Jambo usilolijua ni usiku wa giza, nilifanikiwa kusoma tuhuma hizi kwenye moja ya gazeti na kwa bahati nzuri nimejaribu kufuatilia kidogo ili kujua nini hasa kinatokea katika Dayosisi ya mashariki ya Pwani. Kwa watu ambao hawaijui hii dayosisi ya mashariki na pwani sio rahisi kuelewa haya mambo, wengi watachukulia mambo haya kwa uzito usio stahili.
Kanisa lina maadui kadhaa ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisakama Kanisa . Kwa KKKT Dayosisi ya mashariki na Pwani kumekuwa na maadui wengi. Adui mmoja mkubwa ambaye ameitesa Dayosii hii ni Mambo ya Uzawa, muundo wa KKKT unasababisha kila Dayosisi iamini kuwa wanaostahili kuongoza Dayosisi ni watu wazawa wa eneo hilo, Dayosisi zote zilizopo, nyingi huongozwa na wazawa wa eneo hilo, hili ni tatizo kubwa na kwa kiasi kikubwa pamoja na mambo mengine lilivuruga sana kanisa (Dayosisi ya Mashariki na pwani) wakati wa Askofu Jerry Ngwamba, askofu Jerry Ng'wamba alikuwa ni Mzaramo wa Kisarawe ambapo aliiongoza Dayosisi hii akimpokea Askofu Sendoro ambaye alikuwa mpare. Kutokana na kuamini kuwa wazawa ndiyo wenye uhalali wa kuongoza Dayosisi husika kipindi hicho kilishuhudia ubaguzi na upendeleo ulioweza kuwabagua watu walioitwa "wakuja" jambo hili liliibua harakati za hao "wakuja" ambao ni wengi sana katika Dayosisi ya mashariki na pwani na kwa kiasi kikubwa ndiyo wanaoabudu na kuchangia maendeleo. Watu waliposhindwa kuvumilia pamoja na tuhuma nyingine za wazi zilizoundiwa tume, zilisababisha kuondolewa kwenye Utumishi wa Kanisa Askofu Jerry Ngwamba.
Ninachotaka kuchangia katika huu uzi ni kuwa Dayosisi hii imekuwa na chokochoko nyingi na silaha kubwa ambayo nafikiri imekuwa ikitumika vizuri ili kulivuruga Kanisa ni uzushi kama huu unaofanywa na watu ambao hawakufurahi uwepo wa Utumishi wa Askofu Malasusa kutokana na ukweli kuwa sio mzawa wa Pwani. Kwa wana KKKT waaminifu wanaelewa jambo hili na ndiyo maana hawahangaiki nalo sana, viongozi au wachungaji wale ambao kwa nia moja au nyingine wana maslahi nalo ndiyo wanaohangaika.
Nafikiri ifike sehemu Dayosisi isikae kimya pamoja na kuomba lakini nilazima hatua zichukuliwe ili ukweli wa jambo hili ujulikane, Hatua za kimahakama lazima zichukuliwe ili wale wote wanaotumika kulichafua Kama wana ushahidi wa kweli waueleze na hatua zichukuliwe kwa yeyote atakayekuwa ana nia ovu dhidi ya Kanisa la KKKT.