Dk Bashiru: Vyama vya upinzani vitakufa kimoja baada ya kingine

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1574852532603.png

Katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema vyama vya upinzani nchini Tanzania vitaendelea kufa kimoja baada ya kingine kwa kuwa vinashindwa kufanya siasa vikubalike kwa wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Novemba 27, 2019 wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema baadhi ya vyama hivyo huibuka wakati wa uchaguzi jambo linalovifanya vishindwe kukubalika.

Amesema kwa msingi huo, CCM kitaendelea kuimarika zaidi, akibainisha kuwa udhaifu wa vyama vingi vya upinzani ni kukosa watu sahihi wa kuviongoza.

“Adui wa vyama vya upinzani yupo ndani mwao wenyewe wasitafute mchawi lazima wakubali kubadilika,” amesema Dk Bashiru.


Source: Mwananchi
 
Kuuwa vyama vya upinzani ni rahisi sana,hata dakika hii wakiamua wanaweza wakatangaza hadharani "KUANZIA SASA TUMEFUTA VYAMA VYOTE VYA UPINZANI" au hata sio kutanganza wanaweza wakavinyima ruzuku,mishahara kwa Wabunge wa upinzani,au kupiga marufuku uwepo wa bungeni.

Ila kamwe hawataweza kuuwa upinzani,vyama vitakufa ila upinzani hautakufa kamwe
 
Kama anaamini kuwa Watauwa Upinzani, anapoteza muda kabisa. Kama hiyo Kauli yake Ingekuwa sawa, basi tulitaraji Uchaguzi huu wa SM ndiyo ungekuja Kuwa Kipimo bora. Kiuhalisia, CCM haipendwi na Kazi iliyopo ni Kulazimisha tu Kupitia Majeshi ya Nchi!

Kama wanajiona Wapo Strong kwanini Watumie Majeshi? Usomi wa wapumbavu saana wa wakina Bashiru hawa.
 
beth,

Kama kufa hivi vyama vingekufa ndani ya miaka minne hii, kwa mbinyo mliowapa kwa kushirikiana na policcm tayari vingekuwa historia lakini ajabu ilipofika wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa mmeviogopa.

Wekeni tume huru uchaguzi huru tuone hayo majisifu yenu kwa vitendo kama kweli mnakubalika kwa wananchi.
 
Tangu siku vilizaliwa vikiwa havina; Ofisi, mapato na hata experience ya siasa tulijua havifiki jioni ya pili. Ila sasa, tangu 1995 tumeviona vikisimama wima ka kucha wala havija tetereka. Mawazo ya Bashiru ni ya mgando sana. Afanye tafiti kwanza. Hata G55 walikuwa CCM na bado wakajipinga
 
Wanajua wanachokifanya ,yote ili ni kulinda viti na matumbo yao ila siku itawauma sana kwa kukosa kutenda haki.
 
Wenyewe wenye ccm yao wamesha hamua 20/20 wana mrudishia haki yake membe wame mshitukia huyu zimwi asije kuwala Nyama hawamtaki abadani ndoo maana taharuki imetandaa uko ATTACH=full]1274339[/ATTACH]
 
Back
Top Bottom