Dk Bashiru atangaza kumng’oa Lwakatare Bukoba mjini 2020

Kipapatiro

JF-Expert Member
May 18, 2017
1,129
1,497
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amewataka wanachama wa chama hicho kumuunga mkono Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare, lakini akipania kumng'oa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza na baadhi ya wanachama na viongozi nje ya ofisi za CCM Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba, leo Desemba 22, 2018 Dk Bashiru ametaja sababu za kuunga mkono kuwa ni mbunge halali, muungwana na hapotoshi wananchi.

Hata hivyo, pamoja na sifa hizo amesema mbunge huyo ajiandae kung'oka mwaka 2020.

Mapokezi ya Dk Bashiru mjini hapa yalianzia uwanja wa ndege wa Bukoba ambapo yaliongozwa na waendesha pikipiki.

Katibu mkuu huyo wa chama tawala amesema amekuja nyumbani kwa ajili ya mapumziko ya mwishoni mwa mwaka yatakayokwenda sambamba na ziara hadi Januari 2, 2019 kwa kutembelea wilaya mbalimbali za mkoa huu.

Pia, ameagiza kabla ya kuondoka mkoani Kagera apatiwe maelezo ya sababu ya kufa kwa kilimo cha zao la chai alilodai lilikuwa mkombozi kwa wananchi ambao walifanikiwa kujiongezea kipato na kusomesha watoto.

Dk Bashiru amesisitiza kuwa Taifa lina uwezo wa kujitegemea huku akitaja baadhi ya chanyamoto zilizopo kama ukosefu wa ajira na kuagiza wakuu wa mikoa nchini kutatua kero za wananchi pamoja na kuondoa uonevu kwa wafanyabiashara wadogo.

Vilevile amerejea kauli yake kuwa CCM siyo chama cha matajiri, bali wakulima na wafanyakazi ambapo baadaye ameelekea nyumbani kwake Bukoba Vijiiini.
 
Jamaa alikuwa vizuri sana kichwani.. Huko sisiemu sio salama kabisa aisee.. Watu na usomi wao wanaacha akili walikotoka, wanapandikizwa utumbo ndani ya sisiemu.. So sad aisee..
 
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amewataka wanachama wa chama hicho kumuunga mkono Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare, lakini akipania kumng'oa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza na baadhi ya wanachama na viongozi nje ya ofisi za CCM Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba, leo Desemba 22, 2018 Dk Bashiru ametaja sababu za kuunga mkono kuwa ni mbunge halali, muungwana na hapotoshi wananchi.

Hata hivyo, pamoja na sifa hizo amesema mbunge huyo ajiandae kung'oka mwaka 2020.

Mapokezi ya Dk Bashiru mjini hapa yalianzia uwanja wa ndege wa Bukoba ambapo yaliongozwa na waendesha pikipiki.

Katibu mkuu huyo wa chama tawala amesema amekuja nyumbani kwa ajili ya mapumziko ya mwishoni mwa mwaka yatakayokwenda sambamba na ziara hadi Januari 2, 2019 kwa kutembelea wilaya mbalimbali za mkoa huu.

Pia, ameagiza kabla ya kuondoka mkoani Kagera apatiwe maelezo ya sababu ya kufa kwa kilimo cha zao la chai alilodai lilikuwa mkombozi kwa wananchi ambao walifanikiwa kujiongezea kipato na kusomesha watoto.

Dk Bashiru amesisitiza kuwa Taifa lina uwezo wa kujitegemea huku akitaja baadhi ya chanyamoto zilizopo kama ukosefu wa ajira na kuagiza wakuu wa mikoa nchini kutatua kero za wananchi pamoja na kuondoa uonevu kwa wafanyabiashara wadogo.

Vilevile amerejea kauli yake kuwa CCM siyo chama cha matajiri, bali wakulima na wafanyakazi ambapo baadaye ameelekea nyumbani kwake Bukoba Vijiiini.
Taifa la wajinga
 
Back
Top Bottom