Dk. Tulia asota Dodoma

Dk. Tulia asota Dodoma

Baada ya miezi sita, hii ni awamu mbovu zaidi kutokea so far
 
Tatizo kubwa la huyu Naibu Speaker ni kushindwa kusoma alama za nyakati,she's too mechanical unnecessarily!
Hivi ameshindwa kwa efforts zake binafsi kutafuta mentors(wenye uzoefu kwy hiyo nafasi yake)wakam-guide?au anaamini anajua each n everything, Poor Lady!
 
Mheshimiwa Tulia kaza uzi .usicheke na hiyo misukule kutoka UFIPA tena mwambie Speaker vikao vyote awe anakuachia wewe wasuse wasisuse vikao vinaendelea na mwisho wa siku watarejea kama ilivyo kawaida yao.
Mwendo kasi umewapumbaza
 
Kila anapokuwepo Dk. Tulia, UKAWA wanaondo na hata kusababisha protokali kuvurugika. Ni kwa kuwa, UKAWA wameweka msimamo wa kutoshirikiana ama kutoshiriki shughuli ambayo yeye (Dk. Tulia) anashiriki.
Hivi ndivyo ilivyotokea leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma muda mfupi baada ya Kasimu Majaliwa, Waziri Mkuu kumaliza kuzindua Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Baada ya Waziri Mkuu kumaliza hotuba yake na kufuatia zoezi la ugawaji vitabu vinavyoelezea mpango huo kwa ajili ya kujisomea katika taasisi na baadhi ya viongozi mbalimbali. Katika uzinduzi huo mshehereshaji aliyefahamika kwa jina moja la Mzee Mavunde, alianza kuita viongozi mbalimbali ili kuchukua vitabu kwa ajili ya taasisi ama makundi yao.

Ulipofika wakati wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwenda kuchukua kitabu kuwakilisha kambi hiyo, mshereheshaji alimwita mnadhimu mkuu wa kambi hiyo ambapo hakutokea. Baada ya kuonekana kwamba, hakuna anayejitokeza kupokea kitabu hicho, haraka haraka Steven Hillary Ngonyani,Mbunge wa Korogwe Vijijini maarufu kwa jina la Prof. Maji Marefu alichomoka moja kwa moja na kwenda kupokea kitabu cha mpango huo wa miaka 5 kwa niaba ya kambi ya upinzani bungeni.

Kitendo hicho kiliwafanya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao walikuwa ukumbini hapo pamoja na wageni wengine kuangua kicheko. UKAWA wamekuwa wakitoka bungeni pale Dk. Tulia anapoongoza bunge hilo. Hatua hiyo inatokana na malalamiko yao kwamba, kiongozi huyo wa Bunge anaendesha taasisi hiyo kwa kupendelea CCM.
Kweli? Mbona wanashiriki kuchukua malipo ambayo huyu Mwanamke wa shoka ameidhinisha ushiriki wao kwa mujibu wa kanuni?
Hawa wapumbavu hawakuwa na taarifa tu na muda huenda baadhi walikuwa wakivunja amri ya sita na wengine kwenye pombe. Wengine walikuwa wanafuata virungu vya polisi huko Kahama.
Kuvuja kwa pakacha ni nafuu ya mchukuzi. Kukosekana kwao hakukuharibu shughuli husika.
 
Kweli? Mbona wanashiriki kuchukua malipo ambayo huyu Mwanamke wa shoka ameidhinisha ushiriki wao kwa mujibu wa kanuni?
Hawa wapumbavu hawakuwa na taarifa tu na muda huenda baadhi walikuwa wakivunja amri ya sita na wengine kwenye pombe. Wengine walikuwa wanafuata virungu vya polisi huko Kahama.
Kuvuja kwa pakacha ni nafuu ya mchukuzi. Kukosekana kwao hakukuharibu shughuli husika.
Hela hazikandamizi demokrasia
 
Kila anapo kuwepo Dk. Tulia, Ndugai simuoni. Au naye kamsusa?

Uzinduzi wa daraja la kigamboni Dk. Tulia alikuwepo, Ndugai hakuwepo.

Mei mosi Dk Tulia alikuwepo, Ndugai hakuwepo

Leo uzinduzi wa mpango Dk. Tulia alikuwepo, Ndugai hakuwepo.

Kunani!!!!!!????
 
Sijaelewa ni kwanini Profesa Maji marefu akienda kuchukua kitabu kwa niaba ya wapinzanj; I am trying to join some dots here; juzi kupitia ITV alionekana akiomba swala hili lipatiwe ufumbuzi na sababu aliyoitoa ilikua nzuri sana; kwamba bajeti ikijadiriwa na wao ccm tu inakua hainogi kwasababu kila kitu kinaungwa mkono tu wakati serikali inachukuaga hata maoni ya wapinzani. Sasa kitendo cha yeye kwenda kuchukua kwa niaba ya upinzani inanipa shaka kidogo.
 
Kwa sasa Maji marefu ndio nshauri nkuu wa ukawa
 
Demokrasia bila kufuata taratibu ni vurugu. Mwanamke wa shoka ameamua kusimamia ufuataji wa kanuni za kidemokrasia.
Kanuni ipi wapinzani wamevunja shirikisha ubongo kutaka bunge live nikuvunja kanuni
 
Dr Tulia kila atapokuwepo UKAWA wataondoka! Nimesikia hata ikitokea sherehe au msiba akiwepo tu ukawa wataondoka na hakika hawamtaki! Ila yeye sababu ni robot asiye na busara atalazimisha tu akijua ametumwa kukandamiza demokrasia! Ni aibu sana pandikizi kuvuruga demokrasia!!
Hii ilitakiwa ifanyike kwa wale wote waliofanya maovu...ya kifisadi na tunawajua na tuna uhakika walifanya ingawa hawajatiwa hatiani na mahakama zetu.
 
Wakigoma na kuchukua posho ndo nitajua kweli wanauchungu na nchi yao, ila kama wanaendelea kuweka dole gumba kwenye karatasi za pesa ni wahuni tu kama wahuni wengine
 
Mwendo kasi umewapumbaza
We tokwa na povu tu kila sehemu ya mwili wako,wapumbavu ni wale waliokuwa wanadeki barabara ili fisadi lowassa apite,wapumbavu ni wale waliotoa ahadi kwamba fisadi asipoingia ikulu watakuwa tayari..kuuza line zao za mtandao wa Tigo.
 
Back
Top Bottom