Dkt. Florence Samizi akamilisha ziara yake jimboni Muhambwe kwa kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Baada ya ziara yake ya kutembelea Wananchi kwenye Vijiji mbalimbali Jimboni kwake kusikiliza na kutatua kero zao, Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Mkoani Kigoma Mhe. Dkt. Florence George Samizi alifanya mkutano wa mwisho wa kushukuru wananchi katika Kata ya Kibondo Mjini ambapo alishukuru Kata zote 19 na vijiji vyake.

Dkt. Samizi alitumia Mkutano huo pia kueleza Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Muhambwe kwa kudadavua mipango yote inayokuja ya Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa Wana- Muhambwe huku Wana- Muhambwe wakimshukuru sana Rais Samia na kumkaribisha Muhambwe.

#MuhambweKaziInaendelea
#DktSamizinaMaendeleo
#MwakaMmojawaRaisSamia

IMG-20220310-WA0031.jpg

IMG-20220310-WA0032.jpg

IMG-20220310-WA0033.jpg

IMG-20220310-WA0034.jpg

IMG-20220310-WA0030.jpg

IMG-20220310-WA0029.jpg

IMG-20220310-WA0028.jpg

IMG-20220310-WA0026.jpg

IMG-20220310-WA0027.jpg
 
Watu ni kama walikua hawajafika wengi labda tuone picha ya jioni wakati anamaliza mkutano
 
Safi Sana mh.Mbunge na mwana msimbazi kindaki ndaki kwa mara ya kwanza kibondo wamepata mbunge asiye na makuu asiye mjivuni na anayefikika muda wote namtabiria makubwa huko mbeleni
 
Naona unajipigia debe bi Samizi ila unatupiga fix kusema mbunge ana uwezo wa kutatua shida zote za wananchi
 
Hivi Halmashauri ya wilaya Kibondo inashindwa nini kukopa kupitia soko la hisa ili hapo ilipo community center, kijengwe kituo cha biashara chenye hadhi, chenye maduka ya kupangisha, ukumbi wa mikutano na ghorofa kadhaa zikodishwe?
... Mnakwama wapi wana muhambwe?.

Wekezeni kwenye ile stendi ya mabasi mtavuna pesa na kuachana na mtindo wa kuwa tegemezi.
 
Back
Top Bottom