Dk. Slaa: JK ameliingiza taifa vitani

Dk. Slaa: JK ameliingiza taifa vitani

Status
Not open for further replies.
Hakuna ubishi hii ni tamko la hatar kutolewa na mkuu wa nchi! huku ni kujikinai kulikopita kipimo... Hivi NEC ya ccm kwanini haikujadili DR Ulimboka na Kibanda katika matukio yanayohusisha na vyombo vya ulinzi? hivi anathani kwakuwa raia hawana risas watakuwa wanyonge kukubali kupigwa na green guid? HAPA NAIONA KIMBALI TZ INAKUJA KWA SPEED YA AJABU

CHADEMA mnahusika sana matukio hayo, sasa ndiyo watu wanajua ni jinsi gani mlivyokuwa mkitetekeleza mauaji ili kuisingizia serikali na vyombo vyake, sasa mtakoma.
 
Siasa za fujo za hawa CHADEMA hazitapewa nafasi katika kisiwa chetu cha amani.
 
JK ,atajutia kauli yake hii, ngoja mtaona , haoni uhuru anasota huko The Hegue bila hata kutoa kauli tata kama hii ya kwake ? Ingekuwaje angel iwaki kutoa kauli yenye kuakisi kama hii?
 
bange zinapulizwa na lema pale kijenge mwanama, mara moja moja dr.slaa anamgongea lema pafu ndio mana slaa akili zimemruka

Huwezi ukahamasisha raia wako wadhuriane halafu ukajiona kuwa uko salama kichwani mwako.
 
Siasa za fujo za hawa CHADEMA hazitapewa nafasi katika kisiwa chetu cha amani.
Jk asifikiri kwa kauli hii yeye na CCM watakuwa salama, maana kuna vijana wengi sana ni machinga wanadhulimiwa ni suala la kuwaambia jibuni mapigo nchi I tazama hii,ajisahihishe huyu ...
 
Slaa ni mnafiki na ni mfitinishaji, mbona lema na mbowe walimfanyia vurugu aliyekuwa mwenyekiti cdm arusha mwaka jana lakini alinyamazia. Nyani kawaida hucheka ----- la mwenzie wakati yeye analo. Slaa akome kutuchonganisha wa tz kwa kupotosha kauli ya jk.
 
Mungu ameaamuwa kuwaumbua CCM kwa kuwaweka hadharani baada ya kuendesha mauaji kwa kificho na kudhuru watu kwa kificho.Mungu amechoka na vitendo vichafu vya maccm amemuwa kuwaumbua ili kila mtu ajue uchafu wanao ufanya gizani.
 
“Waswahili wanasema ukishangaa ya Musa utaona ya Firauni. Hivi karibuni tulishangaa kauli ya Pinda kutaka polisi wawapige tu wapinzani, leo rais naye anawataka CCM waache unyonge, wajibu mapigo. Hii ni hatari sana,” alisema Dk. Slaa.

Nikuulize mheshimiwa Slaa, je inawezekana kujibu mapigo ambayo hayapo? Basi mkitaka asiwepo wa kujibu mapigo, basi msianzishe hayo mapigo. Na akina CCM pia inawahusu, kama mkihimizana kujibu mapigo, mkumbuke pia wengine watakaa kwa tahadhari kujibu mapigo pia iwapo mtayaanzisha. Kwa hiyo mheshimiwa Slaa unaonywa usianzishe mapigo maana yatajibiwa, lakini pia nawe jiandae kujibu mapigo kama yataanzishwa maana sasa ruksa imetolewa ya kujibu mapigo. What is good for the goose is good for the gander.

Maana yake: asiwepo wa kuanzisha mapigo maana yatajibiwa pande zote. Tuache unyonge, wote kabisa.
 
Akili ya magamba ni ndogo sana, mnaacha kujadili jambo la msingi lililoigusa taifa mnaishia kupiga propaganda kuhusu Dr Slaa, hivi nyie vijana mmeweka akili wapi, mnafikiri utekelezaji wa kauli ya machafuko uliotolewa na Rais kikwete, nyie mtapona, jihadharini sana ndugu zangu, tunashabikia vitu vingine ambavyo havina msingi wowote, wametoa maoni watu wengi hapo, lakini inaonekana Dr Slaa anawauma sana, mtaipata fresh, hatutishwi na kauli za mwenyekiti wenu wa magamba, eti kisa yeye ni rais, sasa jaribuni kuleta ujinga muone, kupitia kura mmeshindwa, sasa mmeanza michezo isiyostahili, heri nife nikipigania haki, kuliko kuishi kwa manyanyaso na viisho kiasi hiki, hatutarudi nyuma kamwe, Mungu yu pamoja nasi, tuliishasema, ccm ndio wanaovuruga amani ya nchii hii.
 
Slaa ni mnafiki na ni mfitinishaji, mbona lema na mbowe walimfanyia vurugu aliyekuwa mwenyekiti cdm arusha mwaka jana lakini alinyamazia. Nyani kawaida hucheka ----- la mwenzie wakati yeye analo. Slaa akome kutuchonganisha wa tz kwa kupotosha kauli ya jk.

Kama munaona mwenye kiti wenu yuko sahihi kwa kauli ya kuhamasisha raia wake wauane mshaurini akapambane na Kagame.Mbona Kagame kila siku ana mtusi lakini hamchukulii hatua zozote au amegundua kuwa Kagame ni maji marefu ana taka kuwaonea raia ambao wamekosa mtetezi ambae ana weza akawatetea?au mwenyekiti wenu ana ogopa ng'ombe na kuonea mbuzi?.
 
Huyu mkwer.e ni janga kwa kauli zake za ngomani kwenye taifa...Mungu tunusuru.
 
Mtaji mkubwa wa siasa za chadema ni vurugu na maandamano, sasa na nyie mkijibiwa kwa mbinu zenu mnaanza kulia lia, tunataka siasa za hoja na si vurugu, imefikia mahali chadema mkatambua kwamba hii nchi ni ya wote, na si chadema pekee wenye haki ya kuishi humu tanzania, na hakuna mahali popote ambapo haki inapatikana kwa vurugu, mara zote mazungumzo ndio njia sahihi, sasa mjifunze kuacha vurugu mkae tujadiliane kama taifa...
 
Siungi mkono alichosema Kikwete,ninalaani!ila nawaomba vyama upinzani waache vurugu tuone hao CCM,watamchokonoa nani

MKUU, iko hivi, kama ilivyo ngumu kukubali kunyang'anywa kitu ulichokizowea, ndivyo ilivyo kwa maccm. Hawana Haya wala Aibu, yatakufuata tu hata nyumbani kukuchokoza. Camp zao za Green guard wamejaza magaidi, ambao baadae ndio watakaokuja kuwa waasi.Walishawaambia wananchi wasiichague CHADEMA kwani wakifanya hivyo nchi itaingia vitani, cha kujiuliza nchi ingeingia vitani na nani?Nani angeanzisha vita?Kwa nini aanzishe vita?Je CHADEMA wangeweza kujianzishia vita na kujipiga wenyewe?CCM tumewachoka, angalieni KANU waliko, ndo kaburi lenu hilo, nao waliyafanya hayohayo wakati wakitawala, leo hii wako wapi?
 
KAULI aliyopata kuitoa Waziri Mkuu Mizengo Pinda bungeni kuwataka polisi wawapige wapinzani, na kauli ya juzi ya Rais Jakaya Kikwete kuwaagiza wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wajibu mapigo pale wanaposhambuliwa na wapinzani, imeelezwa kuliingia taifa vitani.

Akifungua kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM taifa mjini Dodoma, Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho taifa, alisema bila kumung’unya maneno akiwataka Wana-CCM kuacha unyonge na kujibu mashambulizi pale wapinzani wanapoendesha siasa za vurugu.

Waziri Mkuu Pinda katika kipindi cha Maswali na Majibu bungeni aliwahi kutoa kauli ya kuwataka polisi wawapige wafuasi wa CHADEMA kwa vile walikuwa wakiendesha maandamano katika sehemu mbalimbali nchini, ambayo Serikali ya CCM ilitafsiri kama vurugu.

Pinda ambaye hivi sasa amefunguliwa kesi mahakamani ya kuvunja katiba kutokana na kauli hiyo, alisema serikali imechoka na haina njia nyingine zaidi ya kuwataka polisi wawapige wapinzani.

Wakitoa maoni yao kuhusu msimamo wa Rais Kikwete, baadhi ya wanazuoni, viongozi wa siasa wameeleza kushangazwa na kauli ya kiongozi huyo mkuu wa nchi kwani ameliingiza taifa vitani.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kauli ya Rais Kikwete inatisha, inashangaza na haikupaswa kutolewa na kiongozi mkuu wa nchi.

Alisema kauli yoyote inayotolewa na rais pasipo kujali yupo sehemu gani ni amri kwa walio chini yake, na kwamba kinachofuata ni utekelezaji.

“Waswahili wanasema ukishangaa ya Musa utaona ya Firauni. Hivi karibuni tulishangaa kauli ya Pinda kutaka polisi wawapige tu wapinzani, leo rais naye anawataka CCM waache unyonge, wajibu mapigo. Hii ni hatari sana,” alisema Dk. Slaa.

“Kwa maoni yetu, CHADEMA tunasema Rais Kikwete ameliingiza taifa vitani, amefungua milango ya uvunjifu wa amani, kinachofuata ni umwagaji damu.”

Dk. Slaa aliongeza kwa kusema kuwa anatilia shaka uwezo wa Rais Kikwete katika kuchambua taarifa
anazofikishiwa mezani na wasaidizi wake, ambazo safari hii zimemfanya aamini wanaoanzisha vurugu katika uchaguzi ni wapinzani.

Alisema licha ya Tume ya Jaji Amir Manento na ile ya Haki za Binadamu kulitaja Jeshi la Polisi na CCM kuwa chanzo cha vurugu zinazosababisha mauaji ya watu nchini, Rais Kikwete ameziba masikio na kuwarushia tuhuma hizo wapinzani.

“Watu wameuawa Nyololo na Arusha, ripoti ya Haki za Binadamu anayo ofisini kwake ameifungia na kisha ametoa zawadi ya kuwapandisha vyeo wale waliosababisha mauaji hayo, leo anathubutu vipi kusema wapinzani ndio chanzo cha vurugu?” alisema na kuhoji Dk. Slaa.

Alisisitiza kuwa licha ya Rais Kikwete kuwasingizia wapinzani kuwa chanzo cha fujo, bado ameshindwa kuunda tume huru ya kimahakama ili kuujua ukweli wa matukio hayo.

Alisema kimsingi CHADEMA haitakubali damu ya Mtanzania hata mmoja imwagike kwa sababu ya kupata madaraka, na kwamba agizo la Rais Kikwete linavilazimisha vyama vya upinzani kuwaandaa vijana wao ili kujilinda.

“Hivi kama na sisi tutaamua kuwaambia vijana wetu wajilinde, na katika hali hii ya kunyanyaswa na kuonewa na hao CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola, unadhani nchi itabaki salama?” alihoji Dk Slaa.

Mwenyekiti wa Chama Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amemsikitikia Rais Kikwete kwa kupoteza uelekeo wa kulinda amani ya nchi.

Alisema ameshtushwa na kauli hiyo aliyoieleza kuwa imekosa uvumilivu wa kisiasa, huku akiainisha kuwa chanzo cha vurugu katika sehemu mbalimbali nchini ni CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola.

Alisema alitegemea Rais Kikwete ahimize Watanzania kutii sheria bila shuruti badala ya kuonyesha dalili za wazi kuwa hakuna haja ya kutii sheria, na hata vyombo vinavyotafsiri sheria hiyo.

“CCM ndio waanzilishi wa vurugu zote nchini, na kama mwenyekiti wao ametoa kauli hiyo, unategemea nini kitatokea ikiwa yeye ndiye amiri jeshi mkuu?” alihoji Lipumba.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, kwa upande wake alisema kauli ya Rais Kikwete itamfanya abebe dhamana juu ya jambo lolote la uvunjifu wa amani litakalotokea kuanzia sasa.

Alisema ni hivi karibuni taifa liliingia katika maridhiano ya kuandika katiba mpya kwa ajili ya Watanzania, hivyo Rais Kikwete hakupaswa kutoa kauli hiyo wakati huu.

“Hii kauli haina viashiria vizuri kwa taifa, ni vema aje hadharani atuambie alikusudia nini, vinginevyo atabeba dhamana ya jambo lolote litakalojitokeza,” alisema.

Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambaye ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa na jamii, Bashiru Ally, alisema Watanzania wategemee visa vingi wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa 2015.

Alisema nchi inaweza kuingia kwenye machafuko ambayo hayajawahi kutokea kutokana na kauli za wanasiasa, zinazolenga kuwanufaisha wao binafsi badala ya maslahi ya taifa.

Aliongeza kuwa kitendo cha Mwenyekiti wa CCM kuwaagiza wafuasi wake wasiwe wanyonge na wajibu mapigo, siyo suluhisho la tatizo bali ni kuongeza tatizo.

Alisema NEC ya CCM badala ya kukaa na kuamua kupambana, wangetafuta jibu juu ya kiini cha mapambano hayo yanayodaiwa kutokea katika jamii.

“Mwenyekiti amekuja na majibu mepesi katika maswali magumu, na mimi nasema kuchoka uvumilivu si jawabu la tatizo, wajitokeze hadharani kutibu chanzo,” alisema Bashiru.

Alisema rais kuruhusu hali hiyo ni kutangaza vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa kuwa kauli yake ni amri kwa walio chini yake, na kwamba wananchi watakapokataa kunyanyaswa, madhara yake yatakuwa makubwa kwa jamii nzima.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, alipoulizwa kama kauli ya rais inaashiria Jeshi la Polisi limeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kuwalinda Watanzania na pia kama si uchochezi wa wazi, alisema hajapata taarifa hizo wala kusikia, na kwamba atafanyia kazi ajue kama alichoelezwa kimetamkwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa.

“Mimi ndiyo kwanza ninasikia kutoka kwako, wewe ndiyo unaniambia, ngoja nifuatilie nijue kama kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM,” alisema IGP Mangu.

Akifungua mkutano wa NEC ya CCM juzi mjini Dodoma, Rais Kikwete aliwataka wanachama wa chama hicho kuacha unyonge kwani uvumilivu waliokuwa nao umefika kikomo chake.

Alisema chama hicho kinaingia kwenye uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kalenga mkoani Iringa, kinashindana na vyama vingine ambavyo alisema ni wagomvi, maana kwao ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wa kufanya kazi ya siasa.

“Tulizungumza nalo hilo kwenye Kamati Kuu, tulikubaliana kuacha unyonge. Ndiyo, kwenye Kamati Kuu tumekubaliana, tumesema jamani watu wote waende wakaseme tumekubaliana kuacha unyonge,” alisema huku akicheka na kupigiwa makofi na wajumbe wa NEC.

Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, alitolea mfano wa tukio lilitokea Kahama mkoani Shinyanga, ambapo kijana mmoja alitolewa macho kwa bisibisi, na tukio la Igunga ambapo kijana mmoja alimwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.

“Acheni unyonge na hata katika taarifa ya habari leo (jana) mtoe hivyo hivyo. Na muache habari zote mseme hii tu (waandishi wa habari). Uvumilivu una ukomo wake,” alisema huku wajumbe wakiendelea kumpigia makofi.

“Nalisema kwa sababu yanayotokea yanasikitisha sana. Pale Igunga kijana yule wamemmwagia tindikali, pale Kahama kijana ametolewa macho kwa bisibisi,” alisema.

Uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga lililopo mkoani Iringa unatarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu, huku tayari vyama vya CCM na CHADEMA vikiwa vimetaja wagombea wao.
kweli bwana
 
Mtaji mkubwa wa siasa za chadema ni vurugu na maandamano, sasa na nyie mkijibiwa kwa mbinu zenu mnaanza kulia lia, tunataka siasa za hoja na si vurugu, imefikia mahali chadema mkatambua kwamba hii nchi ni ya wote, na si chadema pekee wenye haki ya kuishi humu tanzania, na hakuna mahali popote ambapo haki inapatikana kwa vurugu, mara zote mazungumzo ndio njia sahihi, sasa mjifunze kuacha vurugu mkae tujadiliane kama taifa...

Mwenyekiti wenu ana ona ni bora aishi kwa amani na Kagame kuliko kuishi kwa amani na raia wake.
 
Watanzania tukatae uchochezi kutoka upande wowote hawa wote wanao sema haya wana faida na vurugu ndio mana wana shabikia na kuyakuza ili itoke vurugu au vita ambayo kwao ina weza kua na faida.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom