Dk Slaa: Kwanini sikumsalimia JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa: Kwanini sikumsalimia JK

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by cjilo, Jan 20, 2012.

 1. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  SOURCE: MWANANCHI GAZETI

  KATIBU Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa amesema kuwa, hakuweza kusalimiana na Rais Jakaya Kikwete kutokana na Jiografia ya eneo la makaburini lilivyopangwa na watu wa usalama wa taifa pamoja na kamati ya mazishi kutomruhusu kufanya hivyo.

  Hata hivyo Dk Slaa alisisitiza kuwa, kwa upande wake, kwenye msiba siyo sehemu ya kwenda kwa ajili ya kusalimiana na watu ama kurekebisha mambo yaliyoharibika bali ni sehemu ya kumwombea marehemu.

  "Siyo hulka ya Dk Slaa kutumia misiba kama sehemu ya kusalimiana, wala kutengeza mambo yaliyoharibika, mimi huwa naenda kwenye msiba kwa lengo moja tu la kumwombea marehemu, huwa simtazami hata mtu aliyekaa pembeni yangu," alisema Dk Slaa alipozungumza kwa njia ya simu jana.

  Alifafanua kuwa, katika eneo la makaburi kulikuwa na mabanda matano ambayo yalipangwa kwa ajili ya Askofu, Rais, Viongozi wa vyama vya siasa, mwili wa marehemu na familia na banda jingine lilikuwa la watu wengine waliohudhuria mazishi hayo.

  "Sasa kutoka alipokuwa amekaa Rais mpaka kwenye banda nilipokuwa mimi, kulikuwa na umbali wa karibu mita 20, sasa mlitaka nikimbie kumsalimia Rais nivunje protokali kisha nikamatwe na usalama wa taifa," alisema Dk Slaa.

  Alisema alikuwa mtu wa kwanza kufika makaburini kwa lengo la kuangalia jinsi kaburi la mbunge wa chama chake lilivyochimbwa kisha akaonyeshwa sehemu ya kukaa na watu wa usalama wa taifa.

  Alisema kuwa, hata katika wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Regia Mtema, katika ukumbi wa Karejee, kulikuwa na utaratibu kama huo ambapo ilitengwa sehemu ya kukaa Makamu wa Rais, Spika wa Bunge, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani na Makamu wake na yeye Dk Slaa akawekewa sehemu yake kama Katibu wa Chama alichokuwa akikitumika marehemu.

  "Mimi sipendi kuweka siasa kwenye mambo kama ya msiba, Dk Slaa siyo kichaa siyo kichaa aanze kukimbia kumsalimia Rais. Katika sehemu kama ile Rais huwa anakuja baada ya watu wote wakiwa wameshakaa, yeye ndiye hupita na kuanza kusalimia watu na hamjaona hata sehemu moja aliponyoosha mkono kunisalimia nikamkwepa," alisema Dk Slaa:

  "Msiba siyo mahali pa kutengeza urafiki, au kutengeza mambo yaliyo haribika, pale ni ibada tu na kumuombea marehemu siyo sehemu ya kufanya siasa" alisisitiza Dk Slaa. Jana baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa, Dk Slaa alishindwa kusalimiana na Rais Jakaya Kikwete katika mazishi ya Regia Mtema yaliyofanyika kijijini kwao Ipangalala Morogoro juzi.

  Regia alifariki dunia Januari 14 kwa ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Ruvu mkoani Pwani.  MY TAKE
  :
  Mwananchi ni gazeti la udaku kwani jana kabla ya kuandika habari ya Dr. Slaa kumuepa kikwete ilishindwa kumuuliza Dr mwenyewe ili athibitishe madai hayo? Tuache kuandika habari za bila utafiti,
  huu nao si uchochezi? usilazimishe kuandika habari za uchochezi ili tu gazeti lako liuzwe
   
 2. Vmark.

  Vmark. JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  This is real weird.....c ndio hawa mwananchi waliosema dr.alimkwepa jk?? Tutasikia na kushuhudia mengi sana b4 2015 but all in all wheat and chaff will be separated!!
   
 3. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Me sioni umuhimu wa suala ili kukuzwa kiasi hikn na hv vyombo vya habari,Dr kaeleza vizuri sana na protocal zinaeleweka!hawa waandishi wa mwananchi wamekuaje?nimeanza ku loose faith na ili gazeti,sasa linaelekea kwenye udaku!nafikiri gazeti la nipashe wanarudi vizuri katika hadhi yao kwa sasa!maana habari zao ni za maana hawana udaku kama mwananchi!me sijawahi ona eti rais awe sehemu mtu akurupuke na kuwapita watu wa usalama kwenda kumsalimia rais,ila kitaratibu,rais ndie uwa anakwenda kusalimia watu
   
 4. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  kulikuwa na maana gani waandike habari kwanza halafu kesho yake ndio waje wamuulize..huu ni upuuzi mtupu. kwa nini wasingemuuliza ndo waandike?. waache unafki na uchochezi bahati ni kwamba Dr ni mstaarabu
   
 5. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,491
  Likes Received: 4,764
  Trophy Points: 280
  Hii protokali ya hapa nayo ni kizungumkuti, iweje ZK, naibu katibu mkuu akae kwenye zulia halafu WS, Katibu Mkuu akae nje ya zulia, besides kushoto ya ZK kulikua na kiti ambacho kilionekana kuwa wazi ikimaanisha kabisa kwamba kilikua kimetengewa Mh WS.........!!!??? anachotuaminisha WS ni kwamba usalama walichakachua haki yake???
   
 6. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Dr la msingi kajieleza vzr na hili gazeti limekua la hovyo kabisa kwa sasa na wengi tunaju Nevil Meena mhariri Mwananchi yupo kundi gani kwa walioanza hayo huko chichiem
   
 7. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  nilishangaa gazeti kubwa kama Mwananchi kuandika habari waliyoipa uzito kwa hisia bila kuwahoji wahusika! Shame on them!
   
 8. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  why is this so important?
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mikono ya JK imejaa dhulma ya wanyonge. Nani anaitakaa?
   
 10. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika orodha ya magazeti, nimejipiga marufuku Mwanachi kulisoma hata kuligusa na mtu akinifungia kitu chochote kwa kipande cha gazeti la Mwanachi..! nazaa nae walahi!
   
 11. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Mwananchi wameanza kampeni maalumu kuelekea 2015 wahariri wameanza kuwa wendawazimu wa habari, misumali ya akili zao imeshavimbishwa na majihela, macho yao yamevalishwa miwani ya noti, wanawehuka na kuandika bila utafiti. Balancing news by hearing from the horses mouth haipo. Tutaona sarakasi nyingi sana na wahariri kuanza kutembea bila nguo.
   
 12. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nadhani kwa kua ZK ni mbunge na naibu kiongozi wa kambi ya upinza bungeni,na mh Mbowe pia walistahili kuwepo jukwaa moja na Mh JK,lakin WS ikumbukwe yeye ni katibu wa chama tu!ni mtizamo wangu lakini
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mbona Dr. Slaaa anasisitiza kwamba msibani si mahali pa kutengeneza mambo yaliyoharibika? Hivi kusalimiana na mtu ni kutengeneza mambo yaliyoharibika? Nadhani Dr. Slaaa ana siri nzito moyoni.

  Hivi ni kweli kabisa kwamba Dr. Slaaa akiwa msibani hamwangalii aliye pembeni yake?
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Dr. anasema alionyeshwa na watu wa usalama ili akae alipokaa. Sasa kama kulikuwa na kiti hicho ambacho kimantiki kilikuwa cha Dr. Slaa na hao watu wa usalama wakamwambia akae kwingine, basi Dr. Slaa anataka kutuambia kuwa watu wa usalama ndio waliomweka mbali na Rais au?
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hivi ni lazima kusalimiana?? mbona sioni sehemu ikisema JK hakumsalimia Slaa??

  Upuuzi wa Mtanzania wa leo, inflation juu, sie tuko bize kuangalia nani kamsalimia nani
   
 16. Ndi.Wa.Nkaka

  Ndi.Wa.Nkaka Member

  #16
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa uhakika hasa naamini itachukua miaka 100 kabla ya Watanzania walio wengi kuwa na upeo na uchambuzi wa mambo muhimu ya kimaendeleo!

  Hivi Dr Dr Dr Jakaya na Dr Slaa ni LAZIMA wapeane mikono kila wanapokuwa wamejumuika sehemu moja? Ninanyofahamu mimi NWK, panapokuwa na mkusanyiko wa watu na MKUU wa NCHI yupo ni MARUFUKU mtu yeyote yule kukatiza na kwenda moja moja kupeana kiganja na MKUU wa NCHI... BALI... Mkuu Wa Nchi kama wakati unaruhusu, YEYE ndiye anweza kukatiza miongoni mwa jumuiko na kupeana viganja na watu ambao YEYE binafsi anaona umuhimu wa kufanya hivyo...

  Mengine ni blah blah's - Anyways - Debe TUPU haliachi KUTIKA
   
 17. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Kwanini unaishi kama mganga wa kiennyeji??
  Acha kuhisi hisi mambo na kuyafanya ndiyo majawabu !!! Kuhusu kile kiti ulichikiona wewe "mwandishi wa mwananchi" si uende Usalama wa taifa uwaulize kilikuwa cha nani na kwa nini hakikuliwa? unaogopa? sasa huo sio uandshi!
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,619
  Trophy Points: 280
  Mode, hamishia habari hii kule Chit chat na baadae Hoja Mchanganyiko. Habari hii haistahili Jukwaa la Siasa!. Hizi double standards zitatufikisha pabaya!.
   
 19. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Zitto ni mbunge na aliyefariki ni mbunge hivyo alipangwa kukaa banda la bunge na spika,naibu na mbowe ambao wote ni wabunge pia.....Dr sio mbunge...fuatilia maelezo ya Dr vizuri....hicho kiti kitupu pembeni ya Zitto kiko wapi?

  [​IMG]
   
 20. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,139
  Likes Received: 7,391
  Trophy Points: 280
  Mbona hata mimi sikumsalimia JK na sio Issue???!!
   
Loading...