Kwa wewe mleta hoja na wengine lipo tatizo la wasomi wa kitanzania kudhani kuwa vyeti vyao ndo utumishi wao, hapana. Wanapaswa waende kwa wananchi ili wakawahoji kama kweli wanadhamira ya kuwaletea maendeleo watanzania. Mfano wa kuigwa ni wa prof.muhongo, prof.tibaijuka, dr.mahiga hawa wameonyesha dhamira ya kuwatumikia watanzania na wameomba ridhaa zao.
Leo huyo ndalichako hapo makongo juu anapoishi hata majirani hawamjui, sio hata mjumbe wa kata wa chama tutampaje wajibu wa kuwatumikia watanzania kwa kigezo kipi kitumike. hebu niambie alichukua form ya ubunge japo kura za maoni hazikutosha kama dr.mahiga? hapana. ajira aliyonayo hapo UDSM inamtosha labda awe head of faculty.