sijui nini
JF-Expert Member
- Sep 29, 2010
- 2,553
- 1,292
SIKU moja baada ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, kunadi sera zake kwa njia ya mdahalo uliokuwa ukirushwa hewani moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV, umeonekana kuwapagawisha watu wa rika mbalimbali mitaani.
Hatua ya Dk. Slaa kunadi sera hizo kwa ufasaha kumewafanya wananchi wa rika mbalimbali kukunwa nazo, ambapo jana walionekana kukaa vikundi vidogo vidogo kwa ajili ya mhadahalo huo na kueleza namna wanavyomkubali kiongozi huyo.
Alipotembelea katika maeneo mbalimbali ya Mivinjeni-Kurasini, mwandishi wa habari hizi alikuta wananchi wakiwa katika vikundi na kujadili yaliyokuwa yakizungumzwa naye.
"Si siri, Dk. Slaa ndiye anayefaa kuwa rais wa nchi, si ulimcheki namna alivyokuwa akizungumza kwa umakini bila kutetereka," alisema John Macha.
Naye Peter Stanley, alisema sera za mgombea huyo ni nzuri na ikiwa zitatekelezwa kwa vitendo ikiwa kiongozi huyo atafanikiwa kutawala nchi ataiweka mahali pazuri tofauti na ilivyo sasa.
"Mi namkubali sana huyu jamaa, kabla ya kufika hapa aliibua mambo mengi ambayo yalitusaidia kuyajua mambo mbalimbali yanayofanywa na wakubwa wetu, hivyo tafadhali jamani tusimfanyie mzaha," alisema Rajabu Jumanne.
Naye Fidelis Mtangi, alisema watu kama Dk. Slaa ndio wenye kuhitajika nchini kwani wataiwezesha Tanzania kufika mahali pazuri na kuondokana na hali ya kutokuwa na maendeleo iliyopo sasa.
"Dk. Slaa anazungumzia masuala yake kwa kutaja vitu vya msingi na vichache sana, bila kusoma mahali popote, si kama mpinzani wake mkubwa wa CCM,
…anaweza kuzungumzia juu ya uboreshaji wa huduma ya afya na elimu na akaeleza kwa kifupi sababu ya serikali kufanya hivyo, namna ya kutekeleza hilo na muda wa kutekeleza. Lakini mpinzani wake amefikia hatua akikuta hospitali ambayo ina hadhi ya hospitali ya wilaya anaahidi itakuwa ya mkoa au ya rufaa," alisema Mtangi.
Naye Daudi Mwakalinga kutoka mkoani Iringa, aliiambia Tanzania Daima kwa njia ya simu kuwa ni wazi Dk. Slaa ametambua uelewa wa wananchi wake wanahitaji nini na yeye kama mgombea amefafanua kwa ufasaha na kwa hoja inayokubalika.
"Watu hawahitaji mgombea kuzungumzia ujenzi wa barabara inayojengwa wakati watu wanaiona kwa macho, watu hawataki mgombea kuzungumzia vitu vinavyofanyika, ambavyo vimetengewa bajeti ya serikali, kwa kuwa bajeti hiyo inapitishwa mwaka hadi mwaka na wabunge wanahusika nayo, hivyo haina maana ya mgombea kuweka kwenye ahadi yake," alisema Mwakalinga.
CHADEMA::israel::israel:
CCM: 😛eep:😛eep: