Kipindi kile cha 2015 Mkewe alisema wanategemea kurejea nchini Tanzania kuja kuanzisha taasisi kubwa sana ya shule za kisasa za kimataifa ili Dr.Slaa awe mkurugenzi. Sasa sijui hilo wazo limeyeyukia wapi?
Maana hilo wazo lingemfaa zaidi Dr.Slaa kuliko hilo la kuuza duka.
Kiasili Dr.Slaa ni Mwanasiasa, Mwanathiologia na Msomi wa falsafa, uwanja wake wa kazi ulipaswa uwe Siasa, Dini au Elimu.
Sasa biashara ya kuuza duka ni kumtesa kisaikologia na kumshosha kimwili na kiakili. Kitaalamu sio sahihi kabisa kwa mtu mwenye umri wa Dr.Slaa(Zaidi ya Miaka 60) kudandia ajira ambazo hakuwahi kujifunza au kuzifanya akiwa kijana.