, adai hajawahi kufanya hivyo alidanganya.
DAR ES SALAAM.
Itakumbukwa hivi karibuni ilienea video mitandaoni kupitia televisheni ya MBENGO TV ikionesha Binti mmoja aliyekuwa amebeba nyoka mkubwa huku akidai kwamba, hufanya naye mapenzi ili kupata fedha.
Kufuatia hali hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt. Gwajima , alichukua hatua ya kukemea kitendo hicho na kumtaka ajitokeze kuomba radhi kwa Umma na kuondoa taarifa hiyo mtandaoni kutokana na kukiuka maadili.
Baada ya mmiliki wa Mbengo TV, Tarzan Mustapha aliyeambatana na mtangazaji Lenny kuomba radhi Mei 11, 2024, walielekezwa kumtafuta binti huyo waliyemrekodi vinginevyo wachukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka sheria ya usajili wao kwa kushirikiana kupotosha jamii kwa habari za utapeli.
Leo 20 Mei, 2024 Binti huyo aitwaye Veronica Bernad Anton aliyekuwa amebeba nyoka huyo naye amejisalimisha kwa Waziri Dkt. Gwajima na kuomba radhi kama video inavyoonesha.
Waziri Dkt. Gwajima ameelekeza kutafutwa kwa mmiliki wa nyoka au ajitokeze mwenyewe kabla hatua za Serikali kumtafuta hazijaanza ambapo, itaongeza makosa yake ya kutotoa ushirikiano kwa Serikali.
Waziri Dkt. Gwajima ameiasa jamii ya wanahabari na wasanii kuachana na utapeli na mambo yote yanayochochea mmonyoko wa maadili maana akiwa Waziri mwenye dhamana na Jamii yenye makundi maalum hatafumbia macho uongo, utapeli na uovu huo.
MWISHO
NB; nawasihi wanajamii wote kuheshimu Sheria kwa maendeleo na ustawi wa jamii na kutunza maadili.
Pia soma: Epuka kusambaza maudhui yasiyo na maadili. Anayedai kumiliki nyoka na kushiriki naye tendo, ajisalimishe