Dk. Kitila Mkumbo hajasoma vema Katiba ya CHADEMA... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Kitila Mkumbo hajasoma vema Katiba ya CHADEMA...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kitero, Oct 16, 2012.

 1. k

  kitero JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 563
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ASALAMU WANA JF. Napenda kuchukuwa nafasi hii kumfahamisha dk.kitila mkumbo kuhusu taarifa yake aliyo itoa ktk gazeti la raia mwema ktk hoja yake kuwa kutangaza niya mapema mwana chama wa chadema hakuna makosa tena sio uvunjaji wa katba ya chama.

  Katka hili Dk. Mkumbo hayupo sahihi ukweli ni kwamba katba ya chadema imeelezea utaratibu wa uchaguzi na mamlaka ya kutangaza ratiba ya uchaguzi ndani ya chama tena imeweka wazi kikao chenye mamlaka ya kupanga kutangaza ratiba ya uchaguzi ndani ya chama uwe ni uchaguzi wa viongozi wa chama au wawa kirishi wa chama ktk serikali hivyo mwanachama tena ni kiongozi yeyote akijitangaza kugombea wakati kikao chenye mamlaka hakija toa tangazo la uchaguzi ni kinyume cha katba ya chadema pia ni kukiuka maadili ya chama mimi nawashauri kwanza someni katba kwa utulivu someni kazi za baraza kuu na kazi za kamati kuu.

  Ndio sasa mtowe ushauri sipo kwa marumbano ila natekeleza wajibu wa katba ya chadema. Pia katba inapatikana ktk www.chadema.com. nawasilisha
   
 2. E

  Eberhard JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,024
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Katba- usijibu/usiandike hivyo kwenye mtihani. Unasikia?
   
 3. Ufipa-Kinondoni

  Ufipa-Kinondoni JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 4,481
  Likes Received: 2,144
  Trophy Points: 280
  Nadhani Dr anaweza eleweka tofauti lakini katiba haijaonyesha muda wa kutangaza nia. Katika sura ya 6.3.1. utaona maelezo ya jumla wa jinsi ya kupata viongozi.

  Hivyo, kutangaza nia sio kosa kwa sababu mwisho ni utaratibu wa kichama utachukuliwa. Kumbuka huwezi kuomba kugombea bila kufanya nia.

  Kama kuna makosa basi marekebisho ya katiba kwa baadaye izingatie hili.
   
 4. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ni nini?
   
 5. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hakuna kosa kutangaza nia, nia haitegemea ratiba ya chama ya uchaguzi ni utashi wa mtu tu!
   
 6. Mwakitobile

  Mwakitobile JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 453
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Haya mambo yenu ya chadema pelekeni kule Chaga forum.
   
 7. JOASH MUSSA

  JOASH MUSSA JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Ijapokuwa hukuweka spaces, koma, nukta na enter lakini sio mbaya nimekuelewa ila sio www.chadema.com ila ni www.chadema.or.tz nawashauri akina kitila mkumbo wasome katiba na hata wanachama na viongozi wa Kata, Matawi na Misingi ya CHADEMA wasome katiba ili wajue nini wafuate nini wasifuate
   
 8. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Sio kuwa hajasoma tu hata kuandika paper hawa Maprof na Madokta wa vyuo vyetu hawaandiki, Tafadali Maprof na Madokta na wanazuoni kwa ujumla andikeni paper, andiken jamani
   
 9. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Naona mleta mada kalewa chimpumu

  Sidhani kama kutangaza nia ni kinyume cha katiba, ila tatizo la kutangaza nia saa hii linadistabilize chadema ambayo bado ipo kewnye team formation

  Kitila is right, ila kugombea sasa si mujarabu
   
 10. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Haya sred itakuwa imeandikwa na Lema sio bure.
   
 11. d

  dkaali1 Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mbona tunakuwa wazito wa kuelewa au tunajaribu kuukana ukweli kwa hofu. Zitto ni janga la taifa. Anatumiwa na hao wachoma makanisa. Huoni wanavyomfanyia reference kila wakileta dhana zao za 'kuonewa'? Mie naomba great thinkers tuipotezee hii issue ya zitto inalenga kuvuruga amani ya nchi kwa kutumia udini.
   
 12. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,503
  Likes Received: 5,616
  Trophy Points: 280
  Kiongozi wa Chama anapotumia makala kutetea jambo linalozua malalamiko kwa baadhi ya viongozi wenzake! Vipi kamanda Mbowe akiandika makala kuwa ni kosa hapo ndio demokrasia mnayoitaka itakuwa imekamilika?

  Swala lililozua gumzo kama hili linahitaji kiongozi kuandika makala? au Chama kutoa kauli rasmi iliyokubaliwa na vikao halali? Au Dr Kitila anadhani mawazo yake na hao wanaofikiri kama yeye watashindwa kushawishi viongozi wenzao ndani ya vikao halali hivyo ikabidi atushawishi kwa namna nyingine?

  Mwisho mbona akina Dr Kitila hawaandiki makala za M4C,operation Sangara,au basi hata sera za kukiuza chama chao lakini mambo yenye element za makundi ndio watu wanakuwa mabingwa wa kuchambua siasa kwenye makala? Sipendi unafiki lakini ujuaji utakiua Chadema,kila mtu anajua na hakuna collective responsibility utafikiri ni serikali ya J.K!

  Yetu macho!
   
 13. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu, na huyo Dr.Kitila ni janga pia
   
 14. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Dr.Kitila mbona aliumbuliwa juzi na mwanafunzi wake wa mwaka wa kwanza kwamba wote ni wavivu wa kuandika na wakiandika wanatoa vitu vya juujuu tu kama hiyo makala yake , sasa naanza kuamini yule jamaa aliyechangia mada ni bora kuliko walimu wake.Pole dr.kilila rudi ktk mstari
   
 15. H

  Haika JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  HASWA!!!
  kama vile uko akilini mwangu.
  Mie huwa nikikutana na wanachama hawa au wakereketwa mara zote nawaambia, Wajitambue kuwa sasa maneno yao ya kienyeji bila mpangilio ndio kifo chao,
  Watofautishe wakereketwa na wanachama, offcourse na critics wa ukweli.
  Hawa wasemaji please waweze kufikia kiwango/ level ya utambuzi ya wantanzania, sasa wanaongea kwa level ya chini mno.

  Ni kweli Wanazania tunataka mabadiliko, ila wengi bado tunahitaji mtu wa wa kuaminika kifikra kutupeleka huko, lazima aongee tumsikie

  Kila mmoja CDM ni mjuaji ajabu!!

  Asante kwa kuliweka hili
  Chama kina nia nzuri, kina viongozi wazuri tu, halafu wengi, lakini sasa, hakuna control, hakuna utaratibu,
  Hatuoni filosofia ya chama ikikiongoza,
  tunaona magumzo, kama vile kimechanganyikiwa kwa mafanikio madogo,

  Inabidi wale wanaoitwa THINK TANKS wao wakae wajue namna ya kucontain hii confusion
   
 16. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ZZK family
   
 17. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,503
  Likes Received: 5,616
  Trophy Points: 280
  Kwakweli umehitimisha vizuri mno kamanda,kudos!!!
   
 18. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tupe ibara tufuatilie vizuri. Asante.
   
 19. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ni vizuri kusoma maandishi pembeni na katikati ya mstari ili kupata mantiki yake vizuri. Ukisoma juujuu utaibuka na hitimisho la juujuu.

  Naelewa hasira zinatokana na makala inayowakosoa Zitto na wakosoaji wake. Naelewa vilevile kwamba ambacho nilitakiwa kuandika ni kuungana na wengine kumlaani vikali Zitto kwa kutangaza kugombea urais, na sio kuwalaumu pia wale wanaomlaumu yeye. Huu ndio utamaduni unaotakiwa kwa sasa katika siasa za Tanzania, hasa hapa jamvini kwetu JF-group think!

  Lakini ni muhimu tukakumbuka kwamba utamaduni wa fikra hodhi kwa kisingizio cha kutetea maslahi ya chama ndio iliyoifikisha CCM hapa na ndio mwanzo wa kumomonyoka kwa utamaduni wa kuwajibika katika nchi hii. Tumeua kabisa fikra huru kwa sababu ya kuogopa kuonekana tunaenda kinyume na watu fulani.

  Mwalimu Nyerere ametufundisha katika kitabu chake cha 'Tujirekibisha' kwamba kosa ni kosa tu bila kujali nani kafanya kosa. Narudia kusema kama nilivyosema katika makala yangu kwamba 'kosa' la Zitto kutangaza urais ni la kimantiki na la kiutamaduni zaidi na wala halina uhusiano wowote na yeye kuvunja sheria au kanuni yeyote ya chama na katika nchi. Sasa sioni kusema hivi kunachangia vipi kuleta mzozo ndani ya chama.

  Demokrasia ndani ya vyama na nje haijengwi kwa kuficha fikra na mawazo ndani ya uvungu wa kitanda. Demokrasia inakuzwa kwa mnyukano wa fikra, uwazi na ukweli. Msimamo wa pamoja wa viongozi unatakiwa katika mambo ya msingi ya kisera na kimkakati na sio katika kila jambo. Kutaka wote muwe na mfanano katika fikra na mitazamo kwa kila jambo ni kujaribu kuwafanya watu wawe binadamu nusu na wanasiasa nusu. Hivi tunavyoongea maelfu ya wanachadema wamekwisha kutangaza nia na haja zao za kugombea udiwani na ubunge katika uchaguzi ujao, katika majimbo na katakata mbalimbali, zenye madiwani na wabunge wetu na zile ambazo hatuna. Sasa kama kule katika majimbo na kata hakuna tatizo kwa nini iwe tatizo juu? Au ndio tunatakiwa tuendelee utamaduni wa CCM wa kuruhusu wanachama wao kufikiria kugombea nafasi yeyote lakini sio uenyekiti?

  Kupachika watu majina na kuwaweka kwenye mafungu kwa sababu hajafikiri na kutenda kama wewe ni fitina, na ni jambo ambalo Mwalimu alilikemea sana katika uongozi, nami nalikemea kabisa katika wiki hii tunayeendelea kumkumbuka Mwalimu. Kwa wale ambao hawakusoma makala yangu, naiweka tena hapa.
  ______________________________________________________________________________________

  Unafsi wa Zitto na wapinzani wake

  Kitila Mkumbo

  Raia Mwema, Toleo la 262

  10 Oct 2012

  KATIKA siku za hivi karibuni kumetokea malumbano kutokana na uamuzi wa Zitto Kabwe kutangaza kwamba atagombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao. Katika kutekeleza azima yake hiyo ametangaza pia kwamba hatogombea tena nafasi ya ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini. Ikumbukwe kwamba hii si mara ya kwanza kwa Zitto Kabwe kutangaza kutogombea ubunge huko Kigoma Kaskazini.
  Mwaka 2007 akiwa ziarani nje ya nchi alitangaza kwamba asingegombea ubunge katika uchaguzi wa mwaka 2010. Hata hivyo aligombea na akashinda na ni mbunge hadi leo hii. Nitaeleza baadaye katika makala haya nini maana yake kisiasa na yeye mwenyewe Zitto ni mwanasiasa wa namna gani.
  Watu kadhaa ndani na nje ya CHADEMA wamehamaki baada ya Zitto kutangaza nia yake ya kugombea urais. Wengi wa wanaopinga kauli ya Zitto wanaipinga kwa minajili kwamba ametangaza mapema na kutangaza huko kutasababisha mgogoro, mgawanyiko na fujo katika chama.
  Hamaki hii imekolezwa zaidi na mwasisi wa CHADEMA na mwanasiasa mkongwe hapa nchini, Mzee Edwin Mtei, ambaye amesema kwamba hatua ya Zitto kutangaza mapema kugombea urais ‘itasababisha mzozo na mpasuko' kwa kuwa wapo wanachama wengine pia wanaoutaka urais. Kuna wengine ambao wamemuona Zitto Kabwe kwamba ni mbinafsi anayejijali zaidi yeye bila kujadili mustakabali wa chama chake.
  Wengine wameenda mbali zaidi na kusema kwamba Zitto Kabwe amenunuliwa na anakitumikia Chama cha Mapinduzi na kutangaza urais ni moja ya mikakati katika kufikia azima ya kuidhoofisha CHADEMA. Katika makala haya ninajadili mantiki ya hoja hizi na kuanisha kama uamuzi wa Zitto kutangaza kugombea urais ni jambo la afya kwa CHADEMA na demokrasia yetu au la.
  Pamoja na kwamba nami pia siungi mkono tabia ya wanasiasa, hasa katika CHADEMA kutangaza katika muda huu kugombea urais, siwaoni wanasiasa hao kama wanakikosea chama chao kufanya hivyo. Aidha, siwaungi mkono kabisa wale wote wanaompinga Zitto Kabwe kutangaza kuutaka urais katika kipindi hiki.
  Siyaungi mkono makundi haya kwa sababu nadhani kwamba yanaenda kinyume cha utamaduni wa kisiasa tunaojaribu kuujenga ndani ya CHADEMA. Kimsingi, makundi yote mawili, Zitto na wapinzani wa tabia zake, wanaendekeza unafsi, jambo ambalo CHADEMA wanajaribu kulikomesha katika siasa za Tanzania. Nitaeleza baadaye maana ya dhana hii.
  Wanasiasa wa aina ya Zitto Kabwe ni waathirika wa mfumo uchwara wa uliberali ambao tumeamua kuufuata kimya kimya bila hata kuuelewa vizuri.
  Aidha, hamaki na upinzani dhidi ya kutangaza kugombea urais inadhihirisha jinsi ambavyo wengi wetu hatujaielewa vizuri dhana ya uongozi katika mfumo tulio nao wa uliberali uchwara. Tunataka tutende kijamaa wakati tunaishi kiliberali. Katika mfumo wa ujamaa tuliojaribu kuujenga baada ya uhuru, suala la uongozi lilikuwa si suala la mtu binafsi.
  Uongozi ulikuwa ni jukumu la wanataasisi kuamua nani anafaa katika nafasi gani. Hivi ndivyo Rashidi Kawawa alivyoweza kuacha cheo cha uwaziri mkuu kwa kumpisha Edward Moringe Sokoine na yeye kuchukua nafasi ya Waziri wa Ulinzi.
  Hii ni kwa sababu enzi hizo waliokuwa wanaamua nani ashike nafasi gani ni chama na si mtu kujichagulia nafasi ya uongozi. Katika enzi za ujamaa wetu wa kitanzania, kiongozi mwenye cheo kikubwa na kidogo wote walikuwa ni viongozi wanaoheshimika na kuheshimiana; na ndio maana wote waliitwa ‘ndugu', sawa na wananchi wenzao ambao hawakuwa viongozi.
  Utaratibu huu tumeuua baada ya kuanza mfumo wa vyama vingi na kuamua kuufuata mfumo wa kiliberali bila kuuelewa sawa sawa misingi yake. Katika mfumo wa kiliberali uchwara inaelekea haikubaliki kwa mtu aliyewahi kuwa waziri mkuu arudi kuwa waziri wa kawaida. Katika mfumo wa kiliberali, ngazi moja ya uongozi huzalisha ngazi nyingine ya juu zaidi, na ukishaenda huko hurudi chini bali unahakikisha unaendelea kwenda juu zaidi. Kwa hiyo, ukizingatia mantinki hii ya uliberali uchwara, huwezi kumshangaa Zitto kwa kuutaka urais na kusema kwamba yeye sasa ubunge basi; anataka kwenda juu zaidi na pengine ubunge sio saizi yake!
  Kwa hiyo, Zitto Kabwe ameonyesha unafsi ambao ni tabia ya kawaida katika uliberali, hususani huu uliberali uchwara tunaofuata sisi. Mfumo huu una tabia ya kuzalisha viongozi wenye matamanio na utashi binafsi. Katika mfumo huu uongozi ni biashara. Ili uwe kiongozi katika mfumo wa kiliberali lazima uonyesha matamanio na utashi, na ujiuze vya kutosha kabisa. Kwa hiyo kutangaza nia na kujimwagia sifa juu ya uwezo ulio nao katika nafasi fulani ni sehemu kabisa ya mfumo wa kutafuta uongozi katika mfumo wa kiliberali.
  Uongozi katika mfumo wa kiliberali ni juu ya mtu na wala sio juu ya taasisi. Anayepata uongozi katika mfumo huu ni yule mwenye uwezo wa kutengeneza mtandao wa wafuasi ambao atahakikisha anakuwa nao kwa kipindi chote hadi uchaguzi utakapofanyika.
  Mkakati mwafaka wa kutafuta uongozi katika mfumo wa kiliberali unaambiwa ni kufanya maandalizi mapema. Huu ndio utamaduni ambao CCM imeuasisi kuanzia mwaka 1995 na ambao mtu alitarajia CHADEMA wangeukwepa.
  Hata hivyo, sioni kwamba kitendo cha Zitto Kabwe kutangaza kuutaka urais kama ni kosa kwa sababu CHADEMA haijaweka rasmi utaratibu wa kuukataa utamaduni huu. Kwa kuwa utamaduni huu haujakataliwa rasmi kimfumo, haiwezi ikawa kosa mtu moja moja kuchagua kuutumia. Ndio maana Mzee Mtei kawataja watu wengine kadhaa, akiwamo yeye, kwamba nao wanaoutaka urais lakini hawajatangaza nia bado kwa hoja eti muda wa kufanya hivyo bado, kama vile ndani ya CHADEMA kuna muda rasmi uliowekwa wa kutangaza nia ya kugombea.
  Ni wazi basi kwamba hata wale wanaompinga na kumzomea Zitto Kabwe kuutaka urais wanaonyesha unafsi. Hawafanyi vile kwa sababu wana misingi fulani wanayoiamini juu ya namna ya kupata uongozi, la hasha. Hawa wanafanya hivyo kwa sababu ya aina ya pili ya unafsi, ambayo ni fitina.
  Hawa wanajaribu kuonyesha kwamba Zitto Kabwe kafanya kosa kubwa kutangaza kugombea urais, lakini hawasemi ni kosa gani na amevunja kanuni gani ndani ya chama. Wengine wameenda mbali zaidi na kumuona Zitto kama ni msaliti ambaye amenunuliwa ili kukidhoofisha CHADEMA.
  Hii ni fitina na ni aina mbaya kabisa ya unafsi na tabia inayojitokeza vile vile katika uliberali uchwara. Nina wasiwasi kwamba watu wanaompinga Zitto kwamba nao labda wana watu wanaodhani wanafaa kuwa marais na wanajaribu kumchonganisha Zitto na jamii, ili hatimaye njia yao ya kuusaka urais iwe nyeupe huko mbele.
  Katika mfumo wa kidemokrasia za kiliberali kutangaza kugombea urais hakupaswi kuleta mzozo wala vurugu katika chama. Wakati mwingine kitendo cha Zitto ni jibu kwa wapinzani wa CHADEMA aina ya Samuel Sitta wanaojaribu kujenga taswira ya hovyo kwamba ndani ya CHADEMA hakuna wenye uwezo wa urais zaidi ya Dk. Slaa aliyegombea kwa mafanikio mwaka 2010.
  Kwa hiyo, wakati huu ambapo CHADEMA haina mwongozo elekezi juu ya namna ya ‘kuutaka' urais, kutangaza kuutaka urais mapema ndio demokrasia yenyewe . Kwa hiyo tunapaswa kuwatia moyo wanachama wengine wenye matamanio ya urais watangaze wakati wowote na mahala popote wanapojisikia, wakati tukiweka misingi murua ya namna ya kupata mgombea mwafaka kwa wakati husika kutoka kwenye kundi la hao wanaojitangaza au wengine.
  Kwa hiyo, wosia wangu wa leo ni kwamba kutangaza kugombea urais mapema hakupaswi kuleta mzozo au vurugu katika chama cha kidemokrasia kama CHADEMA. Ndiyo kusema hakuna sababu ya kupachika watu majina ya kifitina wanaotangaza kuutaka urais sasa na baadaye.
  Muhimu ni kuweka mfumo utakaohakikisha kwamba CHADEMA hakizidiwi na nguvu za mfumo wa uliberali uchwara ambao umetamalaki nchini, ili hatimaye chama ndicho kiamue nani anakuwa mgombea.
   
 20. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #20
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ni vizuri kusoma maandishi pembeni na katikati ya mstari ili kupata mantiki yake vizuri. Ukisoma juujuu utaibuka na hitimisho la juujuu.

  Naelewa hasira zinatokana na makala inayowakosoa Zitto na wakosoaji wake. Naelewa vilevile kwamba ambacho nilitakiwa kuandika ni kuungana na wengine kumlaani vikali Zitto kwa kutangaza kugombea urais, na sio kuwalaumu pia wale wanaomlaumu yeye. Huu ndio utamaduni unaotakiwa kwa sasa katika siasa za Tanzania, hasa hapa jamvini kwetu JF-group think!

  Lakini ni muhimu tukakumbuka kwamba utamaduni wa fikra hodhi kwa kisingizio cha kutetea maslahi ya chama ndio iliyoifikisha CCM hapa na ndio mwanzo wa kumomonyoka kwa utamaduni wa kuwajibika katika nchi hii. Tumeua kabisa fikra huru kwa sababu ya kuogopa kuonekana tunaenda kinyume na watu fulani.

  Mwalimu Nyerere ametufundisha katika kitabu chake cha 'Tujirekibisha' kwamba kosa ni kosa tu bila kujali nani kafanya kosa. Narudia kusema kama nilivyosema katika makala yangu kwamba 'kosa' la Zitto kutangaza urais ni la kimantiki na la kiutamaduni zaidi na wala halina uhusiano wowote na yeye kuvunja sheria au kanuni yeyote ya chama na katika nchi. Sasa sioni kusema hivi kunachangia vipi kuleta mzozo ndani ya chama.

  Demokrasia ndani ya vyama na nje haijengwi kwa kuficha fikra na mawazo ndani ya uvungu wa kitanda. Demokrasia inakuzwa kwa mnyukano wa fikra, uwazi na ukweli. Msimamo wa pamoja wa viongozi unatakiwa katika mambo ya msingi ya kisera na kimkakati na sio katika kila jambo. Kutaka wote muwe na mfanano katika fikra na mitazamo kwa kila jambo ni kujaribu kuwafanya watu wawe binadamu nusu na wanasiasa nusu. Hivi tunavyoongea maelfu ya wanachadema wamekwisha kutangaza nia na haja zao za kugombea udiwani na ubunge katika uchaguzi ujao, katika majimbo na katakata mbalimbali, zenye madiwani na wabunge wetu na zile ambazo hatuna. Sasa kama kule katika majimbo na kata hakuna tatizo kwa nini iwe tatizo juu? Au ndio tunatakiwa tuendelee utamaduni wa CCM wa kuruhusu wanachama wao kufikiria kugombea nafasi yeyote lakini sio uenyekiti?

  Kupachika watu majina na kuwaweka kwenye mafungu kwa sababu hajafikiri na kutenda kama wewe ni fitina, na ni jambo ambalo Mwalimu alilikemea sana katika uongozi, nami nalikemea kabisa katika wiki hii tunayeendelea kumkumbuka Mwalimu. Kwa wale ambao hawakusoma makala yangu, naiweka tena hapa.
  ______________________________________________________________________________________

  Unafsi wa Zitto na wapinzani wake

  Kitila Mkumbo

  Raia Mwema, Toleo la 262

  10 Oct 2012

  KATIKA siku za hivi karibuni kumetokea malumbano kutokana na uamuzi wa Zitto Kabwe kutangaza kwamba atagombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao. Katika kutekeleza azima yake hiyo ametangaza pia kwamba hatogombea tena nafasi ya ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini. Ikumbukwe kwamba hii si mara ya kwanza kwa Zitto Kabwe kutangaza kutogombea ubunge huko Kigoma Kaskazini.
  Mwaka 2007 akiwa ziarani nje ya nchi alitangaza kwamba asingegombea ubunge katika uchaguzi wa mwaka 2010. Hata hivyo aligombea na akashinda na ni mbunge hadi leo hii. Nitaeleza baadaye katika makala haya nini maana yake kisiasa na yeye mwenyewe Zitto ni mwanasiasa wa namna gani.
  Watu kadhaa ndani na nje ya CHADEMA wamehamaki baada ya Zitto kutangaza nia yake ya kugombea urais. Wengi wa wanaopinga kauli ya Zitto wanaipinga kwa minajili kwamba ametangaza mapema na kutangaza huko kutasababisha mgogoro, mgawanyiko na fujo katika chama.
  Hamaki hii imekolezwa zaidi na mwasisi wa CHADEMA na mwanasiasa mkongwe hapa nchini, Mzee Edwin Mtei, ambaye amesema kwamba hatua ya Zitto kutangaza mapema kugombea urais ‘itasababisha mzozo na mpasuko’ kwa kuwa wapo wanachama wengine pia wanaoutaka urais. Kuna wengine ambao wamemuona Zitto Kabwe kwamba ni mbinafsi anayejijali zaidi yeye bila kujadili mustakabali wa chama chake.
  Wengine wameenda mbali zaidi na kusema kwamba Zitto Kabwe amenunuliwa na anakitumikia Chama cha Mapinduzi na kutangaza urais ni moja ya mikakati katika kufikia azima ya kuidhoofisha CHADEMA. Katika makala haya ninajadili mantiki ya hoja hizi na kuanisha kama uamuzi wa Zitto kutangaza kugombea urais ni jambo la afya kwa CHADEMA na demokrasia yetu au la.
  Pamoja na kwamba nami pia siungi mkono tabia ya wanasiasa, hasa katika CHADEMA kutangaza katika muda huu kugombea urais, siwaoni wanasiasa hao kama wanakikosea chama chao kufanya hivyo. Aidha, siwaungi mkono kabisa wale wote wanaompinga Zitto Kabwe kutangaza kuutaka urais katika kipindi hiki.
  Siyaungi mkono makundi haya kwa sababu nadhani kwamba yanaenda kinyume cha utamaduni wa kisiasa tunaojaribu kuujenga ndani ya CHADEMA. Kimsingi, makundi yote mawili, Zitto na wapinzani wa tabia zake, wanaendekeza unafsi, jambo ambalo CHADEMA wanajaribu kulikomesha katika siasa za Tanzania. Nitaeleza baadaye maana ya dhana hii.
  Wanasiasa wa aina ya Zitto Kabwe ni waathirika wa mfumo uchwara wa uliberali ambao tumeamua kuufuata kimya kimya bila hata kuuelewa vizuri.
  Aidha, hamaki na upinzani dhidi ya kutangaza kugombea urais inadhihirisha jinsi ambavyo wengi wetu hatujaielewa vizuri dhana ya uongozi katika mfumo tulio nao wa uliberali uchwara. Tunataka tutende kijamaa wakati tunaishi kiliberali. Katika mfumo wa ujamaa tuliojaribu kuujenga baada ya uhuru, suala la uongozi lilikuwa si suala la mtu binafsi.
  Uongozi ulikuwa ni jukumu la wanataasisi kuamua nani anafaa katika nafasi gani. Hivi ndivyo Rashidi Kawawa alivyoweza kuacha cheo cha uwaziri mkuu kwa kumpisha Edward Moringe Sokoine na yeye kuchukua nafasi ya Waziri wa Ulinzi.
  Hii ni kwa sababu enzi hizo waliokuwa wanaamua nani ashike nafasi gani ni chama na si mtu kujichagulia nafasi ya uongozi. Katika enzi za ujamaa wetu wa kitanzania, kiongozi mwenye cheo kikubwa na kidogo wote walikuwa ni viongozi wanaoheshimika na kuheshimiana; na ndio maana wote waliitwa ‘ndugu’, sawa na wananchi wenzao ambao hawakuwa viongozi.
  Utaratibu huu tumeuua baada ya kuanza mfumo wa vyama vingi na kuamua kuufuata mfumo wa kiliberali bila kuuelewa sawa sawa misingi yake. Katika mfumo wa kiliberali uchwara inaelekea haikubaliki kwa mtu aliyewahi kuwa waziri mkuu arudi kuwa waziri wa kawaida. Katika mfumo wa kiliberali, ngazi moja ya uongozi huzalisha ngazi nyingine ya juu zaidi, na ukishaenda huko hurudi chini bali unahakikisha unaendelea kwenda juu zaidi. Kwa hiyo, ukizingatia mantinki hii ya uliberali uchwara, huwezi kumshangaa Zitto kwa kuutaka urais na kusema kwamba yeye sasa ubunge basi; anataka kwenda juu zaidi na pengine ubunge sio saizi yake!
  Kwa hiyo, Zitto Kabwe ameonyesha unafsi ambao ni tabia ya kawaida katika uliberali, hususani huu uliberali uchwara tunaofuata sisi. Mfumo huu una tabia ya kuzalisha viongozi wenye matamanio na utashi binafsi. Katika mfumo huu uongozi ni biashara. Ili uwe kiongozi katika mfumo wa kiliberali lazima uonyesha matamanio na utashi, na ujiuze vya kutosha kabisa. Kwa hiyo kutangaza nia na kujimwagia sifa juu ya uwezo ulio nao katika nafasi fulani ni sehemu kabisa ya mfumo wa kutafuta uongozi katika mfumo wa kiliberali.
  Uongozi katika mfumo wa kiliberali ni juu ya mtu na wala sio juu ya taasisi. Anayepata uongozi katika mfumo huu ni yule mwenye uwezo wa kutengeneza mtandao wa wafuasi ambao atahakikisha anakuwa nao kwa kipindi chote hadi uchaguzi utakapofanyika.
  Mkakati mwafaka wa kutafuta uongozi katika mfumo wa kiliberali unaambiwa ni kufanya maandalizi mapema. Huu ndio utamaduni ambao CCM imeuasisi kuanzia mwaka 1995 na ambao mtu alitarajia CHADEMA wangeukwepa.
  Hata hivyo, sioni kwamba kitendo cha Zitto Kabwe kutangaza kuutaka urais kama ni kosa kwa sababu CHADEMA haijaweka rasmi utaratibu wa kuukataa utamaduni huu. Kwa kuwa utamaduni huu haujakataliwa rasmi kimfumo, haiwezi ikawa kosa mtu moja moja kuchagua kuutumia. Ndio maana Mzee Mtei kawataja watu wengine kadhaa, akiwamo yeye, kwamba nao wanaoutaka urais lakini hawajatangaza nia bado kwa hoja eti muda wa kufanya hivyo bado, kama vile ndani ya CHADEMA kuna muda rasmi uliowekwa wa kutangaza nia ya kugombea.
  Ni wazi basi kwamba hata wale wanaompinga na kumzomea Zitto Kabwe kuutaka urais wanaonyesha unafsi. Hawafanyi vile kwa sababu wana misingi fulani wanayoiamini juu ya namna ya kupata uongozi, la hasha. Hawa wanafanya hivyo kwa sababu ya aina ya pili ya unafsi, ambayo ni fitina.
  Hawa wanajaribu kuonyesha kwamba Zitto Kabwe kafanya kosa kubwa kutangaza kugombea urais, lakini hawasemi ni kosa gani na amevunja kanuni gani ndani ya chama. Wengine wameenda mbali zaidi na kumuona Zitto kama ni msaliti ambaye amenunuliwa ili kukidhoofisha CHADEMA.
  Hii ni fitina na ni aina mbaya kabisa ya unafsi na tabia inayojitokeza vile vile katika uliberali uchwara. Nina wasiwasi kwamba watu wanaompinga Zitto kwamba nao labda wana watu wanaodhani wanafaa kuwa marais na wanajaribu kumchonganisha Zitto na jamii, ili hatimaye njia yao ya kuusaka urais iwe nyeupe huko mbele.
  Katika mfumo wa kidemokrasia za kiliberali kutangaza kugombea urais hakupaswi kuleta mzozo wala vurugu katika chama. Wakati mwingine kitendo cha Zitto ni jibu kwa wapinzani wa CHADEMA aina ya Samuel Sitta wanaojaribu kujenga taswira ya hovyo kwamba ndani ya CHADEMA hakuna wenye uwezo wa urais zaidi ya Dk. Slaa aliyegombea kwa mafanikio mwaka 2010.
  Kwa hiyo, wakati huu ambapo CHADEMA haina mwongozo elekezi juu ya namna ya ‘kuutaka’ urais, kutangaza kuutaka urais mapema ndio demokrasia yenyewe . Kwa hiyo tunapaswa kuwatia moyo wanachama wengine wenye matamanio ya urais watangaze wakati wowote na mahala popote wanapojisikia, wakati tukiweka misingi murua ya namna ya kupata mgombea mwafaka kwa wakati husika kutoka kwenye kundi la hao wanaojitangaza au wengine.

Loading...