Dk Mwakyembe arejea nchini

Karibu sana braza mwakyembe, najua uliumia kiafya ila kwa sasa utakuwa umepata nafuu kubwa tu, mungu muumba ashukuliwe sana kwa maendeleo ya kiafya alokupatia, nakuomba sana braza, unakumbuka kati ukiwasilisha utafiti wako juu ya richmond mwishoni ulidai kuwa kama utayasema yote serikali yote itaanguka, naomba ayo ulobakisha uyaseme kwani watanzania bado tuna dukuduku na ayo ulobaki nayo bila kuyasema braza, we toboa tuko nyuma yako daktari ulimalize lote dukuduku letu,
 
habari hii imenibariki sana..wa kufa sio mwakiembe..kuna watu wanatakiwa kufa ili nchi hii ipige hatu ila hawafi kudadeki
 
Kwanza, namshukuru Mungu kwa kumuwezesha kiongozi wetu kurejea salama..nadhani ni suala ya kumshukuru Mungu sana,kulingana na taarifa za tatizo lake zilivyokuwa zikitufikia ilikuwa inatisha....
Lakini pili, nina ushauri wa bure kwa Dr..nadhani ni muda muafaka wa yeye kuondoka CCM na kuachana na siasa za ghiliba,ufisadi,utesaji,uuaji,unyanyasaji,visasi,uzushi,ushetani,usengenyaji,ufirahuni,uhafidhina,uchawi,unafiki nk zinazoendeshwa na chama chake cha sasa yaani CCM...Hili ni fundisho kwake na kama asiposikiliza ushauri wa watu wanaomtakia mema,itafika kipindi anataka kutoka and it will be too late....
kweli kabisa mkuu!!!!
 
Nina mtukuza Mungu aliye tukuka na Jina takatifu alilotupa sisi wanadamu kuokolewa kwalo; uhimidiwe baba wa mianga Mungu usiyeshindwa; Baba wa milele; Alfa na Omega; Jehova jire (Mungu Mponyaji); Jehova Shalom Jehova Eloim Jehova Shekenu Jehova Elshadai Mungu wa Ibrahimu Yakobo na Isaka. Ni wewe ndiwe ngome na kimbilio letu wakati wa mateso; kwak kuna amani ipitayo ufahamu wote. Acha kila mwenye mwili ajue kuwa wokovu na wewe milele na kwa jina la Yesu kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri kuwa wewe ni Bwana....

Ndugu yangu Mheshimiwa Mwakyembe kwa unyeyekevu wote nakuomba usiache kupeleka sadaka yako ya shukrani kwenye madhabahu ya Mungu mshahara wako wote na marupurupu wa mwezi huu upeleke mbele ya madhabau ya Mungu samehe wote na umwambie Mungu akulipie kisasi kwa yeyote aliyehusika sirini au waziwazi iwe ni mdudu, binadamu ama chochote haijalishi; nawe hutakaa uondoke dunia hii bila kujua chanzo cha matatizo yako ni nini!

Usidhani ni madaktari wa India na technology yao ndiyo iliyokurudishia afya yako kama utajidanganya then soon hao unaodhani wako mbali sana watarudi kwa kasi na safari hii Mungu atakupa tena nafasi ya kurudi India kuthibitisha ninalokwambia sasa. Sikutishi bali kunapokuwa na ukweli whether tunapenda kusikia ama hatupendi utabakia kuwa kweli na amina. Kwa uhakika wa haya soma Isa:30 na Isa:31 sura zote mbili utakutana na roho mtakatifu hapo naye atakufungua akili yako.

Acha niende mbele kwakutamka neno la unabii juu yako; kuna watu watajisalimisha kwako na kukwambia A to Z usije ukaacha kuwasamehe maana watakuwa wametubu kwakuwa wamehukumiwa ndani ya mioyo yao na roho mtakatifu. Watakuwa wamsaada sana kwako nao watasaidia kufunua mambo mengi na hili jambo litakuwa wazi mpaka kila mtu atashangaa...There is no way they can withstand what am now decreeing; You would be surprised!

Mungu akubariki sana hutakufa kwa mkono wa mwanadamu nawe utaishi miaka yako kamili hapa duniani maana umefanyika kuwa ishara ili jina la Mungu litukuzwe na kupitia wewe wengi watamrudia Mungu!
 
Tunamkumbusha tu kwamba asidhani ndio amepona. Akumbuke tu 'Pollinium 310' inaua taratibu. Inaweza chukua hata miaka miwili. Sisi tulimshauri asiingize kwenye serikali ya Mk*we*re akaona tunamwonea wivu! Haya hayo ndio matokeo yake!

mkuu mlikutana wapi ukampatia ushauri?
 
karibu ndugu yetu na pole ya kuumwa usisahau tu kutuambia ile siri uliyoahidi kuitoa endapo ukipona!
 
Naamin Damage imeisha fanyika katika mwili wa mwakyembe hawezi akawa 100% fit.

Hakuna damage yoyote utasubiri uone kama atakuwa na defect yoyote katika mwili wake; Mwakyembe would be a living testimony japo hata akipona kabisa wengi mtasema madaktari wa India kiboko badala ya kumwamini Mungu awezaye kukurudisha hata ukawa mtoto mdogo...Why people say Mungu anaweza huku mioyoni mwao wakiwa hawana imani na wanachokisema? Ni bora uwe wazi Mungu akusaidie kuliko kujidanganya kuamini kisicho amini moyo wako!
 
Back
Top Bottom