Makamu mkuu wa chuo cha mtakatifu Augustino SAUT,tawi la Mwanza,dk Charles Kitima amesema kutokana na mambo ya hovyohovyo yanayofanywa na serikali dhaifu ya CCM ni lazima itaondoka madarakani 2015 hata kama wataandaa mbinu zote za kuiba kura. Huku akishangiliwa kwa nguvu na wanachuo, Kitima anasema serikali haiwezi kudumu wakati wananchi wamepigika.
Wabunge wake wakipitisha bujeti mbovu na isiyo na maslahi,pia dk Kitima alianza kwa kuuponda upinzani wa Tz huku akimtaja mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani na mbunge wa singida mashariki Tundu Lissu kwa kudai hajafanya jambo lolote jimboni mwake,na akitoboa siri kwamba hyo ndo sababu kubwa iliyomfanya asimruhusu kipindi flani asitoe mhadhara.
Itakumbukwa kuwa mwaka juzi Tundu Lissu alizuiwa asitoe mhadhara chuoni hapa kwa madai amepigiwa simu na usalama wataifa wakimtaka asimruhusu Tundu kutoa mada.,dk Kitima yupo mda huu anazungumza kama mchangiaji wa mada ya'AMANI NA MAENDELEO YA TANZANIA,'ambapo mgeni rasmi ni waziri wa mahusiano ndugu Steveni Wassira ,na mgeni mwalikwa mbunge wa Talime Nyambali Nyagwine.
Katika uwasilishwaji wa mada hii unaofanyika chuoni hapa,Wassira alianza kwa kutamba kwamba serikali kwa mda wa miaka yote 50 tangu uhuru imefanikiwa kudumisha Amani na Utulivu nchini,huku akisema kitu ambacho wapinzani hawawezi.
Nae mbunge Nyangwine amewataka wapinzani kuacha kulalamika kwani wanaweza kuliambukiza taifa na kuwa taifa la walalamikaji,huu ni mfululizo mwingne wa viongozi wa CCM na serikali kukitembelea chuo hiki ambacho ni maarufu kwa siasa za CHADEMA.
Wassira amekuja akitanguliwa na mawaziri wengne kama profesa Muhongo,Nyalandu na Sitta na wote wamekuwa wakipewa ukumbi ndani ya chuo na kuongea mambo tofauti na mada husika,wakijikita ,kinyume na ibara ya 53 na 54 za sheria ya vyuo vikuu inayokataza siasa vyuoni.

MwanzaMakamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino, Dk Charles Kitima amekitabiria kifo Chama Cha Mapinduzi kama kitaendelea na mtindo wa kuwanyima fursa wazawa katika maendeleo.
Akizungumza katika kongamano la kujadili amani na maendeleo na mpango wa miaka mitano wa kukuza uchumi na kuondoa umaskini nchini lililofanyika chuoni hapo jijini Mwanza, Dk Kitima alisema nchi haiwezi kufikia dira ya maendeleo ikiwa Serikali imeshindwa kutoa kipaumbele katika utawala mzuri wa rasilimali na wazawa:
"CCM isipojirekebisha itakufa mapema kama isipoipa kipaumbele sekta binafsi ya wazawa katika kusimamia rasilimali ya nchi.Tunataka rasilimali za nchi tusimamie wenyewe," alisema Charles Kitima.
Akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Uhusiano na Urtatibu, Steven Wassira aliyekuwa mgeni rasmi, aliongeza kuwa nchi itaendelea kwa kuwapa fursa wananchi wake.
Kwa upande wake Waziri Wassira alikiri kuwa umaskini wa Tanzania unasababishwa na kutokuwapo kwa uzalendo, kupungua kwa uadilifu na mfumo mbovu ya ufuatiliaji na utekelezaji wa mipango. "Uadilifu umekuwa mdogo sana kwa viongozi wetu wa leo. Mawazo yaliyotawala ni wizi tu na mimi sina mpango wa kuiba"alisema Wassira.
Hata hivyo Wassira alisema kutokuwa na uelewa tulikotoka nayo ni sababu kubwa kwa wananchi kutokujua maendeleo yaliyofikiwa kwa miaka 50 ya uhuru.
"Tanzania ni nchi tuliyoirithi ikiwa ni shamba tu hatukukuta kitu. Hapakuwa na barabara za kutosha, elimu haikupewa kipaumbele, kutoka wasomi wachache wa mwaka 1961 sasa kuna vyuo 44'' alisema.
Naye Mhadhiri wa Sheria chuoni hapo, Adelardius Kilange alisema tatizo la umaskini nchini linatokana na wananchi kukosa misingi imara ya itikadi ya siasa na uchumi wa jamii na kwamba ipo haja kwa Serikali kujipanga.