pappilon
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 3,192
- 3,565
Mkuu kama kuna mtaalamu wa katiba atusaidie, asiegemee upande wowote.
cc Paschal Mayala
Siku hizi anatumika
Mkuu kama kuna mtaalamu wa katiba atusaidie, asiegemee upande wowote.
cc Paschal Mayala
Still unaongea pumba sasa katiba si ilipigiwa kelele na TMK ikafanya kazi yake na watanzania wakaappreciate sasa nani kma sio lichama lenu hilo waliochakachua hyo katiba ??? Unalaumu wanamageuzi wakati nyie ndo mlivuruga mchakato mzima na huyo kibaraka wenu marehem sitta........ na katiba mpya si tumetaka mwaka jana pia huyo mwenyekiti wenu alijibu nni zaidi ya kusema ananyoosha nchi kwanni usimfate mkamshauri instead of kulaumu wapinznai wakati wanaoharibu ni magamba wenzio..... we jamaa ur insaneAnaapa kuilinda halafu anailind sio? Vp uwezo wake wa kikatiba wa kuchezea katiba nao una ufahamu? Au unafikiri katiba inamfunga rais, kwa taarifa yako ukitaka madaraka ya rais katika katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania utakuta nchi hii kumbe inaendeshwa na rais tu na inampa madaraka ya kufanya ayatakayo. Tuliza kichwa, nyie mliokimbilia mambo kabla katiba haijabadilishwa ndio dawa yenu hiyo, tuliwaambiwa toka mwanzoni mwa miaka ya tisini kisifanyike chochote mpaka katiba ibadilishwe, uroho wenu na tama zenu za sifa mkasaliti watanzania leo mnajifanyakupiga kelele huku akina Leo lekanwa wakionekana wapuuzi. Unamkumbuka yulee mtu alisigina katiba pale Jangwani? Au ulikuwa hujazaliwa. Magu pikia hao maharage, watie gesi waendelee kupumua hewa chafu maana walikuwa na hamu ya kushiba maharage hay na wayale sasa
Unisaidie mmi?? Mtu mwenyewe mwepesi kichwani hivi hta swali dogo tu kuhusu katiba tukabishana wiki nzima hujibu hoja kazi kujadili ndoa ya mbowe nilikudharau sana toka kipindi kile sikutaka hta kuquote leo sema UNABOA sana i found myself replyin.... anyway acha niendelee kifungwa akili na minyororo huku nyie mnaofkiri tofuati muendelee kuaminshwa dunia "inavyoendeshwa".... yaani jitu zima kma wwe unaamini hizo conspirancy?? shame on u and i still pity ur kids
Still unaongea pumba sasa katiba si ilipigiwa kelele na TMK ikafanya kazi yake na watanzania wakaappreciate sasa nani kma sio lichama lenu hilo waliochakachua hyo katiba ??? Unalaumu wanamageuzi wakati nyie ndo mlivuruga mchakato mzima na huyo kibaraka wenu marehem sitta........ na katiba mpya si tumetaka mwaka jana pia huyo mwenyekiti wenu alijibu nni zaidi ya kusema ananyoosha nchi kwanni usimfate mkamshauri instead of kulaumu wapinznai wakati wanaoharibu ni magamba wenzio..... we jamaa ur insane
kijo bisimba bure tu hana lolote kazi yake kama fisi kusubiri mkono wa binadamu udondoke. kitu kidogo wote wanatoa mimacho wakati hakijakosewa kitu. wanatafuta kila kaujiko kuirushia maneno ya ovyo serikali ya jpmAsema atakuwa na uroho kiasi gani kung'ang'ania ubunge.
Awasilisha barua ya kuachia ngazi kwa mamlaka husika.
Chanzo: Mtanzania
Swali:
Kikatiba, Mbunge wa kuteuliwa na Rais akijiuzulu au kukoma kuwa mbunge kwasababu nyingine yoyote ile inayotambulika Kikatiba,idadi ya wabunge waliokwisha teuliwa na Rais inapungua au inabaki pale pale?
=====
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, Dk. Abdallah Possi, amesema tayari amemwandikia barua ya kujiuzulu ubunge Spika wa Bunge, Job Ndugai, kutokana na hatua ya Rais Dk. John Magufuli kumteua kuwa Balozi.
Dk. Possi ambaye alikuwa miongoni mwa wateule wa ubunge wa Rais John Magufuli, uamuzi wake huo ni wazi unavunja mjadala dhidi ya Mkuu huyo wa nchi aliyekuwa akikabiliwa na madai ya kwenda kinyume na Katiba kutokana na uteuzi wake wa wabunge wengine wawili alioufanya wiki hii kuonekana kushindwa kukidhi matakwa ya Katiba katika suala la jinsia.
Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi jana, Dk. Possi ambaye alikuwa mteule wa mwanzo katika Serikali ya Rais Magufuli kabla ya juzi kutangaza kumteua kuwa balozi alisema baada ya taarifa hiyo ya Rais jana alimwandikia barua ya kujiuzulu ubunge Spika wa Bunge.
Mahojiano kati ya gazeti hili na Dk. Possi ambaye kwa sasa anasubiri kupangiwa kituo kipya cha kazi yalikuwa kama ifuatavyo:-
Swali: Dk. Possi hongera sana, umejisikiaje Mheshimwa Rais kukuteua kuwa balozi?
Dk. Possi: Ni kazi nyingine mpya, majukumu tofauti ni challenge (changamoto) nyingine kwa sababu nakwenda kuwa mwakilishi katika nchi nyingine.
Kwa hiyo ni kuichukua hiyo changamoto kwa jinsi inavyokuja kwa manufaa ya Taifa.
Swali: Sasa kwa uteuzi huo wa ubalozi utakuwa tayari kujiuzulu ubunge?
Dk. Possi: Hilo swali nimeulizwa na watu wengi kweli na mimi nikasema hebu ngoja niwape challenge, hivi kweli mnadhani nitakuwa ni mroho kiasi gani, mnajua niko nje halafu mseme sijiuzulu ubunge wakati siwezi kupractize eeeh! Umenielewa?
Swali: Kwa hiyo utajiuzulu?
Dk. Possi: Of course definitely (hakika) kwa sababu haiwezekani uko mbali unawezaje ku- practise ni jibu ambalo liko wazi hata sijui kwanini limekuwa mjadala mkubwa hivyo.
Swali: Kwa hiyo umeandika barua ya kujiuzulu?
Dk. Possi: Yeah nimeshaandika.
Swali: Umeandika lini Dk?
Dk. Possi: Si leo kwa sababu siwezi kuandika kabla ya taarifa
Swali: Umeandika kwa Rais au kwa Spika wa Bunge?
Dk. Possi: Ubunge ni kwa spika kwa hiyo unamwambia spika nimejiuzulu the less ni procedure (zilizobaki ni taratibu) zingine, the fact is (ukweli ni) ni kwamba huwezi kuendelea kuwa balozi and the same time (na wakati huo huo) ni mbunge sasa ni kwa staili ipi hiyo ni wing tu ya kufikia huko na sidhani kama ni big issue (suala kubwa).
Kujiuzulu huko kwa Dk. Possi katika nafasi ya ubunge ni wazi sasa kunampa nafasi Rais Magufuli kukamilisha takwa la Katiba kupitia kifungu Na 66 1(e) kinachompa mamlaka ya kuteua wabunge 10 na kati ya hao angalau watano wawe ni wanawake.
Kabla Dk. Possi kuteuliwa kuwa Balozi na uteuzi wa wabunge wawili ambao ni Profesa Paramagamba Kabudi na Abdallah Bulembo ambao Rais Magufuli aliufanya mapema wiki hii na hivyo kufanya jumla ya wateule wake hao kutimia wanane kati ya 10, kulikuwa na maoni tofauti wengine wakiwa na mtazamo kuwa tayari idadi ya wanaume ilikuwa ikizidi ile ya wanawake na hivyo kwenda kinyume na Katiba.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, alikaririwa na gazeti la MTANZANIA jana akisema Rais Magufuli alikuwa hajavunja sheria.
Dk. Mwakyembe ambaye ni Mwalimu wa Sheria na ambaye alikuwa akizungumza kabla ya uteuzi huu mpya wa Dk. Possi, alisema wanaosema Rais kavunja Katiba wangesubiri amalize nafasi 10 za uteuzi ndiyo waseme.
Wakili kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Judith Kapinga, akinukuu kifungu cha Katiba cha 66 alisema Rais alikwenda kinyume na matakwa hayo.
Dk. Milton Mahanga, aliyewahi kuwa Naibu Waziri katika Serikali ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, ndiye aliyekuwa wa kwanza kuibua mjadala huo.
Katika andiko lake ambalo lilikuwa likisambaa kwenye mitandao ya kijamii siku moja baada ya Rais Magufuli kufanya uteuzi wa wabunge hao wawili, Dk. Mahanga alisema uteuzi huo ulikuwa umevunja Katiba kwa sababu kati ya wabunge wanane waliokuwa tayari wameteuliwa wanaume walikuwa sita na kwa maoni yake alisema walipaswa kuwa watano na wanawake angalau watano.
Ibara ya 66 (1) inayoeleza aina ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sehemu ya (e) inasema; “wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za ibara ya 67 na angalau wabunge watano kati yao wakiwa wanawake.”
Mbali na Dk. Possi na kabla ya uteuzi wa Profesa Kabudi na Bulembo, waliokuwa wameteuliwa na Rais kuwa wabunge ni pamoja na Dk. Phillip Mpango, Balozi Dk. Agustine Mahiga huku wanawake wakiwa ni Profesa Joyce Ndalichako na Dk. Tulia Ackson.
LHRC YATOA TAMKO
Ni katika mjadala huo huo, jana Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), kililazimika kutoa taarifa kwa umma kuhusu uteuzi huo wa wabunge zaidi kikienda mbali na kuzungumzia nafasi nyingine.
Katika taarifa hiyo ambayo ilisainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Hellen Kijo Bisimba, LHRC ilieleza kuwa imetathmini mwenendo wa masuala ya kijinsia katika teuzi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika nafasi mbalimbali za uongozi nchini Tanzania.
“Katika tathmini yetu tumejikita zaidi kuangalia katika muktadha wa haki za binadamu na haki za wanawake kwa kuzingatia mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda ambayo Tanzania imeridhia kuhusu usawa wa kijinsia vile vile kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na pia sheria nyinginezo.”
Ilieleza kuwa kikanda, Tanzania ni nchi mwanachama wa Umoja wa nchi za Kusini mwa Afrika na hivyo imeridhia mkataba wa Jinsia na Maendeleo wa nchi za Kusini mwa Afrika yaani SADC Gender Protocol ambapo mkataba huu katika Ibara ya 12 inazitaka nchi wanachama kuhakikisha kuwa katika ngazi zote za maamuzi kuna usawa wa kijinsia wa asilimia 50 kwa 50.
Pia Mkataba wa Afrika wa Haki za Wanawake (Maputo Protocol), unapinga ubaguzi dhidi ya wanawake katika ngazi za maamuzi.
“Kimataifa, Mkataba wa kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake (CEDAW) katika Ibara ya 7 inazitaka nchi wanachama wa mkataba huo kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika kutunga sera, sheria na kuwa katika ngazi za utekelezaji wa sera na sheria hizo (ngazi za maamuzi).”
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya LHRC, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 13 inaeleza jinsi ambavyo Serikali itachukua hatua za makusudi kurekebisha matatizo yaliyo katika jamii ili kuondoa ubaguzi na kwamba katika muktadha huo Katiba imetoa mwongozo katika teuzi mbalimbali, kwa mfano wabunge wateule wa Rais Ibara ya 66 (1) (e).
Mbali na hilo la wabunge wa kuteuliwa katika tathmini yao, Kituo hicho kimesema kimeangalia nyadhifa nyingine za uteuzi unaofanywa na Rais kama mawaziri na manaibu waziri, wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi wa halmashauri bado idadi ya wanawake imekuwa chini sana na hivyo kutokuzingatia ulinganifu wa kijinsia.
“Kwa mfano idadi ya mawaziri wanawake ni 4 tu kati ya 19, kati ya wakuu wa mikoa 26 wanne tu ndio wanawake, kati ya wakuu wa wilaya 134 wanawake ni 25 tu na kati ya wakurugenzi wa halmashauri na wilaya 185 wanawake ni 33 tu.”
Kutokana na hali hiyo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimeitaka Serikali na mamlaka nyingine za uteuzi kuzingatia mambo makuu manne.
Kwanza, Sheria na Katiba katika teuzi mbalimbali katika nafasi za uongozi.
Pili, kufuata misingi ya haki za kijinsia kwa mujibu wa mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo Serikali imesaini na kuridhia.
Tatu, kuzingatia usawa wa kijinsia na kuchukua hatua za makusudi (affirmative action) ili kuwa na jamii yenye haki na usawa katika suala la uongozi wa nchi.
Nne, Rais aone uwezekano wakurekebisha hii hali iliyojitokeza ya kukiuka maelekezo ya Katiba.
Chanzo: Mtanzania
HaaHahahaa imebidi nicheke tu ndo ya mbowe inanihusu nni?? Huyo magu wenu ameishi na kimada miaka mingapi unajua mbona sijaileta hyo mada hapa?? Hoja yanhu siku ile ilikuwa kuhusu SHERIA YA VYAMA pia katiba kwenye ibara ya 18 uhuru wa maoni..... sasa mkuu ukaacha kujadili hoja yangu ukaanza kutukana mbowe na ndoa yake sijui biashara sasa mie mpinzani wa kawaida tu nisie na uongozi wowote kwenye chama chochote unaacha kujibu hoja yangu unahamia kwa mbowe mie nikueleweje??? Sawa mbowe kapewa hela na kinana mie nimepewa?? Kma sijapewa bado na ninadai sheeia ifuatwe ili niwe huru kwenye majukwaa ya siasa na mimi unanijibu nini?? Kwanni kila hoja yangu unamuinhiza mbowe sijui seif as if mimi ni mfuasi wa mtu??Oh, pole kumbe ndoa ya Mbowe inakuuma mpaka leo, pole sana, kumbe hukujua eeh, ndio hivyo bwana, conspiracy theories ni ujinga na watu vichwa vitupu kama mimi ndio huamini ndio maana sisi tuliokuwa tunasema kuwa USA wanapigana na Urusi Syria tulikuwa tunaota tu, na hata Donald Trump alipomwambia Obama kuwa ameshatandikwa na Urusi kule Syria nae alikuwa ni muota ndoto tu, ila nyie wafuasi wa uongo ndio mnaojua. Pole tena sana kuhusu ndoa ya Mbowe, sikudhamiria kukuumiza, imetokea tu bahati mbaya, usinichuie, usiniwekee kinyongo bado nakuhitaji sana katika mijadala, mawazo yako ni muhimu sana kwangu, naweza nisiwe nakubali hadharani lakini kuna mawili matatu najifunza kutoka kwako. Sisi kama taifa na wazalendo ni budi kukubaliana kujadiliana na hata kukubali kutofautiana na kupingana pasipo kupigana. Pole sana ndugu yangu, I am genuinely sorry!
Ungeanza na Mbowe kwanza anayejitayarisha kuingia ikulu 2020,ingekuwa umefanya la maana sana.Kumkaripia Magufuli na kumuacha Mbowe,maana yake ni kuwa tutaendelea na haya haya hata kama ccm ikiondokaDaaaah kama Rais kwenye mambo sensitive kama haya anakosea .......
Sasa kwenye mambo madogo madogo si ndio kabisa jamaa ana waburuza..........
Kiukweli ni hatari kuwa na Rais asiyefuata katiba................
Naomba Mungu Kuingilia kati miujiza Yake iongoze hii nchi......
Ok mkuu nikuulize kitu unakubaliana na majibu ya rais kuhusu mchakato wa katiba??Hhahahahahah, tumetofautiana kitu kimoja, muda wa kuidai katiba, kuna tulioidai siku nyingi sana lakini tukavurugwa na wapinzani waliotaka ruzuku ya vyama wakati ule.Ile ndio ilikuwa fimbo tuliyopigiwa kiasi kwamba hawa ninyi mnawaona wapinzani sasa kwangu ni vibaraka na ndio maana nasisitiza sana mjitahidi mdadisi na muwafahamu vyema. Maisha yao, elimu zao na kazi zao walizowahi kufanya na hata uhusiano wa nasaba zao na utawala. Mapenzi yasiwapofushe macho. Mwenyekiti wa upinzani anapewaje pesa na Kinana? Mwenyekiti wa upinzani anapewaje pesa na Mbunge wa CCM? Kilichotokea hapa na kinachoendelea sasa wapinzania wa kweli wanachekelea na kushangilia ccm ikiwadhibiti vibaraka wao kama ambavyo wao vibaraka walivyotumika kutudhibiti sisi. Ukiniita ccm sijali kwa kuwa nafahamu ninyi nakifanya, kwa sasa nahangaika na kutangaza kweli, ikikuuma nisamehe lakini sintosita na sintoacha kutumia kipawa chaangu kukuelimisha wewe na kukupa habari wewe na wengine, kama mimi, inawezekana muda mwingine tusikubaliane humu jf lakini tukibaki peke yetu na nafsi zetu kila mmoja wetu anaona uzito wa hoja ya mwenzake. Alamsiki.
Mkuu acha mawazo ya conspirancy theory mie nshasoma vitabu na vitabu na kikubwa zaidi kinaitwa NEW WORLD ORDER cha ROY LIVESEY.. hiko ndio kikanifanya niamini kuwa everythin is planned hapa duniani BUT nkagundua watu wakiamua kukipinga hakitokei kuna nchi ambazo hta free masons sijui iluminati be it malctara hawajaweza kupenya je hizo nchi waliwezeje?? China cjui iran hii ya baada ya mapinduzi na north korea wangeamini hivyo wangekuwa hapo walipo leo??Oh, pole kumbe ndoa ya Mbowe inakuuma mpaka leo, pole sana, kumbe hukujua eeh, ndio hivyo bwana, conspiracy theories ni ujinga na watu vichwa vitupu kama mimi ndio huamini ndio maana sisi tuliokuwa tunasema kuwa USA wanapigana na Urusi Syria tulikuwa tunaota tu, na hata Donald Trump alipomwambia Obama kuwa ameshatandikwa na Urusi kule Syria nae alikuwa ni muota ndoto tu, ila nyie wafuasi wa uongo ndio mnaojua. Pole tena sana kuhusu ndoa ya Mbowe, sikudhamiria kukuumiza, imetokea tu bahati mbaya, usinichuie, usiniwekee kinyongo bado nakuhitaji sana katika mijadala, mawazo yako ni muhimu sana kwangu, naweza nisiwe nakubali hadharani lakini kuna mawili matatu najifunza kutoka kwako. Sisi kama taifa na wazalendo ni budi kukubaliana kujadiliana na hata kukubali kutofautiana na kupingana pasipo kupigana. Pole sana ndugu yangu, I am genuinely sorry!
Hahahaha vyote hivyo ni wewe. ..aisee. .Bye-byeNdezi wewe waliyekuwe nyuma ya mlango kwa kujiona mzalendo katuni,nna elimu yangu ambayo inanifanya niishe nitakavyo ujinga wenu wa buku 7 na ufipa peleka kwenye Nyashimo msengerema wewe
Mbowe kavunja kifungu gani cha katiba ya nci au chama??Ungeanza na Mbowe kwanza anayejitayarisha kuingia ikulu 2020,ingekuwa umefanya la maana sana.Kumkaripia Magufuli na kumuacha Mbowe,maana yake ni kuwa tutaendelea na haya haya hata kama ccm ikiondoka
Mbowe kasigina katiba ya chama chake kwa kumfuta Sosopi dakika tano kabla ya uchaguzi na kumuweka KIbaraka wake Mchungaji Msigwa.Hii haipo kwenye katiba yenu,mambo haya yakiendelea mkichukua dola itakuwa hatari sanaMbowe kavunja kifungu gani cha katiba ya nci au chama??
Hapa tunaongelea mambo ya RAIS KUKIUKA KATIBA YA NCHI mbowe anaingiaje hapa??
Jikite kwenye hoja sio majungu maana sio kila anemkosoa magufuli ni chadema au cuf kumbuka id fake humu ndio zinatumika
Weka hapa kifungu kilichovunjwa kma ambavyo tuliweka hapa kifungu alichovunja magufuli kwa tafsiri ya kiingereza..... nasubiriMbowe kasigina katiba ya chama chake kwa kumfuta Sosopi dakika tano kabla ya uchaguzi na kumuweka KIbaraka wake Mchungaji Msigwa.Hii haipo kwenye katiba yenu,mambo haya yakiendelea mkichukua dola itakuwa hatari sana
Ikulu ni mzigo mzito mno , push up hazisaidii .Tumezoea kupiga makofi acha tuendelee kupiga makofi.Viwanda vipo vingi tu hata waliokuwa na kazi wamepungua sana.Mafisadi kesi zao zinaendelea kwa kasi ya ajabu na wameanza kufungwa vifungo vikali kabisa tumemuona yule Mbunge wa CDM akifungwa,mwenyekiti wa CDM huko Lindi na yule Diwani wa CDM huko Tarime hakika Mahakama ya Mafisadi inafanya kazi sana.Hongera sana Magufuli.
Ok mkuu nikuulize kitu unakubaliana na majibu ya rais kuhusu mchakato wa katiba??