Dk Kitima aitabiria mabaya CCM mbele ya Wassira

oneblood

JF-Expert Member
Dec 27, 2011
244
51
Makamu mkuu wa chuo cha mtakatifu Augustino SAUT,tawi la Mwanza,dk Charles Kitima amesema kutokana na mambo ya hovyohovyo yanayofanywa na serikali dhaifu ya CCM ni lazima itaondoka madarakani 2015 hata kama wataandaa mbinu zote za kuiba kura. Huku akishangiliwa kwa nguvu na wanachuo, Kitima anasema serikali haiwezi kudumu wakati wananchi wamepigika.

Wabunge wake wakipitisha bujeti mbovu na isiyo na maslahi,pia dk Kitima alianza kwa kuuponda upinzani wa Tz huku akimtaja mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani na mbunge wa singida mashariki Tundu Lissu kwa kudai hajafanya jambo lolote jimboni mwake,na akitoboa siri kwamba hyo ndo sababu kubwa iliyomfanya asimruhusu kipindi flani asitoe mhadhara.

Itakumbukwa kuwa mwaka juzi Tundu Lissu alizuiwa asitoe mhadhara chuoni hapa kwa madai amepigiwa simu na usalama wataifa wakimtaka asimruhusu Tundu kutoa mada.,dk Kitima yupo mda huu anazungumza kama mchangiaji wa mada ya'AMANI NA MAENDELEO YA TANZANIA,'ambapo mgeni rasmi ni waziri wa mahusiano ndugu Steveni Wassira ,na mgeni mwalikwa mbunge wa Talime Nyambali Nyagwine.

Katika uwasilishwaji wa mada hii unaofanyika chuoni hapa,Wassira alianza kwa kutamba kwamba serikali kwa mda wa miaka yote 50 tangu uhuru imefanikiwa kudumisha Amani na Utulivu nchini,huku akisema kitu ambacho wapinzani hawawezi.

Nae mbunge Nyangwine amewataka wapinzani kuacha kulalamika kwani wanaweza kuliambukiza taifa na kuwa taifa la walalamikaji,huu ni mfululizo mwingne wa viongozi wa CCM na serikali kukitembelea chuo hiki ambacho ni maarufu kwa siasa za CHADEMA.

Wassira amekuja akitanguliwa na mawaziri wengne kama profesa Muhongo,Nyalandu na Sitta na wote wamekuwa wakipewa ukumbi ndani ya chuo na kuongea mambo tofauti na mada husika,wakijikita ,kinyume na ibara ya 53 na 54 za sheria ya vyuo vikuu inayokataza siasa vyuoni.
MwanzaMakamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino, Dk Charles Kitima amekitabiria kifo Chama Cha Mapinduzi kama kitaendelea na mtindo wa kuwanyima fursa wazawa katika maendeleo.

Akizungumza katika kongamano la kujadili amani na maendeleo na mpango wa miaka mitano wa kukuza uchumi na kuondoa umaskini nchini lililofanyika chuoni hapo jijini Mwanza, Dk Kitima alisema nchi haiwezi kufikia dira ya maendeleo ikiwa Serikali imeshindwa kutoa kipaumbele katika utawala mzuri wa rasilimali na wazawa:

"CCM isipojirekebisha itakufa mapema kama isipoipa kipaumbele sekta binafsi ya wazawa katika kusimamia rasilimali ya nchi.Tunataka rasilimali za nchi tusimamie wenyewe," alisema Charles Kitima.

Akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Uhusiano na Urtatibu, Steven Wassira aliyekuwa mgeni rasmi, aliongeza kuwa nchi itaendelea kwa kuwapa fursa wananchi wake.

Kwa upande wake Waziri Wassira alikiri kuwa umaskini wa Tanzania unasababishwa na kutokuwapo kwa uzalendo, kupungua kwa uadilifu na mfumo mbovu ya ufuatiliaji na utekelezaji wa mipango. "Uadilifu umekuwa mdogo sana kwa viongozi wetu wa leo. Mawazo yaliyotawala ni wizi tu na mimi sina mpango wa kuiba"alisema Wassira.

Hata hivyo Wassira alisema kutokuwa na uelewa tulikotoka nayo ni sababu kubwa kwa wananchi kutokujua maendeleo yaliyofikiwa kwa miaka 50 ya uhuru.

"Tanzania ni nchi tuliyoirithi ikiwa ni shamba tu hatukukuta kitu. Hapakuwa na barabara za kutosha, elimu haikupewa kipaumbele, kutoka wasomi wachache wa mwaka 1961 sasa kuna vyuo 44'' alisema.

Naye Mhadhiri wa Sheria chuoni hapo, Adelardius Kilange alisema tatizo la umaskini nchini linatokana na wananchi kukosa misingi imara ya itikadi ya siasa na uchumi wa jamii na kwamba ipo haja kwa Serikali kujipanga.
 
Bavicha ni janga la Taifa.

Hata mpangilio wa uandishi ni kizungumkuti achilia mbali kujenga hoja kimantiki.

Hiki ulichokiandika ndiyo nini?. Pay attention kwanza kwenye elimu ili uelimike.
 
Haya tusubiri tuone

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Bavicha ni janga la Taifa.

Hata mpangilio wa uandishi ni kizungumkuti achilia mbali kujenga hoja kimantiki.

Hiki ulichokiandika ndiyo nini?. Pay attention kwanza kwenye elimu ili uelimike.

Unaifahamu BAVICHA nini ?, kwani iliyoandika hapo ni BAVICHA ?
 
Bavicha ni janga la Taifa.

Hata mpangilio wa uandishi ni kizungumkuti achilia mbali kujenga hoja kimantiki.

Hiki ulichokiandika ndiyo nini?. Pay attention kwanza kwenye elimu ili uelimike.

ukweli unaumaaa ohooooooooooooo..pole sana
 
Namkubali sana huyu jamaaa.....ni mtu jasiri sana.
 
Unaifahamu BAVICHA nini ?, kwani iliyoandika hapo ni BAVICHA ?
Definition ya bavicha inapatikana kwenye mantiki iliyoko kwenye hilo bandiko hapo juu. Utakacho kipata kwenye hilo bandiko ndiyo bavicha UNLESS na wewe ni bavicha kwa maana kuwa, hutaelewa mantiki iliyotumika katika bandiko hilo.
 
Kwa ujinga ambao bado umeganda kichwani mwa baadhi ya viongozi ni vigumu sana kuiondoa ccm madarakani,labda mpaka waachane na ukabila,udini,na upendeleo.
 
alianza kwa kuuponda upinzani wa Tz huku akimtaja mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani na mbunge wa singida mashariki Tundu Lissu kwa kudai hajafanya jambo lolote jimboni mwake

Hapo ndipo mimi napinga. Kwani kazi ya mbunge ni nini? Ninachofahamu kuwa kazi ya mbunge ni kuwakilisha wananchi wake katika bunge, kufikisha matatizo yao ili yatekelezwe na serikali iliyo na madaraka na uwezo wa kufanya hivyo. Kama mbunge atakuwa anafanya hivyo atakuwa anatimiza majukumu yake. Kama kero za wananchi hazitafutiwi ufumbuzi hapo ni serikali inalaumiwa. Nikimsikiliza Tundu Lisu anaongelea kero nyingi sana za wananchi hata kuliko wabunge wengine wengi. Kama hakuna kitu kilichofanyika jimboni mwake, wa kulaumiwa ni serikali yenye fungu la pesa na si mbunge.
 
ukweli unaumaaa ohooooooooooooo..pole sana
Ukweli utauma vipi kwa bandiko ambalo hata halieleweki kiuandishi achilia mbali kimantiki. Ukweli utaujua wewe kwa sababu fikra zako na mleta bandiko ziko sawa. Ndege huruka kwa makundi hata bavicha nao vivyo hivyo.
 
Kuna kitu bado sijaelewa hapo kuhusu Tundu Lissu na Upinzani.

Huenda mleta mada katuchanganya au Dr.Kitima kapotoka!!

Kusema kuwa Dr.Kitima alimkataza Tundu Lissu asifanye Mhadhara hapo chuoni kisa hajafanya maendeleo jimboni kwake, hicho ni kichekesho kikubwa kwa sababu:

1/Anadai hiyo ilikuwa mwaka juzi(2011) na Tundu Lissu ameingia bungeni mwishoni mwa 2010, alitegemea maendeleo gani kwa muda huo kutoka kwa mbunge mpya tena kutoka upinzani?

2/Je, ni sera ya chuo chake kumwita mwanasiasa kama mbunge ili kutoa muhadhara SAUT kwa kigezo cha maendeleo aliyoleta jimboni mwake?

3/Je, hao wanasiasa wabunge wa CCM wamefanya nini kikubwa cha maendeleo majimboni mwao mpaka wapewe nafasi?

4/Paul Makonda sio mbunge wala kiongozi wa nchi bali ni kada wa CCM, naye siku chache zilizopita alikuja SAUT akiwa na Samweli Sitta nk na kupewa nafasi ya kuongea, ni maendeleo yapi amefanya katika nchi yetu mpaka apewe nafasi hiyo?
 
Unaifahamu BAVICHA nini ?, kwani iliyoandika hapo ni BAVICHA ?

Huwafahamu hao nini!?? kila kitu CHADEMA, wao kila atakaeenda kinyume nao ni CHADEMA, Hukuona Nape alivyowatukana wananchi wa Tabora kuwa CHADEMA wanawashikisha ukuta kisa walimpinga jukwaani...!??
 
Kama ni kweli Dr. Kitima hakumkaribisha TL kwa sababu hajafanya lolote jimboni mwake, basi ni dhahili nchi yetu ina matatizo makubwa kuliko tuynavyodhani!
 
Back
Top Bottom