DR Kitila
Kutokea kwenye post yako ambayo si sehemu ya chapisho la kwenye raia mwema.
Nakubaliana na wewe juu ya hoja ya kuchochea Fikra huru, lakini lazima kuwe na utaratibu basi, ama sivyo inakuwa ni Fujo. Nikigusia swala la Zitto kidogo, mpaka sasa hakuna shaka kwamba angalau si CHADEMA wala CCM mwenye uhakika wa kuibuka mshindi mwaka 2015, na mpaka sasa hakuna mwenye uhakika ni nini kitakua kigezo cha ushindi mwaka 2015 kati ya ushawishi wa mgombea au ushawishi wa CHAMA.
Lakini mpaka sasa inaeleweka kwamba CCM imekuwa ikishinda chaguzi nyingi kutokana na jina lake zaidi kulinganisha na nguvu ya ushawishi ya wagombea wake, mategemeo yetu ni kuona viongozi wa chadema wanaelekeza nguvu zao zote kwenye kukijenga chama chao. inapotokea mtu kama ZITTO anatangaza mawazo yake ya kutaka urais katikati ya mchakato kama huu inalazimisha kuhoji "what kind of character is this?". Mtake msitake, kuzipachika sifa ya fikra huru tabia kama hizi ni sawa sawa na kuwafundisha watoto kumuinterapt mzazi au mtu mzima anapokuwa akiongea.
Ndio maana ya kuwa na kanuni,taratibu, sheria, miongozo na viongozi, ili tuweze kuendesha mambo yetu kwa utaratibu na staha ama sivyo hata kama mtu atajamba wakati watu tunakula pia liwe ni jambo lisilostahili kuuliza, NANI HUYO???