Dk. Tulia asota Dodoma

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Kila anapokuwepo Dk. Tulia, UKAWA wanaondo na hata kusababisha protokali kuvurugika. Ni kwa kuwa, UKAWA wameweka msimamo wa kutoshirikiana ama kutoshiriki shughuli ambayo yeye (Dk. Tulia) anashiriki.
Hivi ndivyo ilivyotokea leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma muda mfupi baada ya Kasimu Majaliwa, Waziri Mkuu kumaliza kuzindua Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Baada ya Waziri Mkuu kumaliza hotuba yake na kufuatia zoezi la ugawaji vitabu vinavyoelezea mpango huo kwa ajili ya kujisomea katika taasisi na baadhi ya viongozi mbalimbali. Katika uzinduzi huo mshehereshaji aliyefahamika kwa jina moja la Mzee Mavunde, alianza kuita viongozi mbalimbali ili kuchukua vitabu kwa ajili ya taasisi ama makundi yao.

Ulipofika wakati wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwenda kuchukua kitabu kuwakilisha kambi hiyo, mshereheshaji alimwita mnadhimu mkuu wa kambi hiyo ambapo hakutokea. Baada ya kuonekana kwamba, hakuna anayejitokeza kupokea kitabu hicho, haraka haraka Steven Hillary Ngonyani,Mbunge wa Korogwe Vijijini maarufu kwa jina la Prof. Maji Marefu alichomoka moja kwa moja na kwenda kupokea kitabu cha mpango huo wa miaka 5 kwa niaba ya kambi ya upinzani bungeni.

Kitendo hicho kiliwafanya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao walikuwa ukumbini hapo pamoja na wageni wengine kuangua kicheko. UKAWA wamekuwa wakitoka bungeni pale Dk. Tulia anapoongoza bunge hilo. Hatua hiyo inatokana na malalamiko yao kwamba, kiongozi huyo wa Bunge anaendesha taasisi hiyo kwa kupendelea CCM.
 
Kila anapokuwepo Dk. Tulia, Ukawa wanaondo na hata kusababisha protokali kuvurugika. Ni kwa kuwa, Ukawa wameweka msimamo wa kutoshirikiana ama kutoshiriki shughuli ambayo yeye (Dk. Tulia) anashiriki.

Hivi ndivyo ilivyotokea leo katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma muda mfupi baada ya Kasimu Majaliwa, Waziri Mkuu kumaliza kuzindua Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Baada ya Waziri Mkuu kumaliza hotuba yake na kufuatia zoezi la ugawaji vitabu vinavyoelezea mpango huo kwa ajili ya kujisomea katika taasisi na baadhi ya viongozi mbalimbali.

Katika uzinduzi huo mshehereshaji aliyefahamika kwa jina moja la Mzee Mavunde, alianza kuita viongozi mbalimbali ili kuchukua vitabu kwa ajili ya taasisi ama makundi yao.

Ulipofika wakati wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwenda kuchukua kitabu kuwakilisha kambi hiyo, mshereheshaji alimwita mnadhimu mkuu wa kambi hiyo ambapo hakutokea.

Baada ya kuonekana kwamba, hakuna anayejitokeza kupokea kitabu hicho, haraka haraka Steven Hillary Ngonyani,Mbunge wa Korogwe Vijijini maarufu kwa jina la Prof. Maji Marefu alichomoka moja kwa moja na kwenda kupokea kitabu cha mpango huo wa miaka 5 kwa niaba ya kambi ya upinzani bungeni.

Kitendo hicho kiliwafanya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao walikuwa ukumbini hapo pamoja na wageni wengine kuangua kicheko.

Ukawa wamekuwa wakitoka bungeni pale Dk. Tulia anapoongoza bunge hilo. Hatua hiyo inatokana na malalamiko yao kwamba, kiongozi huyo wa Bungeanaendesha taasisi hiyo kwa kupendelea CCM.
Type maoni yako kuhusu naibu spika.
 
Dr Tulia kila atapokuwepo UKAWA wataondoka! Nimesikia hata ikitokea sherehe au msiba akiwepo tu ukawa wataondoka na hakika hawamtaki! Ila yeye sababu ni robot asiye na busara atalazimisha tu akijua ametumwa kukandamiza demokrasia! Ni aibu sana pandikizi kuvuruga demokrasia!!
 
Ni kama Slaa alivyogomea wakati wa kutangaza matokeo 2010,
Lakini mwisho wa siku akawa anashinda ikulu kunywa ghahawa.

Hiyo ndo SISIEM mbele kwa mbeeeeeeleeeeeeeeeeeeeee, hatunywi sumu hatujinyongi
Hata Watanzania wanaona CCM ya mwendokasi
 
Hicho kitabu wamegoma kuchukua lakini kesho utasikia wanauliza maswali kutokana maelezo ya kitabu hicho hicho.
Kwani wao wamegomea kitabu au huyo mgawa kitabu? Kwani chake hicho au cha taifa?
Kitabu kitajadiliwa sana na wenye uwezo wa kukijadili kwa kina ni wabunge wengi wa upinzani, wengi wa CCM hata kukisoma na kuelewa pengine hawafikii hata 15% ya idadi yao. Hilo hata serikali yenyewe inalifahamu
 
Back
Top Bottom