Dr,
Hivi huwezi kuishi maisha ya kawaida kwa kutegemea mshahara wa ubunge na kutoa mihadhara katika vyuo vikuu?. Nashauri uache kazi ya Unaibu uwaziri ukipinga kuitumikia serikali ambayo ilishindwa kuyafanyia kazi malalamiko yako ya kutishiwa maisha yako. Kama huwezi kuujali uhai wako, hakuna mwingine anayeweza kuujali zaidi yako. Fedha hazina mwisho lakini uhai una mwisho. Ni heri kuishi ukiwa maskini na amani kuliko kuishi kama mfalme ukizingirwa na hofu ya kutolewa uhai wako
Kazi ya shetani ni moja kuharibu na kuua, haijalishi shetani aje akuchekee na kukufadhili na kuwa mwema kwako, lakini lengo lake la mwisho ni uharibifu tu. Huu n i mtihani wako wa pili, watu walikushauri ukatae kazi ya uwaziri lakini ulikubali, matokeo yake umeyaona. Mbona majaribio ya kukuua yalikuwa ni mengi sana kuanzia yule bibi (Kabhele) mchawi wa kutoka Malawi, ajali ya mlima nyoka, ajali ya Iringa, Alshaabab n.k. Mbona yote yalishindwa?. Unajua kwanini? ulikuwa umesimama kwenye haki
Safari hii yalielekea kufaulu kwasababu wewe mwenyewe uliamua kujiunga na kundi la waovu, japo wewe ni mjuaji sana lakini umeshindwa kujua siri kubwa iliyopo, ambayo sisi watazamaji tunaona wazi kabisa kuwa unaibu uwaziri umekuwa lango la kuingiza adui ndani mwako.
Ushauri wangu kwako jitoe haraka sana serikalini. Sifa moja kubwa ya mwanasheria wa kweli ni kusema ukweli.....................hebu tupe mtazamo wako kuhusiana na hayo yote yanayokutokea. Naomba uwe wazi hata kama ni hisia sema kuwa japo sina uhakika nahisi ni moja, mbili, tatu n.k.
Mungu amekuepusha na kifo ili uje uweke record sawa. Pia yale uliyoyoacha kwenye Ripoti wkati ule sio mbaya kama utayagusia. Hakuna siri tena, mbona EL juzi kwenye NEC kagusia ripoti ya siri ya uchaguzi kuhusu JK wakati ule. Hutakuwa wa kwanza kutoa siri kwa manufaa ya nchi, mwenyewe, familia yako na vizazi vijavyo hasa kwasababu siri hio ndio inataka kukuondoa mapema hapa duniani.