nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
MALUMBANO yanayoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baina ya vigogo wa chama hicho na Jumuiya ya Umoja wa Vijana yamebeba siri nzito, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.
UVCCM inadaiwa imekuwa ikiyatumia matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 30, mwaka jana ya mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, ambaye alipata kura milioni mbili (asilimia 26) pamoja na chama chake kupata wabunge 23 wa majimbo kutoka watano.
Hoja inayojengwa na UVCCM ni kuwa matokeo hayo ya Slaa pamoja na Chadema kwa kiwango kikubwa yamepatikana kwa sababu ya matamshi ya kukikosoa chama na serikali bila kufuata taratibu za vikao vya chama hivyo kukifanya kiyumbe na kukosa imani kwa wananchi.
Dk. Slaa anadaiwa kuchafua upepo ndani ya CCM hasa katika kipindi hiki ambacho Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho tawala inatarajia kukutana mwezi ujao kujadili njia za kukiepusha chama na janga la kutoaminiwa.
Kwa mujibu wa vyanzo kutoka ndani ya CCM vinaeleza kuwa vurugu zinazoonekana sasa zina lengo la kuwaumiza baadhi ya vigogo wanaoonekana kuwa tishio katika chaguzi zijazo za chama na za taifa.
Chama hicho mwakani kinatarajia kufanya uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na wale wa Kamati Kuu (CCM), vyombo ambavyo ni nyeti kwa kuwa ndivyo vyenye jukumu la kupitisha majina ya wanaotaka kuwania nafasi za uongozi ndani na nje ya chama.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, vimebainisha kuwa vikao vya NEC vitakuwa vikali na kuna uwezekano mkubwa baadhi ya vigogo wakapoteza nyadhifa za kichama walizonazo ili kukiondoa chama kutoka kwenye gamba linalodaiwa kubeba uozo mwingi.
Dhana hiyo ya kujivua gamba kwa CCM ilitolewa mwanzoni mwa mwaka huu na Rais Jakaya Kikwete mkoani Dodoma wakati wa kilele cha miaka 34 ya kuzaliwa kwa chama hicho, kuwa kimepoteza mvuto na kina matatizo ambayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa.
Wakati CCM ikionekana kusumbuliwa na kivuli cha Dk. Slaa, Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, inadaiwa ameingia kwenye mapambano bila kujua ni watu wa aina gani wapo nyuma ya wale anaopambana nao.
Sumaye kwa kujua au kutokujua, yupo katika hatari ya kupambana na Rais Jakaya Kikwete badala ya UVCCM, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.
Wakati juzi Sumaye akiitisha mkutano na waandishi wa habari kujibu mashambulizi yaliyoelekezwa kwake na UVCCM, Makamba na Lukuvi, inadaiwa Makamba alitoa maelekezo kwa jumuiya hiyo kumjibu Sumaye.
Tanzania Daima Jumapili limepata taarifa kuwa Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa na Katibu Mkuu wake, Martine Shigela, walipokea maagizo ya kuipitia taarifa ya Sumaye na kuitolea ufafanuzi kwa vyombo vya habari.
Taarifa kutoka CCM zinabainisha kuwa Shigela alitoa tamko la kumpinga Sumaye kwa baraka za Makamba, ambaye naye anadaiwa alizipata kwa Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.
Wachambuzi wa masuala ya siasa wamelidokeza Tanzania Daima Jumapili kuwa kitendo cha Sumaye kulishambulia tamko la vijana wa Mkoa wa Pwani, ambao miongoni mwa wajumbe wake ni Ridhiwani Kikwete, kilionekana kumlenga Rais Kikwete.
Wanaweka wazi kuwa Sumaye atakabiliana na wakati mgumu katika kikao cha NEC, hasa baada ya wajumbe kujenga dhana kuwa anataka kuwania urais mwaka 2015.
Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa malumbano yanayoendelea baina ya vigogo na uongozi wa UVCCM yanaweza kutumiwa na wajumbe wa NEC kuwashughulikia wenzao.
UVCCM inadaiwa imebeba ajenda za siri za kulumbana na vigogo kwa lengo la kuwaharibia sifa walizonazo ndani na nje ya chama ili wasiweze kutimiza malengo yao ya kuwania uongozi.
Inaelezwa kuwa jumuiya hiyo imekuwa ikitumia matokeo ya kura za Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana kulumbana na vigogo wa CCM kuwa hawakukisaidia chama kwa kiwango kilichotakiwa bali walikuwa wakiangalia umaarufu binafsi.
UVCCM inasema umaarufu wa aliyekuwa mgombea wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, ulisababishwa na malumbano na maamuzi mabovu ya viongozi wa CCM ambao kwa wakati tofauti walikuwa wakitoa matamshi ya kukikosoa chama nje ya vikao husika.
Hata hivyo, baadhi ya makada wa CCM, waliweka wazi kuwa matamshi hayo ya jumuiya hiyo si sahihi, kwani yenyewe ndiyo iliyokuwa na jukumu kubwa la kuwashawishi vijana kuwachagua wagombea wa chama hicho tawala.
Makada hao wanaweka wazi kuwa Chadema walikuwa wakiungwa mkono na idadi kubwa ya vijana kutokana na kujipanga kwao na si kwa sababu ya makada wa CCM kulumbana hadharani.
Walibainisha kuwa jumuiya hiyo hivi sasa inaendeshwa kwa utashi wa kundi la wachache ambalo lina ajenda za kuunda mitandao itakayowasaidia katika mbio za ujumbe wa NEC, CC na kinacholengwa zaidi ni urais wa mwaka 2015.
Hata hivyo UVCCM kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Martine Shigela, ilikanusha madai hayo ambapo alisema dhamira yao ni kukisafisha chama ili kirejeshe umoja, amani na mshikamano kwa wananchi. Shigela alisema vijana ndio injini ya chama, hivyo ni lazima washauri na kukemea pale inapoonekana malumbano yanayoendelea hivi sasa baadhi ya makundi yanatumia mbinu chafu.