Dk. Slaa ashuhudia mjamzito akizidiwa foleni kujiandikisha BVR; atoa maagizo

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,071

Katibu Mkuu Dk. Slaa anaendelea na ziara ya siku tatu mkoani Kagera ambayo itamfikisha katika maeneo ya Bukoba, Karagwe na Muleba ambapo katika siku yake ya kwanza wakati akikagua uandikishaji wa wapiga kura katika Daftari la Kudumu kwa mfumo wa BVR, ameshuhudia kasoro nyingi, ikiwemo wahusika kutofuata sheria zinazoelekeza kuhusu namna ya kuwahudumia watu wenye mahitaji au makundi maalum, hali ambayo inaweza kusababisha kuwakosesha haki ya kuandikishwa...

........

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa (pichani), amewataka waandikishaji na wasimamizi wa uandikishaji wa wananchi kielektroniki katika daftari la kudumu la wapiga kura (BVR), kutoa kipaumbele kwa kina mama wajawazito, wazee, wagonjwa na walemavu, ili waweze kujiandikisha bila kupata madhara.


Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Hamugembe jana baada ya kuzunguka kwenye baadhi ya vituo vya uandikishaji, Dk. Slaa alisema kuwa kitendo alichokutana nacho katika manispaa ya Bukoba cha kukuta mama mjamzito amezimia kutokana na kukaa kwa muda mrefu katika mstari bila kuandikishwa, hajafurahishwa nacho.

“Kama waandikishaji na wasimamizi wa zoezi hili hawafahamu vizuri sheria ya uchaguzi, basi waitafute waisome ili waelewe kuwa makundi haya ya watu hayapaswi kukaa katika mistari muda mrefu, badala yake inabidi wanapofika wahudumiwe na kuondoka,” alisema.

Kutokana na hali hiyo alimwagiza mwenyekiti wa Chadema Bukoba mjini, Victor Sherejey, kufuatilia katika vituo vyote na kuhakikisha kasoro zilizobainika zinafanyiwa kazi, ikiwamo ya makundi hayo ya watu kuandikishwa bila kusumbuliwa.
Alisema kuwa kila mwananchi mwenye sifa bila kujali hali aliyonayo anapaswa kuandikishwa na kuwa hiki ni kipindi kigumu kuliko vipindi vyote maana uandikishaji ndiyo mwanzo wa kupiga kura, ambaye hatajiandikisha hawezi kulalamika baadaye dhidi ya viongozi wasiofaa watakaochaguliwa.

Aidha Dk. Slaa alizungumzia sheria inayolenga kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari na kuwa kitendo cha serikali kuandaa kupeleka bungeni muswada wa sheria ya habari kwa hati ya dharura, kuzifunga redio na vyombo vingine, zisitangaze matokeo ya uchaguzi, ili serikali iliyoko madarakani iweze kufanikisha azma yake ya kuiba kura.

“Serikali ina maana gani kuzitaka redio binafsi zijiunge na redio ya taifa kila ifikapo saa mbili, muda huo watu ndipo wanakuwa wametoka kuhangaika na shughuli za hapa na pale wanataka kutulia kusikiliza taarifa za ukweli kutoka vyombo mbalimbali, leo hii serikali inasema redio zote zijiunge na redio ya taifa, huu ni ukandamizaji wa vyombo vya habari,” alisema.

Aliitaka serikali kutowafunga midomo waandishi wa habari hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu, maana wananchi wa Tanzania wana haki ya kupata habari sahihi na kwa wakati wanaotaka.

CHANZO: NIPASHE





 
  • Thanks
Reactions: jme
Atoe maagizo kwani yeye ni nani? Hapo wa kulaumiwa hao wahaya. Hiyo haikubaliki hata kidogo. Utaratibu wa kujali wajawazito, wagonjwa, walemavu na wazee upo kila kona ya nchi hii. Ina maana huko kwa wahaya hakuna utaratibu huo? Wamelewa na nini hao?
 
Atoe maagizo kwani yeye ni nani? Hapo wa kulaumiwa hao wahaya. Hiyo haikubaliki hata kidogo. Utaratibu wa kujali wajawazito, wagonjwa, walemavu na wazee upo kila kona ya nchi hii. Ina maana huko kwa wahaya hakuna utaratibu huo? Wamelewa na nini hao?

Watakuwa wamelewa rubisi.
 
Atoe maagizo kwani yeye ni nani? Hapo wa kulaumiwa hao wahaya. Hiyo haikubaliki hata kidogo. Utaratibu wa kujali wajawazito, wagonjwa, walemavu na wazee upo kila kona ya nchi hii. Ina maana huko kwa wahaya hakuna utaratibu huo? Wamelewa na nini hao?
Mkiambiwa mechoka mnabisha kweli mechoka mnaitaji kupumzika
 
Dah seriously nimeguswa na ushauri na maelekezo ya Dr.W.Slaa kuwapa kipaumbele makundi maalum kwenye jamii hasa wajawazito wagonjwa wazee walemavu na akina mama

Bravo Dr Slaa
 
Last edited by a moderator:
Hilo sio suala la kutoa maamuzi yeye sio mwajiri wao!taratibu ziko wazi ni tukio moja tu ambalo limesababishwa na wazembe wachache wasiojua majukumu yao kwa kushindwa kutoa kipaumbele kwa watu wa makundi maalumu!
 
Acha ukabila. Una maana gani kutumia neno wshaya. Hakuna makabila mengine kagera? Chunga ulimi wako
 
Back
Top Bottom