Dk Slaa: Hakuna anayemchukia Ben Mkapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa: Hakuna anayemchukia Ben Mkapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Jan 27, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa amesema hakuna Mtanzania anayemchukia Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, ila malalamiko yao dhidi yake ni kutaka kujua ukweli kuhusu mambo yanayomhusu.


  Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana, wakati akitoa maoni kuhusu kauli ya Mkapa aliyotoa mkoani Iringa Jumapili iliyopita, akiwaonya wanasiasa kuacha fitina, chuki, majungu, udini na ukabila kwa hofu kwamba nchi inaweza kuingia katika machafuko.


  Mkapa alinukuliwa na vyombo vya habari jana akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Walolesi la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa alipokaribishwa na Askofu Dayosisi hiyo, Dk Owdenburg Mdegella kuwasalimia waumini.


  Dk Slaa pia alimtaka Askofu Mdegella kuwaomba radhi Watanzania kwa kitendo chake cha kumtetea na kumsifu Mkapa. Alisema kwa kitendo kama hicho makanisa yanaweza kufika pabaya, kwa kurukia mambo na kusifu watu wakimezea mate michango ya fedha.


  "Hatumchukii Mkapa, hakuna mtu anayemchukia, yeye ni rais mstaafu, tunachotaka ni kuwa aache blaablaa za kupotosha hoja. Anachofanya ni kujaribu kupoteza muda na kuwapamba wananchi wasahau hoja ya msingi iliyopo sasa," alisema Dk Slaa.


  Dk Slaa ambaye pia ni mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema alisisitiza kuwa, hakuna chuki dhidi ya rais huyo mstaafu zaidi ya kutaka kujua iwapo alifanya biashara alipokuwa Ikulu kama rais wa Tanzania.


  "Sisi hatumchukii ila tunataka kujua ukweli, kama alipokuwa Ikulu, akiwa Rais wa taifa hili alifanya biashara na kuuza mali ya Watanzania. Tunataka atueleze kama kampuni iliyonunua Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira ni yake, mkewe, watoto wake na rafiki yake Yona au la?" alihoji Dk Slaa.


  Aliongeza kuwa, wananchi wa Tanzania wanataka kusikia kauli ya rais huyo mstaafu, kwa kuwa mgodi wa Kiwira ulikuwa ni mali yao kabla ya kuuzwa.


  "Hayo ndiyo tunayotaka kusikia kwa faida ya wananchi, kwani ni haki kujua," alisema Dk Slaa.


  Alifafanua kuwa Mkapa anapaswa kuwaambia wananchi kama tuhuma zinazomkabili ni kweli au uongo na kwamba, akithibitisha ni uongo ni vema, lakini ikiwa ni kweli basi sheria ichukue mkondo wake badala ya kuendeleza maneno aliyoyaita blaablaa ambazo hazitamsaidia.


  Alisema kuwa siasa za chuki, majungu, fitina, ukabila na udini anaozungumzia Mkapa utaisha pale atakapowaweka wazi Watanzania kuhusu tuhuma zinazomkabi.
  "Hizo siasa za chuki, majungu, fitina, ukabila na udini zitaisha akiwaweka wazi Watanzania juu ya umiliki wa Mgodi wa Kiwira. Zaidi ya hayo nashangaa kwa nini azungumzie hayo wakati huu anapokabiliwa na tuhuma za kufanya biashara Ikulu," alisema Dk Slaa.


  Akizungumzia hatua ya Askofu Mdegella kumtetea Mkapa na kueleza kuwa anazushiwa uongo na vyombo vya habari, Dk Slaa alisema askofu huyo amewakosea Watanzania na anapaswa kuwaomba radhi.


  "Yule Askofu wa Iringa aliyemtetea Mkapa kuwa anazushiwa, lazima awaombe radhi Watanzania, kwa sababu amewakosea," alisema Dk Slaa.


  Alifafanua kuwa anayepaswa kujisafisha mwenyewe mbele ya watu aliowaongoza ni Mkapa na si askofu huyo.


  Alisema hatua ya askofu huyo na viongozi wengine wa dini hasa makanisa si sahihi, kwani inaendeleza utaratibu wa zamani wa kutomwonya au kumwambia ukweli mkubwa anapokosea.


  "Baba kutoambiwa akikosea hiyo ni tabia ya zamani na mbaya, haifai katika ulimwengu wa leo. Tabia ya baba kutosahihishwa ndiyo imetufikisha hapa tulipo," alisema Dk Slaa.


  Alisema anawaheshimu viongozi wa dini, lakini akaonya kuwa wasiingie mahali pabaya kwa kusifu watu kwa sababu ya kuhitaji michango makanisani.


  "Viongozi wa dini tunawaheshimu, wasiingie mahali pabaya na kusifu watu kwa sababu ya kutaka michango ya harambee. Kama hawajui kitu bora, wanyamaze, vinginevyo watalifikisha kanisa pabaya. Sisi tunawategemea wao wawe safi, lakini hii inatia hofu juu yao," alisema Dk Slaa

  Source:Mwananchi
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Na ikiwa ni ndio itakuaje... na ikiwa ni la itakuaje?
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,763
  Trophy Points: 280
  Mkapa aache kujificha na kutumia nyumba za Ibada ili kutaka kuficha madhambi yake. Hakuna ukweli wowote wa kuthibitisha kauli yake kwamba nchi imejaa majungu, chuki na fitina.

  Watanzania tunataka kujua kwa kina maovu mbali mbali yaliyofanyika wakati akiwa madarakani na yeye mwenyewe kuhusika na maovu hayo. Watanzania tuna haki ya kujua kwa kina na sauti za kutaka MKapa upandishwe kizimbani ili kujipatia utajiri kwa njia za haramu hazionyeshi majungu, fitina wala chuki dhidi yako, bali Watanzania tunataka kuona haki inatendeka. Kama ulihusika kuwafisadi na kuwaibia Watanzania basi sheria iachwe ifuate mkondo wake. Uchunguzwe nan kama ukionekana una hatia basi upandishwe kizimbani.

  Ukiwa madarakani yametokea maovu chungu nzima ikiwemo bilioni 133 za EPA, bilioni 155 za Meremeta, Kashfa ya ununuzi wa Rada ambayo wewe ulihusika katika kumtafuta wakala Vethlani, ununuzi wa ndege ulioufanya ukiwa umebakisha miezi mitatu madarakani, kuwaleta Net Group ili waendeshe TANESCO pamoja na kuwa Watanzania wengi tulipinga uamuzi wako huo, kusaini mikataba ya uchimbaji wa rasilimali zetu ambayo haina maslahi kwa Watanzania na kuifanya siri hata kukataa wabunge ambao ni wawakilishi wa Watanzania kuiona mikataba hiyo, kuuza nyumba za serikali kwa bei ya bure uamuzi ambao umeiingizia serikali hasara ya mabilioni, kujiuzia Kiwira katika mazingira ya kutatanisha tena kwa bei ya kujipangia mwenyewe. Na kufanya biashara ukiwa Ikulu.

  Tuhuma dhidi yako ni nzito sana hasa ukitilia maanani wewe ulijiita ni "Mr Clean" na awamu yako ya "uwazi na ukweli" acha unafiki na kutaka kubadilisha subject badala ya kutwambia kwa kina yale yaliyojiri katika tuhuma mbali mbali dhidi yako. Je, ulipindisha taratibu za serikali ili maovu yaliyosababisha wizi wa mabilioni ya pesa, kusaini mikataba mibovu, ununuzi wa ndede ya Rais, Rada na magari ya jeshi, uuzaji wa kiholela wa nyumba za serikali na kujiuzia Kiwira?

  Wengi hatuaamini kwa Tanzania sasa imejaa chuki, fitina na majungu bali tunachoona ni Watanzania kufungua macho na kugundua kwamba kuna viongozi kama wewe wanaoingia madarakani ili kukidhi uroho wao wa utajiri wa haraka haraka kwa kuwafisadi Watanzania na sasa tunataka majibu na kuona viongozi hao wanapandishwa kizimbani na kama wana hatia basi pia wafilisiwe na wafungwe.

  Wakati umefika sasa wa kukaa chini na waandishi wa habari hata kwa masaa matano ili ujibu tuhuma mbali mbali dhidi yako badala ya kutumia nyumba za ibada kutaka kubadilisha subject.
   
 4. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145

  Mimi nadhani akamatwe mara moja awaleze watanzania ni kwanini alisimamia uharamia wa kiasi hiki ndani ya nchi yake.

  Rais hawezi akawa hajui thamani ya miradi mikubwa nchini. Ni mfano mdogo, huo wizi wa minara pacha ni zaidi ya 5% ya budget ya Tanzania nzima kwa mwaka kwa wakati huo. Kamwe hawezi kuwa hajui. Hawezi akawa hajui EPA, rada, ndege ya rais na mazagazaga yote. Hapana huyu mtu haihitaji huruma ya Watanzania. Wengi wamekufa kutokana na maamuzi yake, ndio maana aliwatisha sana wabunge, na watanzania kwa ujumla.

  Ni wajibu kabisa kufikishwa mbele ya sheria aweze kueleza nini kilisababisha haya yote. Kitendo cha viongozi wa dini kuendelea kumwekea kivuli na ishara tosha kuonyesha jinsi wao wanavyofikiri tu juu ya maisha yao ambayo huneemeshwa na sadaka. Ni aibu kubwa, kuna kila sababu ya kubadilika
   
 5. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Anataka kugonganisha wananchi kwa mujibu wa imani zao.Kwani hadi sasa ni wachungaji na maaskofu wanao mtetea.(kama nimekosea naomba kukosolewa)
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Jan 27, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mh. Dr.Slaa mkuu kaza uzi hadi huyu jamaa tumfikishe asipotaka..Hayo ni mawazo ya mtu mmoja tu kwani hata Bush ana watu wanaomkubali na ikasemekana kuwa ni chuki dhidi yake.
  Pia nakuomba sana usitumie sana jina na imani ya dini kufikisha ujumbe wako kwani kimsingi (Kisiasa) huyo kiongozi wa dini ni raia wa Tanzania..Aliyozungumza huyo mchungaji hayahusiani hata kidogo na mafundisho ya dini yake...Ni wakati wetu sisi kuwaonyesha watu kama hawa kuwa tunaifahamu dini na tunaweza kuchambua mchele toka ktk pumba..
   
 7. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280
  Mkuu unafikri hata hao viongozi wa dini hawaijui dini? wanaijua sana. ni unafiki tuu. Kama Dr. Slaa alivyonena....wanakuwa wana-interests na michango/harambee za kuchangia makanisa yao. Na wala siamini kwamba waumini wao wana-share huo mtizamo wao wa kinafiki! Si uliona Arusha jinsi Lowassa alivyopokelewa na Askofu Laizer? Yaani at times nafika point naamini kwamba hata kama hizi dini zetu ni nzuri..lakini wanaozitafsiri wana mshkeli!

  Hivi ni lini tutaacha partisanship kwenye mambo ya msingi yanayotugusa wote? Hivi hatuwezi kujiuliza hizo hela walizoiba akina Liyumba (samahani simhukumu kesi bado iko mahakamni), akina Yona, Mramba, Karamagi..the list is endless...tujiulize kama WATANZANIA bila ushabiki wa hivi vyama visivyo na msaada wowote kwetu.....hizo hela zingefanya mangapi ya msingi kwa taifa letu? Personally nakubaliana na Dr. Slaa..no body hates Mkapa..ni kwamba madudu yake yamekuwa too much! Na honestly speaking taifa letu kusonga mbele tunahitaji kuwaadhibu watu kama Mkapa. Perhaps watakaofuata au kuwa na nia ya uongozi wa taifa letu..wajue kabisa uongozi ni dhamana na siyo kuwaibia wanachi.

  Mkapa kwa kweli anaudhi. Sijui hata nisemeje. Huyu mzee AMETUSALITI WATANZANIA.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,555
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Mkapa amefanya maamuzi mengi maovu lakini ya maamuzi hayo, ameyafanya kama rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo ana kinga dhidi ya kushitakiwa.
  Uamuzi wa kuanzisha kampuni ya AnnBen aliufanya kama Benjamin Mkapa ambayo ni haki yake kama raia mwingine yoyote wa Tanzania.
  Uamuzi wa kufanya biashara akiwa Ikulu, haya siyo majukumu ya rais kwa mujibu wa katiba, hivyo ile kinga ya kutoshitakiwa haihusiki. Kitendo cha kujiuzia Kiwira kwa bei poa, huku ni ukiukwaji wa maaadili ya uongozi ambayo nayo hayana kinga kwa mujibu wa katiba.
  Kwa kifupi, kifungu kile kile kilichompa rais kinga ya kutoshitakiwa, pia ni kifungu hicho hicho kimeiondoa kinga hiyo endapo rais atavunja katiba ama atakiuka maadili ya uongozi.
  Kutofikishhwa mbele ya vyombo vya sheria kwa Mkapa ni staha na heshima kwa rais mstaafu lakini sio kwa sababu ya kinga ya urais.
   
 9. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni kweni hakuna anayemchukia Mkapa ila tamaa yake ndiyo ilyomponza na kukiuka maagizo ya Baba wa Taifa.Labda alijua akishamzika hatajulikana kwa atakayoyafanya,awe mwazi kwa Watanzania la sivyo atakufa na laana ya kuvuja rasilimali za TZ.Kama ni machafuko anahamasisha yeye kwa kutafuta huruma ya Watanzania kupitia kwa mafisadi wenzake.Tuhuma zinazomkabili Mkapa wala hazihitaji kufutiwa kinga kwani ziko wazi kuwa alifanya biashara akiwa Ikulu kitu ambacho ni tafauti na kazi za kuongoza Nchi alizoapa kwayo.Serikali ichukue hatua kumfikisha Mkapa mahakamani ili akayaseme huko hayo anayoyasema kanisani.
   
 10. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu, kwa taarifa tu, Katiba inasema katika Ibara ya 46.-(1) "Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai." Ibara ya 46. -3, inatoa mamlaka kwa Bunge kama ifuatavyo. "Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la
  kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii."


  Pia ifahamike kuwa kila kipengele ndani ya Katiba hiyo kinajitegemea na hakuna kipengele kinachopinga kipengele kingine. Ndio maana hutumika maandishi kama "Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria yoyote iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo,....."

  Ukizingatia Katiba hiyo hiyo, nadhani ndio maana hakuna mtu aliethubutu kufungua mashitaka hayo mpaka sasa.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,555
  Trophy Points: 280
  Asante kuniwekea vifungu vya katiba, umenirudisha mbali enzi za kudesa.
  Japo jukumu la kutafsiri katiba na sheria ni la Mahakama kuu pekee, hebu naomba ionyeshe Ibara ya 46A kifungu (2)(a) na unitafsirie kama unamtafsiria mwananchi wa kawaida.
   
 12. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Haya Mkuu, hii hapa;

  46A.-(1)
  (2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja
  yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama
  inadaiwa kwamba Rais-
  (a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja
  Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;


  Tafsiri:
  Bila kuathiri masharti mengineyo...: Ina maana mashitaka yote ni lazima hazingatie kuwa kuna kinga iliyotangulia hapo juu (katika Ibara ya 46).
  hoja itatolewa isipokuwa kama Rais atavunja Katiba au sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.: Maana yake ni kwamba, Rais atakapovunja Katiba ama Maadili ya Viongozi wa Umma, Bunge linaweza kumuondolea kinga ya kushitakiwa. Maadili ya Viongozi wa Umma hayamkatazi Rais au kingozi mwingine yeyote kufanya biashara (sharti la kizuizi cha kufanya biashara liliondolewa kwenye Azimio la Zanzibar). Na vile vile, Katiba hamzuii Rais wala kiongozi mwingine yeyote kufanya biashara. Kwahiyo, kama shutuma ni kufanya biashara, Rais hawezi kuondolewa kinga kwa kuzingatia kifungu hiki.

  Kwa kuwa kuna tuhuma nyingine zinazomuhusu Rais mstaafu, kama kununua mgodi wa Makaa ya mawe wa Kiwira, inachotakiwa ni kuangalia taratibu zilizotumika katika kufikia maamuzi ya ununuzi huo. Kama akigundulika kuwa alitumia nguvu zake kama Rais, ama alitumia Rushwa ama alipata umiliki huo kinyume cha sheria, anaweza kufunguliwa mashitaka baada ya kuondolewa kinga. Uchunguzi haujafanywa kufikia uamuzi kama huo. Izingatiwe pia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano anayo mamlaka makubwa sana kisheria na kikatiba. matumizi hayo yakitumiwa kwa namna yoyote haiwezi kuwa uvunjaji wa sheria zilizopo. Kinachotakiwa ni kuangalia namna ya kuweka controls katika uwezo huo mkubwa.
   
 13. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kazi nzuri sana Dr. Slaa, huyu JAMBAZI Benjamin Mkapa lazima afikishwe kwenye vyombo vya sheria na kwenye suala lake naamini he is Guilty Until Proven Innocent. Hawa Maaskofu UCHWARA wanaomtetea wasituyeyushe hapa, Makazi ya Mkapa yanatakiwa yawe ni gerezani na sio kwenye mahekalu aliyoyajenga kwa pesa za kuwaibia watanzania.
   
  Last edited: Jan 28, 2009
 14. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mambo aliyoyafanya yeye kama Rais ndio yanayohusika, sio WIZI MTUPU alioufanya kama mjasiriamali Benjamini William Mkapa na mkewe, mtoto na wakwe zake

  Asha
   
 15. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #15
  Jan 28, 2009
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kimsingi kuna matatizo makubwa katika jamii yyetu yanasababishwa na viongozi wetu wa nchi na wale wa dini na madhehebu.

  Itakumbukwa kuwa awali kabisa rais Kikwete alisema waziwazi kuwa hana mpango wa kumshitaki Mkapa kwa kuwa eti alilitumikia taifa vizuri hivyo ni wajibu wetu tumwache apumzike kwa amani.

  Kama kiongozi mkuu wa nchi anatamka hivyo ni wazi kuwa mzee Mkapa anakila sababu ya kujitetea au kuwa na kiburi cha kusema atakavyo kuhusu tuhuma dhahiri na zisizo dhahiri zinazomwandama.Tulitegemea rais Kikwete angekuwa muungwana kwa kuweka mazingira ya kuruhusu Mkapa asafishwe au athibitishwe katika tuhuma husika.Kutokuweka mazingira hayo ni ushahidi tosha wa kuwepo kwa mkakati wa kufunika kombe mwanaharamu apite.

  Hivi karibuni Askofu Mdegella wa K.K.K.T Mkoani Iringa alitumia mimbara kumsafisha na kumsifia Mkapa.Kwa maneno mengine alikuwa anamsafisha mawaa yote ambayo jamii inamtuhumu kwayo.
  Kitendo hicho cha Askofu kimeacha maswali mengi magumu.Je, kazi ya kanisa na watumishi wake ni kuwasafisha watu makosa yao? Ni kigezo gani Askofu alitumia kumwona Mkapa ni safi?Kwa hakika ni vigumu kuamini kuwa Askofu anaufahamu undani wa utumishi wa Mkapa kwa kiasi cha kumtetea.

  Ndiyo maana nashawishika kusema kuwa kwa mazingira aliyokwisha kujenga rais Kikwete na Askofu Mdegella, ni wazi kuwa Mkapa anazidi kurushiwa maboya kusudi asizame.Wananchi tunaonekana machizi tu.Huu ndio utawala chongo.
   
 16. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Dr. Slaa wengi wanaweza sema ni political interest ila mimi nazikubali sana hoja zako. Kimsingi wakuu wa makanisa kumtetea mtu ambaye anatuhuma na pengine hajatubu huko kanisani sii jambo zuri. Wakristo wanautaratibu mzuri wa kutopinga kauli fulani ya Padri au Mchungaji kanisani isipokuwa katika vikao maalum hivyo ni vema wakuu hawaratibu wa dini wakaheshimu utaratibu huu. Isijefika mahali kukawa na mabishano kati ya wachungaji/mapatre/maaskofu na waumini wao.

  Kama nilivyowahi andika juu ya swala la mkapa, personally mkapa namkubali sana kama rais aliyekuwa na speech zilizotulia mfano hapa nilikuwa najikumbusha speech yake moja aliyoitoa kwenye mikutano ya Davos ''Davos Annual Meeting - Funding the War on Poverty'' unaweza google na wewe ukajikumbusha ni nzuri sana unajifeel kuwakilishwa na rais wako katika mambo mhimu. Mkutano huu ulisababisha nchi ifutiwe baadhi ya madeni.

  Hili niwala moja tuu kuna mengi mkapa anastail pongezi kama rais kama mabo ya uchumi ie inflation, tax collection, etc nilisha andika sana juu ya haya. Pamoja na yoooote Mkapa huyu huyu ndie mwenye tuhuma nyingi za kifisadi hivyo naungani na Dr. Slaa atoe tamko hama ni kweli au sio na kama ndivyo sheria ichukue mkondo wake. Ni hayo tu. Mi binafsi hata nkutane na mkapa leo bado namkubali sana japo siwezi kumtetea juu ya hizi tuhuma nikubwa eti, jamaaa wamevuna bro.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Jan 29, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,555
  Trophy Points: 280
  Mkuu Recta, asante. Hapa sasa nimekukubali na darasa limeeleweka. Tafsiri yangu ilikuwa kwa Ben kufanya biashara akiwa Ikulu, niliitafsiri kama ukiukwaji wa maadili ya uongozi. Lakini sasa nakubaliana na wewe. Pia nilitafsiri kinga ya rais, ilihusu utekelezaji wa majukumu yake ya urais kwa mujibu wa katiba, mimi nikahesabu deal ya Kiwira sio sehemu ya majukumu ya rais. Baada ya kunielimisha kuhusu madaraka makubwa aliyonayo rais wetu, sasa nimekubali na nimeelewa kwa nini kuna wakati sauti ziliwahi kupazwa rais apunguziwe madaraka.
  Baada ya darasa lako sasa nakubaliana na kauli ya rais Kikwete, "Tumwache Mkapa astaafu kwa amani".
  Pia nimekubali baadhi yetu wabongo, tunamaind sana Mbongo mwenzetu akipata. Ingekuwa Kiwira kapewa mwekezaji mzungu, hata kama kapewa bure, tusingesikia kelele kubwa hivi, lakini kapewa mwenzetu ni issue.
  Akipita mwarabu, mhindi ama mzungu, anaendesha latest model ya Mercedes S-Class, Vogue, Escalade, au Hammer , hakuna atakayetaka hata kumjua huyo ni nani, lakini akionekana mwenzetu, kunatokea interest ya ajabu wabongo kutaka kumjua huyo ni nani, akiwa na jina kubwa, maswali huishia hapo, akiitwa Juma, watadadisi zaidi huyu Juma ni nani haswa?. Jee shughuli zake ni nini, pesa kapata wapi?. Na zitafuata speculatios nyingi, mara EPA au Mzungu wa Unga etc. Kwa ngozi nyeupe safi, kwa ngozi nyeusi 'Wizi Mtupu' . Tubadilike.
   
 18. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #18
  Jan 29, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe kabisa. Ila ikumbukwe kwamba baada ya Mkapa kuchaguliwa kuwa Rais, kila jambo alilolifanya alilifanya akiwa Rais. Hata alipokuwa akiangalia TV, alikuwa Rais pia. Hakuna sekunde hata moja ambayo hakuwa Rais katika kipindi chote cha uongozi wake. Na ndio maana hata kiapo alikula kama "Mimi Benjamin William Mkapa, naapa kwamba.....". Nadhani wanasheria wanaweza kutafsiri vizuri zaidi vifungu hivi vya Katiba wakitaka kufanya hivyo.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,763
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana Asha kwa mchango wako mzuri.
   
 20. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hapa mkuu tupo ukurasa mmoja kabisaaaaaaa.hutuhitaji longolongo kamata mkapa piga pingu ,pandisha mahakamani kwa kutumia ofisi na madaraka vibaya..hivi Zambia waliweza wana nini na sisi tushindwe tuna nini
   
Loading...