Dk. Bana awajia juu CHADEMA/CUF kuhusu M4C & V4C

huyu mzee Bana anazeeka vibaya..bila shaka anatamani mtabiri maarufu angekuwepo ili wasaidiane kufanya study inayopendelea magamba...mawazo ya Bana hayana tija
 


Ndiye huyu hapa, picha yake haitofautiani sana na maneno yake!


Asante Mkuu kwa hii picha, Jinsi jamaa alivyo na sura ya hovyo kama meno na maneno yake, itabidi ni i print ili watoto wangu wakianzia kulia niwatishie kwa picha ili wanyamaze.
 
Kwa hiyo ana kubaliana na kauli mbiu ya ccmweli ya kuwakandamiza wapinzani kwa kutumia polisi?
 
Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu 2010 ni takribani miaka 2 lakini serikali ya ccm haijatekeleza japo asilimia 10% ya ahadi zake. M4C ya Chadema na hiyo V4C ya cuf hazijaizuia ccm kutekeleza ahadi zake. Vyama vya siasa vitafanya kazi zao sambamba na serikali ikitekeleza mipango yake. Kama wameshindwa majukumu yao wasitafute kisingizio cha M4C ama V4C.
Kama vipi ccm na serikali yake waanzishe Manifesto 4 Completion.
 
 

Huyu kada bado ana matumaini ya kupewa ukuu wa wilaya maana ana kera mno
 
na kutotekeleza hizo ahadi kwa kasi inayostahili kunakipa CDM kazi ya kuwafafanulia wananchi hayo na hiyo ndio siasa, na ndio maana CCM hawataki hilo kwa kuwa udhaifu wao unazidi kuwekwa hadharani!
 
Huyo nae ni wa kumouuza tu, tunapo hangaika nae anajiona na ni mtu wa maana sana kaytika siasa za tanzania,
 
 
Orijino komedi was session yao inaitwa LE PROFESSERI huyu mzee naona anasadifu mazingira hayo.
 
 

Yaani Tendwa ndio alitaka CHADEMA wakae chini kumsikiliza huyo Benson Bana? Huyu Benson Bana anakiri hajui ni kwanini uchumi wa Tanzania ni mbovu, wakati huo huo anasema wananchi wana matatizo mengi. Yote tisa, kumi, Benson Bana amenukuliwa akisema hajui CHADEMA wanataka nini?

Ah hebu nipate supu yangu maana vituko vya Benson Bana ni vingi mno. Hivi REDET yake imefikia wapi, I know wafadhlili walijitoa baada ya kuona ujuha wake.
 
Watu wa CCM wana tabu sana, wakati wa kampeni wanaviita vyama vya msimu i.e siasa zao wakati wa kampeni tu, leo wanawasha moto kila siku, wanalalamika sio wakati wake... Damned if you do, damned if you don't.
 
Kwani harakati za wapinzani zinawazuia nini Magamba kutekeleza ilani za Chama chao?? huyu naye mwehu....Alitaka hatakati ziwe wakati wa Kampeni?? Kilaza msomi - The Proffesori
 
Hii inadhihirisha wazi jinsi tunaowaita kuwa wasomi wa nchi hii wasivyokuwa na umuhimu katika mabadiriko ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. CCM ndio wanaongoza dola, ndiyo yenye bajeti ya kufanya maendeleo kwa wananchi. Vyama vya upinzani kazi yake ni kuangalia makosa ya chama tawala na kuyatumia kuwaeleza wananchi ili chama tawala kichukiwe hivyo kutoa fursa kwa vyama vingine kushika dora kama wananchi wataona inafaa kufanya hivyo. Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugezi mbona wanafanya kazi za ukada wa CCM, mbona huyo Banana hajasema chochote? Cuf na Chadema kujiimarisha kwa kuwaambia wananchi ukweli na madudu yanayofanywa na ccm kunakosa gani? Kujiimarisha kwa kufungua matawi na kutafuta wanachama kuna kosa gani? Hilo linawazuia nini ccm kutekeleza sera au kuwatumikia wananchi? Huwezi kuamini kama ni msomi ndio katoa hoja yenye kupwaya kama hii.
 
mh!!!!!!!!!!,ukitaka upoteze hadhi kwenye mijadala km hii ijadili cdm vibaya!,sasa uko c kulazimishana kufikiri sawa!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…