Dk. Slaa aichafua CCM; Kuwaponza vigogo

Dk. Slaa aichafua CCM; Kuwaponza vigogo

kwa hiyo mkwele na Sumaye nani zaidi mnadhani?

Hawa wote ni vibaka. Sumaye naye hafai hata kidogo! Leo tu mmemsahau mambo yake? Leo anatumia weakness ya watanzania kujijenga upya kisiasa ili aje agombee urais 2015. HATUTAKI!

Katika hao zaidi ni Dr. Slaa!
 
MALUMBANO yanayoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baina ya vigogo wa chama hicho na Jumuiya ya Umoja wa Vijana yamebeba siri nzito, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.
UVCCM inadaiwa imekuwa ikiyatumia matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 30, mwaka jana ya mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, ambaye alipata kura milioni mbili (asilimia 26) pamoja na chama chake kupata wabunge 23 wa majimbo kutoka watano.

Hoja inayojengwa na UVCCM ni kuwa matokeo hayo ya Slaa pamoja na Chadema kwa kiwango kikubwa yamepatikana kwa sababu ya matamshi ya kukikosoa chama na serikali bila kufuata taratibu za vikao vya chama hivyo kukifanya kiyumbe na kukosa imani kwa wananchi.

Dk. Slaa anadaiwa kuchafua upepo ndani ya CCM hasa katika kipindi hiki ambacho Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho tawala inatarajia kukutana mwezi ujao kujadili njia za kukiepusha chama na janga la kutoaminiwa.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka ndani ya CCM vinaeleza kuwa vurugu zinazoonekana sasa zina lengo la kuwaumiza baadhi ya vigogo wanaoonekana kuwa tishio katika chaguzi zijazo za chama na za taifa.
Chama hicho mwakani kinatarajia kufanya uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na wale wa Kamati Kuu (CCM), vyombo ambavyo ni nyeti kwa kuwa ndivyo vyenye jukumu la kupitisha majina ya wanaotaka kuwania nafasi za uongozi ndani na nje ya chama.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, vimebainisha kuwa vikao vya NEC vitakuwa vikali na kuna uwezekano mkubwa baadhi ya vigogo wakapoteza nyadhifa za kichama walizonazo ili kukiondoa chama kutoka kwenye gamba linalodaiwa kubeba uozo mwingi.

Dhana hiyo ya kujivua gamba kwa CCM ilitolewa mwanzoni mwa mwaka huu na Rais Jakaya Kikwete mkoani Dodoma wakati wa kilele cha miaka 34 ya kuzaliwa kwa chama hicho, kuwa kimepoteza mvuto na kina matatizo ambayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa.
Wakati CCM ikionekana kusumbuliwa na kivuli cha Dk. Slaa, Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, inadaiwa ameingia kwenye mapambano bila kujua ni watu wa aina gani wapo nyuma ya wale anaopambana nao.
Sumaye kwa kujua au kutokujua, yupo katika hatari ya kupambana na Rais Jakaya Kikwete badala ya UVCCM, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.

Wakati juzi Sumaye akiitisha mkutano na waandishi wa habari kujibu mashambulizi yaliyoelekezwa kwake na UVCCM, Makamba na Lukuvi, inadaiwa Makamba alitoa maelekezo kwa jumuiya hiyo kumjibu Sumaye.
Tanzania Daima Jumapili limepata taarifa kuwa Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Benno Malisa na Katibu Mkuu wake, Martine Shigela, walipokea maagizo ya kuipitia taarifa ya Sumaye na kuitolea ufafanuzi kwa vyombo vya habari.

Taarifa kutoka CCM zinabainisha kuwa Shigela alitoa tamko la kumpinga Sumaye kwa baraka za Makamba, ambaye naye anadaiwa alizipata kwa Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wamelidokeza Tanzania Daima Jumapili kuwa kitendo cha Sumaye kulishambulia tamko la vijana wa Mkoa wa Pwani, ambao miongoni mwa wajumbe wake ni Ridhiwani Kikwete, kilionekana kumlenga Rais Kikwete.
Wanaweka wazi kuwa Sumaye atakabiliana na wakati mgumu katika kikao cha NEC, hasa baada ya wajumbe kujenga dhana kuwa anataka kuwania urais mwaka 2015.
Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa malumbano yanayoendelea baina ya vigogo na uongozi wa UVCCM yanaweza kutumiwa na wajumbe wa NEC kuwashughulikia wenzao.

UVCCM inadaiwa imebeba ajenda za siri za kulumbana na vigogo kwa lengo la kuwaharibia sifa walizonazo ndani na nje ya chama ili wasiweze kutimiza malengo yao ya kuwania uongozi.
Inaelezwa kuwa jumuiya hiyo imekuwa ikitumia matokeo ya kura za Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana kulumbana na vigogo wa CCM kuwa hawakukisaidia chama kwa kiwango kilichotakiwa bali walikuwa wakiangalia umaarufu binafsi.

UVCCM inasema umaarufu wa aliyekuwa mgombea wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, ulisababishwa na malumbano na maamuzi mabovu ya viongozi wa CCM ambao kwa wakati tofauti walikuwa wakitoa matamshi ya kukikosoa chama nje ya vikao husika.
Hata hivyo, baadhi ya makada wa CCM, waliweka wazi kuwa matamshi hayo ya jumuiya hiyo si sahihi, kwani yenyewe ndiyo iliyokuwa na jukumu kubwa la kuwashawishi vijana kuwachagua wagombea wa chama hicho tawala.

Makada hao wanaweka wazi kuwa Chadema walikuwa wakiungwa mkono na idadi kubwa ya vijana kutokana na kujipanga kwao na si kwa sababu ya makada wa CCM kulumbana hadharani.
Walibainisha kuwa jumuiya hiyo hivi sasa inaendeshwa kwa utashi wa kundi la wachache ambalo lina ajenda za kuunda mitandao itakayowasaidia katika mbio za ujumbe wa NEC, CC na kinacholengwa zaidi ni urais wa mwaka 2015.
Hata hivyo UVCCM kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Martine Shigela, ilikanusha madai hayo ambapo alisema dhamira yao ni kukisafisha chama ili kirejeshe umoja, amani na mshikamano kwa wananchi. Shigela alisema vijana ndio injini ya chama, hivyo ni lazima washauri na kukemea pale inapoonekana malumbano yanayoendelea hivi sasa baadhi ya makundi yanatumia mbinu chafu.

Story ya kuunga unga kumpatia umaarufu Padre Slaa! Haina Connection yoyote!
 
Story ya kuunga unga kumpatia umaarufu Padre Slaa! Crap ya Kichadema!
 
Discussion hapa ni tamu sana. Kuna msemo nadhani upo kwenye vitabu vya dini fulani usemao kwamba majira na nyakati yapo tayari kwa mavuno isipokuwa hakuna wavunaji. Sasa ukiangalia hali ya kisiasa nchini, na watu wengi walio walivyochoka, wagonjwa kupindukia, wamekata tamaa, hawajui kesho kama watakula unapata picha clear kabisa kuwa watu wana kiu ya mabadiliko, na wanahitaji mabadiliko halisi yatakayo gusa penyewe si mabadiliko feki.

Sasa pamoja na watu kuichukia CCM lakini wakitafuta mbadala wake ni nani, unakuta hakuna. CHADEMA sasa kinapaswa kucapitalize kwenye mindset za watanzania wengi hasa wale walio vijana sasa na kuwaaminisha kuwa kama chama wanastahili kuwa mbadala wa CCM.

Hii kazi ya kuwaaminisha watu kuwa wewe unastahili kuongoza serikali badala ya CCM ndio kazi amabayo CHADEMA wanapaswa kuifanya sasa. Si tu kufanya maandamano ambayo mi naona ni rahisi watu kuyatafsiri kama vile mnachochea au mnafanya ghasia. Si tu kureact baada ya kusikia kashfa ya ufisadi. Sisemi kwamba haya yasifanyike, la, yafanyike pamoja na mikakati mingine proactive kama vile kubuni namna ya kuongeza viable membership, kudhamini majukwaa mbalimbali za kisiasa kuanzia vyuo vikuu mpaka sekondari, kuonyesha exemplary governance katika vijiji, wilaya au manispaa ambazo tayari zinaongozwa na CHADEMA. Na la mwisho, ambalo naona ni la muhimu zaidi, kuweka mikakati ya kukubalika miongoni mwa jamiii ya waislam Tanzania. Tusijidangaye huwezi kwenda ikulu mpaka angalau ukubalike kwa nusu ya electorate waislam. Lakini ninachokiona kwa chadema naona kama vile waislamu wote wameapa kutoikubali chadema. Ni lazima kuweka mikakati ya kubuild bridges between CHADEMA and the moslem community.
 
Tatizo la Jf ni

kupenda CDM kiasi cha kutotaka kusikia mawazo yanayopingana na yenu . Hakim anaependa matusi yenu, bora muendelee na upofu wenu

Ndugu yangu sailor1, JF si ya CDM. Ni free forum kwa kila mwenye teknohama ya kuingia. Chukulia JF kama sampuli(sample) ya watanzania. Ni kama ukitaka kufanya utafiti utatumia sehemu ya jamii itakayowakilisha jamii husika. Matokeo ya utafiti yatareflect picha ya jamii nzima.
Haya mawazo yanayowakilishwa JF, hayamaanishi ni wapenda CDM, ila ni jamii iliyochoka na mfumo kandamizi, mfumo fisadi, mfumo wa kinyonyaji wa utawala tajiri wa CCM dhidi ya watanzania masikini.
Unachokishuhudia hapa ni mawazo ya kimapinduzi yaliyozaliwa na kukomazwa na CCM yenyewe.
Na kama ungefanya utafiti kwa members wote wa JF ambao kwa muono wako unadhani wanakishabikia CDM utagundua kuwa si zaidi ya 10% (kama inaweza fika) wenye kadi ya CDM.
Sailor1, watanzania wamechoka na CCM sababu kila mtanzania anajua including JK.
Kama kutofautiana na ukoloni wa CCM ndo unaita ni wana CDM and so be it.
Truly Tanzanian
 
MALUMBANO yanayoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baina ya vigogo wa chama hicho na Jumuiya ya Umoja wa Vijana yamebeba siri nzito, Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.
UVCCM inadaiwa imekuwa ikiyatumia matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 30, mwaka jana ya mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, ambaye alipata kura milioni mbili (asilimia 26) pamoja na chama chake kupata wabunge 23 wa majimbo kutoka watano.

Hoja inayojengwa na UVCCM ni kuwa matokeo hayo ya Slaa pamoja na Chadema kwa kiwango kikubwa yamepatikana kwa sababu ya matamshi ya kukikosoa chama na serikali bila kufuata taratibu za vikao vya chama hivyo kukifanya kiyumbe na kukosa imani kwa wananchi.

Dk. Slaa anadaiwa kuchafua upepo ndani ya CCM hasa katika kipindi hiki ambacho Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho tawala inatarajia kukutana mwezi ujao kujadili njia za kukiepusha chama na janga la kutoaminiwa.

....ndugu wakigombana,chukua jembe kalime;wakipatana,chukua kapu kavune...
 
kuimaliza kwa ccm sas ahivi sio kwa bunduki bali ni kwa kutumia busara,vita basi tena vimepitwa na wakati,sasa kumekuja mjadala wa katiba,kuna mambo ambayo lazima tuyatoe katika viongozi ili kuwanyima fursa ya kutawala ki udi tector,, kwa mfano

1.Rais asipewe power kuwa yeye ndiie amiri jeshi mkuu-hii hata ulaya hakuna kuwa rais ndio amerijeshi mkuu,,,hapa ndio udictetor unapokuja kama gadafi.
2.Iwepo sheria ya kumshitaki rais ikiwa amepewa urais kwa kutimia udanganyifu,na kuhoji tume,,pamoja na ule urais aliopewa..
3. kuwepo kwa sheria ambayo inayo uwezo kwa wananchi kuwa na fursa ya kumuondoa kiongozi wao japo kwa thelusi 2 ,ikiwa mbunge hawafai kwa wanachi basi wananchi wanaweza kupeleka maoni yao kwa tume ya uchaguzi ili kuondolewa mbunge huyo,,ha ta rais na viongzi wengine..
4. Tume ya uchaguzi uindwe kwa kupitia chombo cha sheria bunge sio rais kuteuwa viongozi wa tume ili kulinda wazifa wake na chama chake.
5. kuweka sheria kwa vikosi vya ulinzi kulinda haki ya mwananchi na usalama,na kuweka hatua za kisheria pindi mmoja wa jeshi la usalama nchini kumzuru mwananchi achukuliwe hatua ipasavyo.
6.kuwepo kwa wagombea binafsi.
7. vyama vya siasa vipewe uhuru kwa wananchi,na jumua za kiraia pamoja na wananchi wenyewe.
8.wananchi washirikishwe kwa jambo lolote lile kwa ajili ya nchi yao,kwa mfano kujiunga kwa EAC,lakima wananchi washirikishwe katika hili kwa kupewa nafasi wapige kura ya maoni sio viongiz kujiamulia wenyewe.
9. kuwepo na sheria ya viongiz ambao wamepata uwongozi huo kwa kutmia vyama vyao kuwapa uwongzi badala ya kuwatumikiwa wanachi wote wakawa wanawatumikia wanacha wake,,,sheria zimuhukumu..

MENGINE MUTAMALIZIA

HAPo ccm lazima itatoka madarakaniii

Ningeomba watanzania wote tujadili muungano wenye fair baina za pande zote mbili tanganyika na zanzibar ,,,tusiwe na jazba na mukari na tuondoe tofauti zetu...kila upande upewe uhuru wa kushiriki,,na maamuzi yake sio kutawaliana..

NAWAKILISHA.
 
Inakuja tsunami kuliko ile ya japan kwenye vyama vya siasa. Wananchi tumezidi ugeugeu, tungekwua wote tunaongea moja lazima hawa CCM na vichaa wote tungewang'oa. Tukiacha tu unafiki 2015 hawapo.
 
Umenena vyema sana,

Huwa naonekanaga ant-chadema humu, lakini ukiangalia kwa umakini seriousness ya chadema ni ndogo sana. Ukiangalia jinsi walivyompata mgombea mwenza wa urais ilikuwa ni kama wamekurupushwa, it was a big shame!

Umesema jambo la maana KAMA WAKIJIPANGA vizuri! hili ni neno zito sana , kuna mambo mengi mno ambayo chadema wameishakosea, wanaogelea kwenye matope na kuinuka kwao ni kazi sana, kama ulivyosema wananchi wako tayari KUAMINISHWA TU kuwa Chadema can lead the country! ni nguvu kidogo yenye akili sana.

Tuhuma za udini ( ambazo wanapakwa nazo na si kweli kuwa kuna udini) ni tuhuma za ku-deal nazo seriously! tuhuma za ukabila na ufanya biashara nazo hazipaswi kuwekwa kando.

My teknik ni simple kuwaamsha kwa vijembe na mitusi

Leo hii saa hii wakati huu jitayarisheni kwa 2015! kuwa wizi wa kura ulifanyika ni kichekesho sana na huwa haiingii akilini

CCM ndiyo imekwisha, wakuingia madarakani hataingia ki-RAHISI kama wengine wanavyojipa moyo, hawa jamaa na deal zao chafu wanajua tu wakiingia wapinzani wamekwisha!!! IS NOT EASY wala msipeane moyo semeni na shaurianeni kama huyu mpendwa hapa.

Wengine tunaochukulia kuwa ukiwa kwenye siasa basi unajua siasa tukiona kitu fulani hakifanyiki huwa hatuna lugha nzuri saana ni VIJEMBE tu kama si mijembe ili MUAMKE!

Lakini Web wewe uko upande gani? Wa nchi, wa CCM ama wa CHADEMA? Some of us are for the country's future so for me it does not matter whatever available resources can be used to build future; unfortunately I see CHADEMA for politics to be an avenue where we can take our national agenda for its not yet developed into a dominant system na baadaye tutaiacha iendele na politics zake na kuwapa nafasi wengine kuanza parties zinazoweza kufanya politics na siyo kulinda mafia interests; wakati huo wengine tutaendelea na profession zetu na kujitenga mbali na siasa kwani siasa siyo sehemu yetu. This is a war where we dont care what can be used to deafeat the enemy! I ask you to join us in this fight; the fight for our true identity as a country. Its a holly fight which the reward is not from man but from Him we all belong to. Is a fight for the help of the poor and needy who are taken captive at their own will by the people they trusted can defend them and their interests. Few can die and few can loose some of their parts but majority including our descendants, shall win and rejoice forever.

If God is with us who can be against us? If God say Yes who can say no? A thousands shall fall by our sides and ten thousands by our right hands. I am a risine to shine, the light which is in me nobody can put it off for its a greater light and have decided to live on the day time of my country's life. I leave the darkness to whoever feel comfortable to stay with it but for me no time to waste and for this case it does not mater whether CHADEMA or whatever available to be used to reflect the light I am giving out to make others see we are heading in the wrong direction and soon will fall into a ditch.
 
Hali sasa hivi inatisha sana na CDM wanapaswa kununua kiona mbali, maana CCM imeshindwa Siasa na kuacha siasa kabisa sasa sijui nini kinakuja katika nchni yetu, nimejaribu kufuatilia siasa za nchni nyingi sijawai kuona nchni ambayo chama tawala imeregea na kukaa pembeni kabisa kama haipo kiasi hichi!

Sasa hivi wameachia CUF, UDP, na baadhi ya asasi kwa pamoja ndio wanaoongea badala ya CCM, nadhani CCM labda haipo ingawa sisi tunadhani ipo. Maana ukiangalia hata hao wanajitokeza kuisemea CCM mi nadhani wanafanya kama njia ya kujipendekeza iliwavute kitu kwa Mkuu wa Dola lakini sidhani kama ni CCM inawatuma! mtu aliyeopo ICO haongei sidhani kama anaweza kutuma.
 
SOMA JAHAZI JPILI,katika Gazeti la Tzn Daima YA LEO.
By P Karugendo
CCM WANAPOJIFUNGA GOLI LAWAMA ZIMWENDEE NANI.?

CCM wanapojifunga goli lawama zimwendee nani?
ban.blank.jpg

Prudence Karugendo

amka2.gif

JUMA lililopita nilionyesha jinsi kanuni mojawapo, katika mpira wa miguu, inavyoweza kutumika vilevile kwenye ushindani wa kisiasa na kuleta manufaa yale yale yanayokuwa yamelengwa na kanuni hiyo katika mchezo wa mpira wa miguu.
Kanuni hiyo ni ya mtego wa kuotea "off side trick" ambayo chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema, kimejinufaisha nayo kinapoitumia dhidi ya chama tawala, CCM.

Katika makala hiyo nilikuwa nimejaribu kuangalia mashambulizi ya chama tawala dhidi ya upinzani, hasa yanayoelekezwa kwa chama kinachoonekana kuwa ni tishio zaidi kwa sasa katika mustakabali wa CCM, Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Kwa jinsi mashambulizi hayo yanavyofanyika kwa papara na bila mpangilio maalumu, kutokana na sababu nitakazozieleza baadaye kwenye makala hii, na hivyo CCM kushindwa kuelewa au kuzisoma mbinu za mpinzani wake.

Papara hizo ndizo zinazokifanya chama hicho kikongwe kuingizwa kirahisi kwenye mtego wa kuotea, kwa maana ya chama hicho kujikuta kikifanyishwa kazi ya kukijenga na kukipamba chama pinzani kwa imani kuwa kinaubomoa upinzani.
Kufuatia makala hiyo baadhi ya wasomaji wameniomba niangalie pia na upande wa ngome ya CCM ili kuleta uwiano wa mfumo wa timu.

Kwahiyo katika makala hii nataka niangalie jinsi CCM ilivyoiweka ngome yake dhidi ya mashambulizi ya upinzani hasa yale makombora yanayofyatuliwa na washambuliaji wa Chadema.

Je, CCM imefanikiwa kuiimarisha ngome yake dhidi ya mashambulizi hayo? Baada ya kuwaona washambuliaji wake kuwa hawauelewi mtego wa kuotea, je, ngome ya CCM imekaa sawa kuyadhibiti mashambulizi ya Chadema?
Ngome hiyo ya CCM inazo mbinu kama walizo nazo walinzi wa Chadema za kutumia nguvu kidogo kuzuia mashambulizi yenye nguvu za ziada lakini yasiyo na mpangilio maalumu?

Ngome ya CCM ikitazamwa si tu kwamba inaonekana inapwaya bali pia iliyo tayari kujifunga mabao yenyewe baada ya kutiwa msukosuko kidogo tu na washambuliaji wa upinzani.
Mara kadhaa tumeishuhudia CCM ikijifunga mabao yenyewe na kushindwa kuyarudisha kutokana na kukosa safu iliyo imara ya ushambuliaji.

Mwaka 1995 CCM walijifunga bao wenyewe, bao ambalo bado wanalijutia mpaka leo, pale walipolipoteza kiuzembe jimbo la Karatu. Bila mizengwe ya CCM si ajabu jimbo lile lingekuwa bado ni mali yake mpaka leo, kama chama hicho kingekuwa kinayasikiliza na kuyaheshimu matakwa ya wanachama wake.

Ikumbukwe wana CCM wa jimbo la Karatu walikuwa na chaguo lao, mtu waliyemtaka awe mgombea wa jimbo hilo katika nafasi ya ubunge kwa tiketi ya chama chao, naye si mwingine bali Dk. Willbrod Slaa.
Lakini chama chao, kwa mtindo wake maarufu wa huyu si mwenzetu, kikaamua kuyapuuza matakwa ya wanachama wake katika jimbo lile. Kikamwengua Dk. Slaa ambaye wanachama wachache wa chama hicho katika ngazi ya kitaifa walimuona kuwa si mwenzao.

Pamoja na ukweli kwamba alikuwa mwanachama hai na zaidi ya hapo kipenzi cha wanachama ngazi ya jimbo. Badala yake CCM ikamuweka mtu (to impose) aliyekuwa hakubaliki jimboni, Patrick Qorro.
Wana CCM wa Karatu kuona vile, wenyewe, wakamuonyesha Slaa njia ya kutokea na mahali pa kuelekea, ndipo Dk. Slaa akatua Chadema. CCM ikawa imejifunga goli yenyewe na kuipa Chadema ushindi bila jasho. Tangu wakati huo CCM wanapigana kufa na kupona kulirudisha jimbo lile bila mafanikio.

Ni wazi kwamba CCM wameishatumia gharama kubwa sana katika jitihada za kulirudisha jimbo lile kwenye ngome yake. Na sidhani kama gharama inayotumika kuusafisha uzembe uliofanywa na ngome ya chama hicho inatokana na michango pekee ya wanachama wake.

Nina imani kwamba gharama zinazosababishwa na uzembe wa ngome ya CCM, inayojifunga magoli badala ya kuyazuia, zinatugusa Watanzania wote walio ndani ya CCM na walio nje yake. Sote ni waathirika wa uzembe wa ngome ya chama tawala.
Pesa ambayo ingetumika kufanyia mambo ya maana kwa ajili ya ustawi wa wananchi inabidi itumike kuusaka kwa mabavu ushindi wa chama tawala baada ya chama hicho kuwaweka kwa mizengwe kwenye ushindani baadhi ya wanachama wake wasio na uwezo wa kushindana.

Ni kwa nini chama hicho kinachukua maamuzi hayo yanayogeuka mzigo kwa wanachama na wasiokuwa wanachama? Hilo ni swali ambalo sina hakika kama kuna kada yeyote wa chama hicho aliye tayari kulitolea maelezo ya kina.
Ipo mifano zaidi ya jinsi ngome ya CCM inavyojifunga magoli yenyewe kwa faida ya wapinzani wake. Mkoani Shinyanga, katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Jimbo la Maswa Magharibi lililazimishwa kwenda Chadema kwa mtindo uleule wa CCM kujifunga goli yenyewe.

Kwingine ni Kawe, Iringa Mjini, Nyamagana, Ilemela na kwingineko. Pia yapo majimbo mengine ambayo CCM imeyatetea kwa kutumia mtutu wa bunduki baada ya kila njia kuwa imeshindikana.
Anayelitilia shaka hilo awaulize wapiga kura wa Jimbo la Karagwe, mkoani Kagera, njia iliyotumika kumtangaza mgombea wa CCM kuwa ndiye mshindi.

Pia awaulize wapiga kura wa Jimbo la Segerea namna alivyopatikana mshindi wa kiti cha ubunge wa jimbo hilo kitu ambacho mpaka sasa bado kimewaacha midomo wazi.

Hizo zote ni gharama ambazo chama tawala kinalazimika kuziingia ili kujiepushia aibu inayosababishwa na udhaifu wa ngome yake inayolazimishwa na wapinzani kujifunga magoli badala ya kuyazuia.

Timu yoyote inayokuwa na ngome yenye wachezaji wanaojifunga magoli badala ya kuyazuia magoli yasiingie upande wake ni wazi kwamba inakuwa na kasoro katika muundo wake.

Inawezekana kwamba wachezaji ambao wangepaswa kuwekwa kwenye nafasi za ushambuliaji ili wakafunge magoli na kuipatia timu ushindi ndio wanaowekwa nyuma kwenye nafasi za ulinzi wakati walio na uwezo wa ulinzi wakiwekwa mbele ili wakashambulie.

Matokeo yake wale walio mbele wanaishia kuotea kwenye "off side trick" wakati walinzi wake wakipachika mabao kwenye goli lao. Hivyo ndivyo CCM ilivyo kwa wakati huu. Sijui ni nani anayepaswa kubeba lawama za muonekano huo wa timu iliyojichanganya kimfumo namna hiyo?

Na kwa vile hiki ni chama tawala tusije tukajidanganya kwamba kasoro hizo za kichama zitaishia tu katika chama. Ni lazima kasoro hizo zijitokeze katika ngazi ya utawala wa nchi.
Ni lazima nchi nayo ionekane pia inajifunga magoli wakati safu yake ya ushambuliaji ikiwa butu. Mifano tunayo mingi inayolishadidia jambo hilo bila pingamizi.

Tuangalie mikataba tunayoingia na watu wanaoitwa wawekezaji. Wengi wa watu hao wanakuja kuzoa tu rasilimali za nchi yetu wakiwa hawajawekeza lolote.
Tujiulize, mtu anayekuja kuzoa tu madini yetu na kupeleka kwao anakuwa amewekeza nini? Ardhi yetu, madini yetu, watumishi wetu, na wakati mwingine mitaji tunawapa sisi, lakini wao eti ni wawekezaji, wanaondoka na kila kitu na kutuachia makorongo yaliyojaa vumbi!

Wawekezaji wengine kama IPTL, Richmond, Dowans na wengine wa aina hiyo wanakuja kutuuzia huduma wakiwa wametusainisha mikataba sawa na ile ya kina Karl Peters, mikataba ya kwamba hata kama huduma zao hatuzihitaji ni lazima tuzinunue, tukazifanyie nini? Hilo sio tatizo lao kujua, wao wanachokitaka ni pesa yetu basi.
Kwa kukubali kuingia katika mikataba ya aina hiyo ni nani atabisha kwamba hatujifungi mabao sisi wenyewe kwa faida ya hao wageni ambao kwa hapa naweza kuwaita wakora?

Tatizo linaloanzia kwenye mfumo wa chama tawala linageuka kuwa tatizo la nchi. Nchi inalazimika kuugua ugonjwa unaokisumbua chama tawala.
Lakini tatizo hilo linaanzia wapi? Au niulize tatizo hilo ni lini na kwa nini limekipata chama tawala?
Wakati nchi yetu ikiendeshwa kimaadili, miaka ya nyuma kidogo, siasa nayo ilikuwa ni taaluma inayojitegemea. Ilikuwa si rahisi kama ilivyo sasa kwa kila mtu kuivamia siasa.

Si kila mfanyabiashara, kwa mfano, angeamua kuingia kwenye siasa jinsi anavyotaka yeye. Hata wanazuoni si wote walikuwa wanajiona wanaiweza siasa. Kwa maana hiyo maprofesa walibaki vyuoni kufundisha.
Madaktari nao walibaki mahospitalini kuwatibu wananchi, wafanya biashara walibaki kwenye biashara zao nakadhalika. Siasa ilibaki kwa wanasiasa.

Walioitamani siasa, hata kama walikuwa wanazuoni, iliwabidi waende shule kwanza. Vilikuwepo vyuo vya siasa, mfano kile cha Kigamboni. Tena wakati huo chama cha siasa kikiwa kimoja tu lakini kikiwa na itikadi ambayo ilikuwa lazima mtu aisomee kwanza ndipo aweze kujitambulisha kama mwanasiasa.

Tuseme kilikuwepo kitu ambacho ilimbidi mtu kukisomea na kukielewa vizuri kabla ya kujitambulisha kama mwanasiasa.
Lakini baada ya utaratibu huo kuondolewa katika mpango wa soko huria ndipo siasa ikabaki haina mwenyewe. Kila mmoja akajiona anaiweza siasa. Hiyo ikawa fursa ya wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo kuwekeza kwenye siasa baada ya kuona kuwa inalipa.

Matokeo yake ndiyo haya, tuna watu wanaofanya siasa wakiwa si wanasiasa kwa vile chama tawala kimeiondoa siasa katika taaluma na kuifanya ni shughuli inayoweza kufanywa na kila mtu.
Ni kwa maana hiyo chama tawala kimewawezesha hata wacheza tunguli kuingia bungeni wakiwa tayari ni wanasiasa.
Kwa vyovyote vile hawa hawawezi kukisaidia chama hicho kisiasa, kwa vile kiuhakika hawa siyo wanasiasa, bora tuwaite wawekezaji tu waliogundua kuwa siasa inalipa na kuamua kujibana mle kwa vile ni mfumo wa soko huria.
Hilo linaweza likatuonyesha ni jnsi gani Chama Cha Mapinduzi kinavyoelemewa na mzigo kiliojitwisha bila kuelewa kinaupeleka wapi.

Chama cha siasa kinaposheheni wawekezaji wakijiita wanasiasa tujue kuwa huo ni mzigo mkubwa kwa chama na inapotokea chama hicho kikawa chama tawala basi huo ni mzigo wa nchi. Na ieleweke kwamba ni vigumu kuwapambanisha wawekezaji hao katika siasa na wanasiasa machachari waliodhamiria kufanya siasa.
Tofauti na CCM ambamo kwa sasa watu wanaingia kama wawekezaji, chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema, kina wanasiasa waliodhamiria kufanya siasa.

Hawa wamelazimika kuingia kwenye siasa baada ya kuiona siasa ya nchi yao ikienda mrama, wamelenga kuinusuru nchi yao kisiasa. Siwezi kuwaita hawa kuwa nao ni wawekezaji, hapana, hiyo ni kwa sababu Chadema bado ni kama pori, waliomo wameingia ili wakalime. Ni tofauti na CCM ambalo ni shamba linalotoa mavuno, kwahiyo wanaoingia mle wanakuwa wamevutiwa na matunda na si kitu kingine. Kwa jinsi hali ilivyo ni kwamba CCM wanajifunga mabao wenyewe kutokana na chama hicho kuwachezesha watu wasioelewa mbinu za mchezo. Kwahiyo kwa tatizo hilo hawapaswi kumtafuta mchawi nje ya kikosi chao.
 
congratulats kipimapembe. umezungumza jambo la msingi sana.ni uchambuzi uliojaa realities. good and thanks!
 
Back
Top Bottom