Dk. Kawambwa, umeshindwa nini kuvunja mkataba wa TRL? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Kawambwa, umeshindwa nini kuvunja mkataba wa TRL?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magezi, Nov 5, 2009.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Watanzania bado tuna machungu ya Chenge kutuibia vijisenti na akaviwekeza ughaibuni. Kumbe mdudu huyu huyu ndiye ali-sign mkataba baina ya serikali na Rites wakati huo akiwa waziri wa miundo mbinu, tena akijigamba kuwa alikuwa makini.....sasa madudu yake tunayaona.

  Sasa tatizo langu ni kwa nini Kawambwa ana kigugumizi kuhusu kuvunja mkataba na wahindi hawa?? Kawambwa wewe ni Mechanical engineer lakini nashangaa unashundwa kuelewa kuwa wahindi wanataka kuitumia TRL kukuza shirika lao la reli (Rites). Wahindi wana kiwanda sasa hivi cha kutengeneza mabehewa, engines (japo siyo nzuri) sasa wanataka wavuruge mifumo yote ya kiufundi ili tuanze kuwategemea wao ktk kila kitu. Na wahindi na dharau zao wakisha hakikisha unawategemea, basi cha moto utakiona.

  Kama mafundi wameweza kutengeneza engines zetu za zamani na kuweza kuzitumia kufanya kazi wakati wahindi walishasema hazifai na wakaleta za kwao kuikodisha TRL, kawambwa huoni kwamba huo ni ujanja wanautumia?? Unashindwa nini kuvunja mkataba?? Hata kama ni kulipa fidia, mbona tulikuwa tunawalipa na bado tunawalipa IPTL??

  Tafadhali kawambwa unadhalilisha uhandisi wako......kama umeshindwa si ujiuzuru??....au na wewe uko kama Hosea anayesema hawezikuacha kitumbua chake hata kama anavunja sheria??
   
 2. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Haya yalipokuwa yakifanyika Dr. Eng. S. Kawambwa alishirikishwa? Au pakitokea matatizo ndiyo tuwasukumie wengine
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  yeye kwa sasa ndo waziri mwenye dhamana ya wizara husika lazima achukue hatua......unataka kuniambia mkeo akifanya maamuzi mabaya ya kuigharimu familia wakati huo haupo uko masomoni mfano ukirudi utasema ah....acha tu mpate shida??
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,312
  Likes Received: 1,783
  Trophy Points: 280
  Kuvunja mkataba ni kitu ambacho kinahitaji wide consultations. Eng Kawambwa peke yake shughuli hiyo itakuwa kubwa sana kwake. Ninachoweza kuona ni pengine kufanya initiative za kupata input toka kwa wahusika mbalimbali mpaka ushauri wa kisheria ili aweze kuuvunja mkataba.
  Mheshimiwa anaongoza wizara yenye mambo mengi tena mazito sana. Kama yuko vile alivyokuwa ile iliyoitwa IPI enzi zile basi siasa hizi zenye verse za taarabu sidhani kama anaziweza.
  Ila naamini bado ni mtu muungwana ambaye kutokana na kujifunza kwa makosa ya hapa na pale atakuwa kiongozi mzuri siku za usoni.Asijaribu tu kujiingiza kwenye mambo waliyofanya watangulizi wake ya kusaini kila document inayokuja mezani bila kujari hatima yake.
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Pamoja na yeye kuwa waziri lazima taratibu zifuatwe katika kuvunja mikataba na upate ushauri wa kutosha! Yeye ni Mhandisi huenda hajui lolote kuhusu mikataba ambayo wahusika ni wanasheria! Na je umefuatilia na kuona kuwa halifanyii kazi au ndo kukimbilia tu kwenye JF na kuanza kutoa Lawama?
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,070
  Likes Received: 5,553
  Trophy Points: 280
  Ujajua tu mpwa kwa nini ataki??

  10% kila mwezi wana mishara yao hao kila kampuni walioingia mikataba
   
Loading...