Dk Slaa: Kwanini sikumsalimia JK

Nimependa sana penye red, Dr. Slaa hatimaye anatambua JK ni rais wa tz

Umetoa hewa ya uvundo kwa kufikili kwa masburi yako, kama ungekuwa unafikili kwa kutumia kichwa ungejua kuwa Dr. Slaa analazimishwa kumtambua Rais aliyechaguliwa na tume ya uchaguzi kwa mjibu wa katiba inayoturazimisha kufanya hivyo. Kama si kufikili kwa kutumia masaburi yako ungejua kabisa kwamba Dr. Slaa asipomtambua JK kuwa Rais ni Kesi ya Uhaini.
 
Naomba nitofautiane na wewe Mkuu, kwamba JK ndiye mwenye kuyumbisha vichwa vyetu humu, laiti kama angeliujua umarufu wa Dr. Slaa hapa nchini angewaagiza watu wa uslama wa taifa wamwamuru Dr. Slaa aende kumsalimia. Lakini kwa sababu JK aliamua kutomsalimia Dr. Slaa matokeo yake ameyatengenezea magazeti biashara, Jamani umarufu wa Dr. Slaa hapa nchini we achatu.
Hivi kuna mamlaka ya Rais kumwamuru mtu amsalimie!!?? au mnapost vitu bila kufikiri vizuri?
 
usalama wa taifa sijui wana kazi hapa Nchini, walipaswa kuwachunguza na kuwawajibisha mwandishi na mhariri wa hizi habari, maana huu ni uchochezi, fitina na uchonganishi.....
 
Hivi kuna mamlaka ya Rais kumwamuru mtu amsalimie!!?? au mnapost vitu bila kufikiri vizuri?

wO6mmdbRzeLQwAAAABJRU5ErkJggg==


Mkuu matola hii ikaeje? Hiali kama hii ingefanyaka tusingeumiza vichwa humu
 
Hii protokali ya hapa nayo ni kizungumkuti, iweje ZK, naibu katibu mkuu akae kwenye zulia halafu WS, Katibu Mkuu akae nje ya zulia, besides kushoto ya ZK kulikua na kiti ambacho kilionekana kuwa wazi ikimaanisha kabisa kwamba kilikua kimetengewa Mh WS.........!!!??? anachotuaminisha WS ni kwamba usalama walichakachua haki yake???

Wewe bwana/bibi usalama tafadhali weka picha tukione hicho kiti kilichoonekana kuwa wazi kushoto kwa ZK. "Stop the misinformation"
 
Kwani JK lazima asalimiwe na kila mtu? Nini cha ajabu Dr Slaa kutomsalimu, kama ni urais kwani hio nayo ni special talent au inataka mtu special kiasi kila mtu atatamani kumkimbilia angalau apate mkono wake tu? Mimi pia naweza ubunge na Urais pia and i think nitafanya vizuri tu na kupunguza machungu ya wabongo manake mi sijui kama kuna mtu alieko madarakani muda huu anawaza chochote kuhusu Watz! Hata kucontrol bei ya SUKARI tu eti nayo ni issue ya KITAIFA! mi nitajinyonga siku moja haki ya Mungu.
 
Kwenye Itifaki hasa kwenye matukio kama hayo, anayepaswa kusalimia ni Rais, maana yeye ndo anakuja wa mwisho kwa hiyo anawasalimia wale aliowakuta, na amba wako katika mstari wa mbele. Vinginenvyo, huwezi tu kukurupuka ukatoka sehemu unasema unaenda kumsalimia Rais, ukifanya hivyo, usalama wa Taifa wanakukamata mara moja.
 
source: Mwananchi gazeti

katibu mkuu wa chadema dk willibrod slaa amesema kuwa, hakuweza kusalimiana na rais jakaya kikwete kutokana na jiografia ya eneo la makaburini lilivyopangwa na watu wa usalama wa taifa pamoja na kamati ya mazishi kutomruhusu kufanya hivyo.

Hata hivyo dk slaa alisisitiza kuwa, kwa upande wake, kwenye msiba siyo sehemu ya kwenda kwa ajili ya kusalimiana na watu ama kurekebisha mambo yaliyoharibika bali ni sehemu ya kumwombea marehemu.

“siyo hulka ya dk slaa kutumia misiba kama sehemu ya kusalimiana, wala kutengeza mambo yaliyoharibika, mimi huwa naenda kwenye msiba kwa lengo moja tu la kumwombea marehemu, huwa simtazami hata mtu aliyekaa pembeni yangu,” alisema dk slaa alipozungumza kwa njia ya simu jana.

Alifafanua kuwa, katika eneo la makaburi kulikuwa na mabanda matano ambayo yalipangwa kwa ajili ya askofu, rais, viongozi wa vyama vya siasa, mwili wa marehemu na familia na banda jingine lilikuwa la watu wengine waliohudhuria mazishi hayo.

“sasa kutoka alipokuwa amekaa rais mpaka kwenye banda nilipokuwa mimi, kulikuwa na umbali wa karibu mita 20, sasa mlitaka nikimbie kumsalimia rais nivunje protokali kisha nikamatwe na usalama wa taifa,” alisema dk slaa.

Alisema alikuwa mtu wa kwanza kufika makaburini kwa lengo la kuangalia jinsi kaburi la mbunge wa chama chake lilivyochimbwa kisha akaonyeshwa sehemu ya kukaa na watu wa usalama wa taifa.

Alisema kuwa, hata katika wakati wa kuaga mwili wa marehemu regia mtema, katika ukumbi wa karejee, kulikuwa na utaratibu kama huo ambapo ilitengwa sehemu ya kukaa makamu wa rais, spika wa bunge, kiongozi wa kambi ya upinzani na makamu wake na yeye dk slaa akawekewa sehemu yake kama katibu wa chama alichokuwa akikitumika marehemu.

“mimi sipendi kuweka siasa kwenye mambo kama ya msiba, dk slaa siyo kichaa siyo kichaa aanze kukimbia kumsalimia rais. Katika sehemu kama ile rais huwa anakuja baada ya watu wote wakiwa wameshakaa, yeye ndiye hupita na kuanza kusalimia watu na hamjaona hata sehemu moja aliponyoosha mkono kunisalimia nikamkwepa,” alisema dk slaa:

“msiba siyo mahali pa kutengeza urafiki, au kutengeza mambo yaliyo haribika, pale ni ibada tu na kumuombea marehemu siyo sehemu ya kufanya siasa” alisisitiza dk slaa. Jana baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa, dk slaa alishindwa kusalimiana na rais jakaya kikwete katika mazishi ya regia mtema yaliyofanyika kijijini kwao ipangalala morogoro juzi.

Regia alifariki dunia januari 14 kwa ajali ya gari iliyotokea katika eneo la ruvu mkoani pwani.



my take
:
Mwananchi ni gazeti la udaku kwani jana kabla ya kuandika habari ya dr. Slaa kumuepa kikwete ilishindwa kumuuliza dr mwenyewe ili athibitishe madai hayo? Tuache kuandika habari za bila utafiti,
huu nao si uchochezi? usilazimishe kuandika habari za uchochezi ili tu gazeti lako liuzwe

nakubaliana nawe mdau! Naona mwananchi linataka kuanzanza kupotea?????????!!!! Maana habari zake zinaanza kuwa za kidaku badala ya kitafiti kama zamani. May be mafisadi washa lichakachua!!!!
 
yaani watanzania tunafurahisha sana..badala ya kudiscuss mambo muhimu tunaongelea mambo ya kupeana mikono.rubish
 
Huu ni uCHOCHEZI raisi wa nchi akipungia ina maana kasalimia Wote Hasa Wananchi sasa Iweje Rais awe tena anaenda kusalimia Mtu mmoja mmoja?
 
Umetoa hewa ya uvundo kwa kufikili kwa masburi yako, kama ungekuwa unafikili kwa kutumia kichwa ungejua kuwa Dr. Slaa analazimishwa kumtambua Rais aliyechaguliwa na tume ya uchaguzi kwa mjibu wa katiba inayoturazimisha kufanya hivyo. Kama si kufikili kwa kutumia masaburi yako ungejua kabisa kwamba Dr. Slaa asipomtambua JK kuwa Rais ni Kesi ya Uhaini.

Mapenzi yasizidi sana penye ukweli sema, Je JK ni tume ya uchaguzi?? Mwanaume hatakiwi kuakasirika kila wakati
 
Kile kikao cha siri kati Mh Mbowe na Rais wetu kitalimaliza hili. Subirini tu. Wasiunde tu SUK kama Zanzibar
 
waandishi wa Mwananchi kwa kweli sasa wameanza kuharibu! hizi habari za ''kiudaku'' zitawapotezea wasomaji. nakumbuka habari yao ya ''Vita ya urais Chadema'' ilivyokuwa ya kizushi. kisha baada ya Chadema kiukanusha wakaiandika habari hiyo bila kuelezea kuwa wao ndio walioandika udaku huo. jamani sio lazima habari za kisiasa tu ndio ziandikwe, mwishoni ndio mnatunga habari sasa. au mmegundua Wa Tz tunapenda sana habari za siasa? ni wakati wenu huu kubadilika!
 
Dkt. umejibu kistaarabu kabisa, protokali unaifahamu vyema, ni matumaini yangu hauko mbali kukutana na kiongozi wa nchi na mambo yatakuwa mazuri. Big up! ingawa kuna taarifa arusha nzima ya kuwa una matatizo na mwenyekiti mbowe kwa vile hukupenda wazo la kwenda ikulu! pia kuna maneno mengi tu ya kuwa mbowe amefikia kusema ya kuwa una hiari ya kuendelea kuwa kiongozi na mwanachama wa chadema au uondoke, hili linakatisha tamaa.
 
wewe na hawa kenge ni nani? hata moyo wako unakusuta! unamtukana mtu ambae hata hajui kama uliingia duniani na ujinga wako huo siku ulipozaliwa. hala waratibu wa jf mnaangalia tu! lakini kama ingekuwa ni wana chadema wametukanwa tayari mhusika angeshafungiwa, be fair please! acheni umachame hapa.
 
jamani siyo siri ya kuwa magazeti ya nation na taifa leo ndiyo yaliyosakule kenya baada ya uchaguzi 2007. nation ndiyo wenye mwananchi na citizen na ndiyo huko wanataka kutupeleka, mbeya tumewashtukia na tayari tumeanza kuwasusia na leo hii niko safarini arusha pia nimeanza kuona dalili kama hizo. tuwaepuke kama maradhi, wasije tuingiza vitani.
 
jamani siyo siri ya kuwa magazeti ya nation na taifa leo ndiyo yaliyosababisha vita kule kenya baada ya uchaguzi 2007. nation ndiyo wamiliki wa mwananchi na citizen na ndiyo huko wanataka kutupeleka, mbeya tumewashtukia na tayari tumeanza kuwasusia na leo hii niko safarini arusha pia nimeanza kuona dalili kama hizo. tuwaepuke kama maradhi, wasije tuingiza vitani.
 
Back
Top Bottom