Dk. Slaa awapagawisha wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa awapagawisha wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sijui nini, Oct 25, 2010.

 1. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  SIKU moja baada ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, kunadi sera zake kwa njia ya mdahalo uliokuwa ukirushwa hewani moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV, umeonekana kuwapagawisha watu wa rika mbalimbali mitaani.

  Hatua ya Dk. Slaa kunadi sera hizo kwa ufasaha kumewafanya wananchi wa rika mbalimbali kukunwa nazo, ambapo jana walionekana kukaa vikundi vidogo vidogo kwa ajili ya mhadahalo huo na kueleza namna wanavyomkubali kiongozi huyo.

  Alipotembelea katika maeneo mbalimbali ya Mivinjeni-Kurasini, mwandishi wa habari hizi alikuta wananchi wakiwa katika vikundi na kujadili yaliyokuwa yakizungumzwa naye.

  "Si siri, Dk. Slaa ndiye anayefaa kuwa rais wa nchi, si ulimcheki namna alivyokuwa akizungumza kwa umakini bila kutetereka," alisema John Macha.

  Naye Peter Stanley, alisema sera za mgombea huyo ni nzuri na ikiwa zitatekelezwa kwa vitendo ikiwa kiongozi huyo atafanikiwa kutawala nchi ataiweka mahali pazuri tofauti na ilivyo sasa.

  "Mi namkubali sana huyu jamaa, kabla ya kufika hapa aliibua mambo mengi ambayo yalitusaidia kuyajua mambo mbalimbali yanayofanywa na wakubwa wetu, hivyo tafadhali jamani tusimfanyie mzaha," alisema Rajabu Jumanne.

  Naye Fidelis Mtangi, alisema watu kama Dk. Slaa ndio wenye kuhitajika nchini kwani wataiwezesha Tanzania kufika mahali pazuri na kuondokana na hali ya kutokuwa na maendeleo iliyopo sasa.

  "Dk. Slaa anazungumzia masuala yake kwa kutaja vitu vya msingi na vichache sana, bila kusoma mahali popote, si kama mpinzani wake mkubwa wa CCM,

  …anaweza kuzungumzia juu ya uboreshaji wa huduma ya afya na elimu na akaeleza kwa kifupi sababu ya serikali kufanya hivyo, namna ya kutekeleza hilo na muda wa kutekeleza. Lakini mpinzani wake amefikia hatua akikuta hospitali ambayo ina hadhi ya hospitali ya wilaya anaahidi itakuwa ya mkoa au ya rufaa," alisema Mtangi.

  Naye Daudi Mwakalinga kutoka mkoani Iringa, aliiambia Tanzania Daima kwa njia ya simu kuwa ni wazi Dk. Slaa ametambua uelewa wa wananchi wake wanahitaji nini na yeye kama mgombea amefafanua kwa ufasaha na kwa hoja inayokubalika.

  "Watu hawahitaji mgombea kuzungumzia ujenzi wa barabara inayojengwa wakati watu wanaiona kwa macho, watu hawataki mgombea kuzungumzia vitu vinavyofanyika, ambavyo vimetengewa bajeti ya serikali, kwa kuwa bajeti hiyo inapitishwa mwaka hadi mwaka na wabunge wanahusika nayo, hivyo haina maana ya mgombea kuweka kwenye ahadi yake," alisema Mwakalinga.


  CHADEMA::israel::israel:
  CCM: :peep::peep:
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,364
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo Jk aliachia ngazi za kutawala.....................
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kampe kura 31/10!
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  sirogwi hata chembe
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  kesho naanza safari ya kwenda Mwanza kwa lengo moja nalo ni kupiga kura ili kuuondoa utawala wa kiimla nchini kwangu

  Hon.dk Slaa ndo Rais wangu. sina utani juu ya hili
   
 6. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pepoziiiiiiiiiii...........................................
   
 7. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mie hata kama nitakuwa na drip ya malaria nitaweka ki-memo ili docta aruhusu nikapige kura na drip yangu. Sitaki Dr. Slaa akose kura yangu.


   
 8. M

  MULANGIRA Member

  #8
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hakikisheni kuwa wazazi, watoto, wajomba na jamaa wote kuwa wanampigia kura Dr. Slaa tafadhali hiki ni kitu cha muhimu sana. Kura zetu zisigawanyike.
   
 9. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wananchi sasa wameelewa nini wanataka!!!

  God bless Tanzanians.

  VOTE FOR CHADEMA
   
 10. k

  kingwipa1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2010
  Joined: Jul 2, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Nitasafiri ijumaa kwenda dar kwa ajili ya kujipanga kumpigia kura Slaa (PhD) na kuilinda kura yangu. Mimi na rafiki zangu tumeamua kufanya hivyo ili kuongeza kura zetu kwenye ushindi huu mkubwa wa watanzania wa kutafuta kuikomboa nchi yetu.

  usisahau nina zaidi ya kura za CCM nilizozipeleka CHADEMA mwaka huu. Nikiwa kama mmoja wa wana-CCM waasi kwani hata kadi niliipoteza na wala sihitaji kuwa nayo tena, nimeamua kuondoka na watu wengi ili yale majigambo ya ccm ya kuwa na wanachama wengi yathibitike ni uongo. wanannihesabu mimi kuwa mmoja wao ilhali si mmoja wao kwa kuwa sikuwaaga na wala sijabisha hodi chadema, isipokuwa moyo wangu umeenda huko na matumaini mapya ya nchi ni Slaa (PhD) na si Kikwete (BA)
   
 11. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli hata Ma-waitress/Mawaiter waliokuwa wanashudia... Mwanzoni walidhani ni Mipira ya Ughaibuni... Lakini walikuja-ng'amua ni Mdahalo... Walikuwa wampigie kura Kikwete lakini wamekata shauri... HAWADANGANYIKI!!!
   
 12. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi, Mke wangu, Wadogo zangu wanne na mama ni Dr Slaa. Bado namshawishi mzee naye sasa ameanza kumkubali ze Dr! So count 7 votes from my family...wewe watakoma this year!
   
 13. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hayo ndo tulikuwa tukitaka watu waelewe nani anaupendo wakweli na watanzania siyo upendo wamafisadi tuu!
   
 14. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kutambua kuwa una tatizo kuna kupa uwezo wa kulichambua na kulitafutia dawa ama jawabu lake. Dr Slaa ametambua nini matatizo ya Tanzania, ameweza kuyachambua kwa kina na ameweza kupata majibu ya matatizo hayo. Hivyo itakuwa ni jambo la hekima sana kwa Watanzania kumpa Dr Slaa nafasi ya kuwa Kiongozi wetu wa juu ili aweze kutatua matatizo yetu. Ni jambo la aibu na kusikitisha sana kuona Jakaya hajui kwanini Tanzania ni masikini pamoja na kuwa amekuwa Raisi wetu kwa muda wa miaka mitano. Hii inanipa jawabu kwamba Jakaya hajui anafanya nini Ikulu. Watanzania hatuna sababu ya kumrudisha Jakaya Ikulu, aende Bagamoyo ama Msoga kulima mananasi.
   
 15. p

  paison Member

  #15
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dr.anafaa,mimi na nyumba yangu tutamchagua.
   
 16. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ambaye atapigia kura ccm katika nyumba yangu nikigundua, atakula polisi!
   
 17. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  nimeshau na kazini kwangu,wafanyakazi wa kampuni yangu wako kama 89 wote wanaenda kwao lengo ni kuhakikisha slaa anashinda, potelea mbali acha kampuni ipate hasara
   
 18. K

  Kibento Member

  #18
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  frm nw na kuendelea,rais wa awam ya 5 wa tz ni Dr.wilbroad slaa,
  kwa m2 muelewa huhitaji kuhoji,kikwete aende kufanya ufisad na akina rosti tamu ya ndizi (rostam aziz)
   
 19. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Go Slaaa
   
 20. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Na tulio nje ya nchi tutampaje kura Rais Mpya????????
   
Loading...