Elections 2010 Diwani wa CHADEMA (na member wa JF) atekwa Igunga

CCM mnataka na sisi tuanze kazi ya utekaji? Mnaona sasa hasara za kuhalalisha silaha hata kwa majambazi? Kwa kitendo hiki sasa nashawishika kusema CCM ni CHAMA CHA MAJAMBAZI.BAAAAAAS!!!!!!!!!
 
Diwani wa CDM Ndg Nanyaro Ephata alitekwa yeye na mwenzake mmoja aitwaye Boniface na kupelekwa kusikojulikana. Wakiwa njiani kurudi hotelini ghafla walivamiwa na watu ambao walikuwa katika Toyota Landcruiser S/W T 203 BKW na kutekwa.

Huo ulikuwa ni usiku wa saa saba ambapo walikuwa wamemaliza kikao chao na kwenda kupaki magari mbali kidogo na hoteli waliyofikia ambayo haina parking. Wakiwa ndani ya gari, waliambiwa kuwa wasali sala zao za mwisho kwani kiherehere chao ndicho kilichowaponza! Baada ya kusikia hivyo Nanyaro ambae ni diwani wa Chadema Arusha kata ya Revolosi alijipanga ama afe yeye au wao nao wafe, hivyo alimrukia dereva na kuanza kung'an'gania steringi ili gari lipoteze mwelekeo. Kuona balaa limeanza jamaa mmoja alikimbia katika hao watekaji na kubaki watatu.

Dereva alipoona anashindwa kulimudu gari alimpa kipigo Nanyaro na kumsukuma nje ya gari yeye na mwenzake na kuondoka kwa kasi. Huo ulikuwa ni usiku na porini, kibaya zaidi katika purukushani ile jamaa walidondosha simu katika gari lile. Wakajitahidi kufika mjini na kupata msaada toka kwa viongozi wa CDM na kwenda kulipoti tukio hilo polisi ambapo walipofika walikuta tayari wameshafunguliwa kesi na wale jamaa kuwa walitaka kuwateka hao jamaa na wao walifanikiwa kuwadhibiti na kuwapora simu! Basi ikabidi nao watoe maelezo ambayo yalipelekea kurudishiwa simu zao!

Angalizo langu, tabia hii ya utekaji watu naona imeanza kushamiri, tabia hii ni mbaya na inapaswa kukomeshwa mara moja.

Craaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap hakuna kitu hapa !
 
Haya mambo haya sasa naanza kutoyaamini!!
Crashwise, hiyo story yako ina matundu mengi sana.

1)akamrukia dereve...........washirika wa dereva wakakimbia, je gari ilikuwa imesimama au inatembea? na ni station wagon, right?
2) dereva aliyepewa roba au ambaye anapambana na mtu aliyeng'ang'ania steering wheel huku gari ikitembea, aliwezaje kumpa kipigo Ephata, na kumtupa nje ya gari?? na huyo mwenzake Ephata alikuwa anafanya nini??

hizi story zinaanza kuniudhi sasa!!

santeee
 
Craaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap hakuna kitu hapa !

hizi taarifa hata polisi wanazo sasa sijui ni crap kwenye masaburi yako..cha msingi Magamba acheni mchezo mchafu maana tutakapo anza na sisi sijui kama tutaishi kwa utulivu tena nchi hii..
 
Eti kweli mambo kama haya ya kihuni ya kutekana sasa yanaelekea kuwa SEHEMU KAMILI YA UTAMADUNI WETU kwa kuwa tu wao CCM wamependezewa nazo. Jamani tunakwenda wapi kama taifa na hizi siasa UCHWARA?????????????????
 
Tunaelekea wapi huko? Tumeanza kutekana tena? Hizi sasa ndizo Siasa Uchwara. Mbona hapa kila mtu anadai katekwa? Mwenye gari anasema alitaka kutekwa na akawazidi nguvu na kuwanyang'anya simu na mwenye simu anasema alitekwa na kujiokoa ila simu zikabaki kwenye gari!!! Tunaishi kimjinimjini na ukitaka kumchinja kobe basi fanya timing!! Hapa naona ni timing tu inacheza.
 
Siri ipo kwenye ulinzi wa kura mpaka zitakapohesabiwa na kutangazwa mbele ya hadhara.

Tuige mtindo wa watu wa Mara kutoondoka kituoni zaidi tu ya kupiga hatua kumi nyuma. Jiulize unapoondoka kutuoni kura zako huwa unamwachia nani akulindie wakati tume, polisi na vyombo vingine vyote ni vya CCM.

Ulinzi na usalama wa kura ni haki ya msingi ya wapiga kura popote pale!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom