Dk Hoseah akiri Takukuru ‘kunuka’ rushwa

Dk Hoseah akiri Takukuru ‘kunuka’ rushwa

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,283
dk+hosea.jpg

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, Dk Edward Hosea.
Na Anthony Kayanda, Mwananchi

Posted Jumatano,Februari11 2015 saa 17:39 PM
Kwa ufupi
Dk Hoseah alisema wanapokea utafiti huo kama changamoto na watatumia sheria, kanuni na taratibu kuwapa adhabu watumishi watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Kigoma. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imekiri kuwapo kwa baadhi ya watumishi wake wanaojihusisha na vitendo vya kupokea rushwa, hivyo kuchafua sifa ya taasisi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma jana, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alisema tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na taasisi zilizofanya utafiti juu ya masuala ya rushwa nchini, baadhi yake zina ukweli.

Dk Hoseah alisema wanapokea utafiti huo kama changamoto na watatumia sheria, kanuni na taratibu kuwapa adhabu watumishi watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa.

"Takukuru siyo malaika, iwapo nitasema hakuna kabisa rushwa ndani ya taasisi hii nitakuwa ninajidanganya kwani hili tatizo lipo sehemu zote, inawezekana maofisa wasio waadilifu wanapokea rushwa lakini ninawahakikishia kwamba tutachukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika," alisema Dk Hoseah na kuongeza:

"Serikali imefanya jitihada kubwa kuhakikisha Takukuru inaboreshwa, ndiyo maana bado sielewi kwanini kuna baadhi ya watumishi wanalalamikiwa kujihusisha na ulaji rushwa, wanalipwa vizuri na kuna mazingira mazuri ya kufanya kazi. Nitafanya jitihada kuondoa changamoto hizi."


Pia, alitoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini na matapeli wanaojitangaza kwamba wao ni maofisa wa Takukuru, hivyo kuomba rushwa kwa baadhi ya maofisa wa Serikali na watu wengine ambao wanabainika kufanya makosa yanayohusiana na ubadhirifu mbalimbali.

Dk Hoseah alisema ili kupambana na rushwa lazima Serikali iwe na uongozi bora na imara,
ambao utasaidia kuweka mipango thabiti kwa maendeleo ya wananchi, kufanya mambo kwa uwazi, kuwajibika kwa umma, kuwashirikisha watu katika mipango mbalimbali na kusimamia utawala wa kisheria.

CC: Tized, Mr Rocky, Fixed Point, lyinga, NATA, Chakaza, Elly B, Ablessed, MziziMkavu, afrodenzi, Heaven on Earth, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Dingswayo, MANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, JokaKuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, Honolulu, August, dyuteromaikota, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto, Daudi Mchambuzi Kill 3




 
...labda na Kikwete atakubali hivi karibuni kwamba Ikulu yake inanuka rushwa na inaongoza kwa kupokea rushwa kuliko taasisi yoyote ile nchini.
 
mtu aliyejiuzia nyumba ya Takukuru msasani kwa bei ya karibu na bure leo mnategemea apambane na rushwa
hii ni sawa na kusubiria kuona jinsi nzi atakavyomuua tembo ni jambo lisilowezekana na yeye mwenyewe alishasema kuwa kwa sheria na utaratibu zilizopo haiwezekani kupambana na rushwa amebakia kupalilia mkate wake wa siagi na wanawe.
 
Kuna mahali kafunguka....Kasema uongozi wa nchi kwa sasa ni mbovu ndio maana mapambano na rushwa ni magumu. .....
 
This Hosea is a real daft. what is he doing in office then?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tukisema tnaaambiwa Wazushi, wanafiki, tuna uchu wa Madaraka, tunataka Nchi isitawalike, na kadhia zote za kijinga na za kitoto, sasa na huyu aliesema Leo hii kwa kinywa chake mwenyewe tumuiteje?? Pumbavu kabisa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
mtu aliyejiuzia nyumba ya Takukuru msasani kwa bei ya karibu na bure leo mnategemea apambane na rushwa
hii ni sawa na kusubiria kuona jinsi nzi atakavyomuua tembo ni jambo lisilowezekana na yeye mwenyewe alishasema kuwa kwa sheria na utaratibu zilizopo haiwezekani kupambana na rushwa amebakia kupalilia mkate wake wa siagi na wanawe.

Na mzito mmoja wa PCCB aliyepewa sh millioni 30 na Benki Kuu ya Tanzania wakati wa kashfa ya EPA je? Muda umefika wa kuonyesha alivyopokea na aliyempelekea. Hii ndo itakuwa funga kazi ya rushwa nchini.
 
Li mtu lizima unaweza kudhani lina akili kichwani kumbe hovyo kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
I could see that coming .................... ANTI-CORRUPTION CORRUPTION!!
 
Tuanze na maadili kwenye familia zetu
Twende kwenye jumuiya zetu
Ngazi zote za msingi iwe na mipango kuhusu malezi mazuri ya vijana wetu
Sheria iwe bora na tukelezaji wa uhakika siyo bla blah
 
iwapo nitasema hakuna kabisa rushwa ndani ya taasisi hii nitakuwa ninajidanganya kwani hili tatizo lipo sehemu zote, inawezekana maofisa wasio waadilifu wanapokea rushwa lakini ninawahakikishia kwamba tutachukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika," alisema Dk Hoseah[/QUOTE]

Well said Dr Hoseah. Hata ningekuwa mimi ningesema hivyo na sio kukimbilia kukanusha totally. Cha msingi ni kusafisha nyumba yako kwakuwa jirani ameona uchafu ambao wewe ulikuwa hujauona.
 
Na Bado yuko OFISINI.. Hii taasisi ni kiini macho tu maana meno yake bado hayajaota.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hii taasisi bora isepe tu kazi iendelee kufanywa na polisi kimagumashi hivyo hivyo kuliko kuwa taasisi yenye wafanyakazi kibao ambao kazi yao ni hiyo hiyo alafu mwisho wa siku mambo yale yale. Bora hata wapewe hiyo kazi polisi wasipofanya twatasikingizia wapo busy na mambo mengine ya kiusalama

Kama viongozi wa serikali hawaipi support bora waivunje tu sasa
 
hivi first appointment wa hii taasisi huwa wanalipwa kiasi gani wakuu?
 
Tuanze na maadili kwenye familia zetu
Twende kwenye jumuiya zetu
Ngazi zote za msingi iwe na mipango kuhusu malezi mazuri ya vijana wetu
Sheria iwe bora na tukelezaji wa uhakika siyo bla blah
Mkuu umenena japokuwa wakati mwingine yote hayo huwa yanategemeana hasa kipindi hiki ambacho tumeosa mwelekeo kiasi kwamba hata mtoto mdogo anasikia kelele kuhusu ufisadi sehemu mbalimbali
 
Hii taasisi bora isepe tu kazi iendelee kufanywa na polisi kimagumashi hivyo hivyo kuliko kuwa taasisi yenye wafanyakazi kibao ambao kazi yao ni hiyo hiyo alafu mwisho wa siku mambo yale yale. Bora hata wapewe hiyo kazi polisi wasipofanya twatasikingizia wapo busy na mambo mengine ya kiusalama

Kama viongozi wa serikali hawaipi support bora waivunje tu sasa
You don't know what you are talking about!
 
Mkuu BAK na bado jamaa anakula mshahara wa nguvu wakati taasisi ya kupambana na rushwa inapokea rushwa naona tuuiite taasisi ya kupokea na kutakatisha rushwa
 
Last edited by a moderator:
You don't know what you are talking about!
Naelewa nachozungumza kwa kuwa tatizo si la TAKUKURU kama TAKUKURU kwani tumeunda taasisi kwa maana ya kupambana na kuzuia rushwa lakini wahusika ambao ni serikali wanachukulia poa tu kuwa support hawa jamaa kiasi kwamba mtu kiongozi kabisa anatamka hadharani 'hawa mafisadi wana nguvu na mtandao mkubwa ni kwenda nao kwa tahadhari', unategemea nini sasa hapa kwa Hosea na timu yake. Wangepewa menu na nguvu na kuweka siasa pembeni wangefanya kazi lakini hawapewi
 
Back
Top Bottom