Dk Slaa: nina shaka na Uchaguzi Mkuu

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
4chadema-1-564x272.jpg
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.

Na Godfrey Kahango, Mwananchi

Jumatatu,Juni1 2015
Dk Slaa alitoa kauli hiyo juzi wakati akihutubia wananchi wa Mji wa Vwawa, mkoani Mbeya.
Lissu asema Dk Slaa ni Rais ajaye
Mbozi.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amedai kuwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, huenda usiwe huru na haki kutokana na sababu kadhaa, ikiwamo uamuzi wa Serikali kununua magari ya polisi zaidi ya 700 kwa lengo la kukabiliana na wapinzani.

Dk Slaa alitoa kauli hiyo juzi wakati akihutubia wananchi wa Mji wa Vwawa, mkoani Mbeya.
Alisema badala ya kutengeneza na kuboresha mazingira mazuri ya uchaguzi, Serikali inaonekana kujiandaa kupambana na wapinzani.

"Serikali imetumia dola 29 milioni kununua magari 700 ya polisi, yakiwamo yale maarufu kwa jina la ‘washawasha'. Haya yote wanataka yatumike wakati wa uchaguzi," alisema Dk Slaa.

Kuhusu vituo vya kuandikisha wapigakura wilayani hapa, Dk Slaa aliwataka mawakala kuwapa ushirikiano wananchi ili waweze kujiandikisha kwa wingi.

"Mawakala na viongozi wa Serikali, acheni kuwabagua wananchi kwa misingi ya ushabiki wa vyama vya siasa," alisema.
Alisema ubaguzi wa aina yoyote kwa misingi ya vyama haukubaliki na kwamba kila mmoja ana haki ya kujiandikisha.

Aliongeza: "Ubaguzi katika uandikishaji kwa kuwataja wananchi kwa majina ya vyama CCM, Chadema au CUF hautavumilika."

Akizungumzia wanafunzi wa vyuo vikuu na sekondari kupata haki ya kupiga kura, Dk Slaa alimtaka Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva kuwaruhusu vijana hao kupiga kura mahali popote kutokana na ukweli kwamba siku hiyo watakuwa maeneo tofauti na walikojiandikisha.

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mchungaji Stephen Kimondo alisema hivi sasa kuna mpasuko kati ya Serikali na wananchi wake ndiyo maana kila kukicha migomo na maandamano inazidi kutikisa.
Chanzo Mwananchi
 
Mbozi. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amedai kuwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, huenda usiwe huru na haki kutokana na sababu kadhaa, ikiwamo uamuzi wa Serikali kununua magari ya polisi zaidi ya 700 kwa lengo la kukabiliana na wapinzani.

MWANANCHI
 
“Serikali imetumia dola 29 milioni kununua magari 700 ya polisi, yakiwamo yale maarufu kwa jina la ‘washawasha’. Haya yote wanataka yatumike wakati wa uchaguzi,” alisema Dk Slaa.

Kuhusu vituo vya kuandikisha wapigakura wilayani hapa, Dk Slaa aliwataka mawakala kuwapa ushirikiano wananchi ili waweze kujiandikisha kwa wingi.

“Mawakala na viongozi wa Serikali, acheni kuwabagua wananchi kwa misingi ya ushabiki wa vyama vya siasa,” alisema.

Alisema ubaguzi wa aina yoyote kwa misingi ya vyama haukubaliki na kwamba kila mmoja ana haki ya kujiandikisha.

Aliongeza: “Ubaguzi katika uandikishaji kwa kuwataja wananchi kwa majina ya vyama CCM, Chadema au CUF hautavumilika.”

Akizungumzia wanafunzi wa vyuo vikuu na sekondari kupata haki ya kupiga kura, Dk Slaa alimtaka Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva kuwaruhusu vijana hao kupiga kura mahali popote kutokana na ukweli kwamba siku hiyo watakuwa maeneo tofauti na walikojiandikisha.

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mchungaji Stephen Kimondo alisema hivi sasa kuna mpasuko kati ya Serikali na wananchi wake ndiyo maana kila kukicha migomo na maandamano inazidi kutikisa.
MWANANCHI
Uzushi na udaku kama huu kutoka kwa mmoja wa viongozi wa CHADEMA ndio unasababisha watanzania walio wengi tuvichukie vyama hivyo.
Mimi nitafia CCM.
 
Serikali gani hii kama sio ya kidhalimu?

Wafadhili nao ni wanafiki.

Wanakubali kuiachia CCM kufuja pesa za kodi zetu kututesa tusifanye mabadiliko ya Amani?

Wanaikaribisha vita?
 
Dr.Slaa uwa simuelewi leo anaongea haya maneno kesho anaongea mengine kukanusha meneno ya kwanza.

Baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu utamsikia tena Dr.Slaa akilalamika kuwa Usalama wa Taifa wameiba kura zake.

Huyu ndiyo Dr.Slaa.
 
Dr Slaa atueleze i lini atamrejeshea Mahimbo mke wake. Haya mengine ni ulaghai wa kisiasa
 
Dr.Slaa uwa simuelewi leo anaongea haya maneno kesho anaongea mengine kukanusha meneno ya kwanza.

Baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu utamsikia tena Dr.Slaa akilalamika kuwa Usalama wa Taifa wameiba kura zake.

Huyu ndiyo Dr.Slaa.
Dr Slaa amekuwa kama Lissu vile. Anajichanganya na anawachanganya na wenzake
 
Back
Top Bottom