Elections 2010 Diwani wa CHADEMA (na member wa JF) atekwa Igunga

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,177
3,326
Diwani wa CDM Ndg Nanyaro Ephata alitekwa yeye na mwenzake mmoja aitwaye Boniface na kupelekwa kusikojulikana. Wakiwa njiani kurudi hotelini ghafla walivamiwa na watu ambao walikuwa katika Toyota Landcruiser S/W T 203 BKW na kutekwa.

Huo ulikuwa ni usiku wa saa saba ambapo walikuwa wamemaliza kikao chao na kwenda kupaki magari mbali kidogo na hoteli waliyofikia ambayo haina parking. Wakiwa ndani ya gari, waliambiwa kuwa wasali sala zao za mwisho kwani kiherehere chao ndicho kilichowaponza! Baada ya kusikia hivyo Nanyaro ambae ni diwani wa Chadema Arusha kata ya Revolosi alijipanga ama afe yeye au wao nao wafe, hivyo alimrukia dereva na kuanza kung'an'gania steringi ili gari lipoteze mwelekeo. Kuona balaa limeanza jamaa mmoja alikimbia katika hao watekaji na kubaki watatu.

Dereva alipoona anashindwa kulimudu gari alimpa kipigo Nanyaro na kumsukuma nje ya gari yeye na mwenzake na kuondoka kwa kasi. Huo ulikuwa ni usiku na porini, kibaya zaidi katika purukushani ile jamaa walidondosha simu katika gari lile. Wakajitahidi kufika mjini na kupata msaada toka kwa viongozi wa CDM na kwenda kulipoti tukio hilo polisi ambapo walipofika walikuta tayari wameshafunguliwa kesi na wale jamaa kuwa walitaka kuwateka hao jamaa na wao walifanikiwa kuwadhibiti na kuwapora simu! Basi ikabidi nao watoe maelezo ambayo yalipelekea kurudishiwa simu zao!

Angalizo langu, tabia hii ya utekaji watu naona imeanza kushamiri, tabia hii ni mbaya na inapaswa kukomeshwa mara moja.
 
Joss

JF-Expert Member
May 28, 2009
759
176
Siasa za kistaarabu walizo zitaka akina Beno Malisa, January ,na Bashe ziko wapi?
 
Bigirita

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
15,866
7,161
Haya mambo haya sasa naanza kutoyaamini!!
Crashwise, hiyo story yako ina matundu mengi sana.

1)akamrukia dereve...........washirika wa dereva wakakimbia, je gari ilikuwa imesimama au inatembea? na ni station wagon, right?
2) dereva aliyepewa roba au ambaye anapambana na mtu aliyeng'ang'ania steering wheel huku gari ikitembea, aliwezaje kumpa kipigo Ephata, na kumtupa nje ya gari?? na huyo mwenzake Ephata alikuwa anafanya nini??

hizi story zinaanza kuniudhi sasa!!
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
37,388
64,474
Nanyaro ni member hapa JF aje atujuze vizuri kitu gani hasa kilitokea. Maadamu hata hao waliripoti polisi basi wameshafahamika ni nani.
 
kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
18,518
11,269
Dawa ya moto ni moto, hawa magamba si watu wa kuwachekea hata kidogo,ni bora ijulikane moja kama akikupiga la kushoto we unapiga yote mawili,haiwezekani kuonewa bila kosa eti kwa sababu police wako upande wao.
 
boybsema

Senior Member
Oct 28, 2010
124
14
hi ki2 naona,inashamiri,hao wafuasi wa magamba polic wanadhani wanaweza didimiza demokrasia wanavyodhania?ijulikane moja,kama siasa ni uadui wananchi tuanze,ukimkuta mwanachama wa magamba ni kipondo!maana polc wamekuwa ni walinzi wa magamba!ole wao wanaodidimiza demokrasia kwnye taifa la watu wanaotafuta uhuru wa kweli wa tanzania inayo na viongozi dhalimu!
 
Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
3,150
695
Dawa ya moto ni moto, hawa magamba si watu wa kuwachekea hata kidogo,ni bora ijulikane moja kama akikupiga la kushoto we unapiga yote mawili,haiwezekani kuonewa bila kosa eti kwa sababu police wako upande wao.

Hii ni mbaya sana. CCM?
 
SEAL Team 6

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
655
118
Naona Wassira anafanyakazi yake vizuri kama alivyoelekezwa na JK. Huyo ndiye Waziri wa mahusiano yasiyojulikana. Hongereni makamanda wa CDM kwa umahiri wenu, pole sana kamanda Nanyaro Efatha, ila nakupongeza kwa ushujaa wako.
 
Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,177
3,326
Haya mambo haya sasa naanza kutoyaamini!!
Crashwise, hiyo story yako ina matundu mengi sana.

1)akamrukia dereve...........washirika wa dereva wakakimbia, je gari ilikuwa imesimama au inatembea? na ni station wagon, right?
2) dereva aliyepewa roba au ambaye anapambana na mtu aliyeng'ang'ania steering wheel huku gari ikitembea, aliwezaje kumpa kipigo Ephata, na kumtupa nje ya gari?? na huyo mwenzake Ephata alikuwa anafanya nini??

hizi story zinaanza kuniudhi sasa!!
Kwanza siyo Crashwise ambaye umemzoea kuwa ni mnazi wa CDM! Unachobisha ni ni hapo? Watekaji walikuwa wane na jamaa walikuwa wawili dereva ambaye kwa mujibu wa Nanyaro mwenyewe ni baunsa hivyo alivyoona gari linaekea porini aliamua kumdhibiti kwanza Nanyaro ambae kiumbo ni mdogo na kisha kumtupa nje kwa kushirikiana na wenzake. Umeelewa au bado unapinga mazingira ya wao kuepuka dhahama hiyo? Elewa hii story siyo ya kutunga kama story za Erick Shigongo kule globalpublishers.
 
Daniel Anderson

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
872
140
Siyo kila story hapa tushabikie. Hebu diwani funguka tujue mbivu na mbovu hapa.
Pia tunasubiri taarifa kutoka upande wa pili.
 
Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,177
3,326
Naona Wassira anafanyakazi yake vizuri kama alivyoelekezwa na JK. Huyo ndiye Waziri wa mahusiano yasiyojulikana. Hongereni makamanda wa CDM kwa umahiri wenu, pole sana kamanda Nanyaro Efatha, ila nakupongeza kwa ushujaa wako.
Bila kujitoa mhanga nadhani tungekuwa tunazungumza mengine, halafu Nanyaro ni mwanaJF hapa ila kutokana na mazingira ya Igunga kuna kipind hapatikani ila atakuja kuthibitisha habari hii kwa wale wenye mashaka kama Birigita.
 
Ndechumia

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
1,062
292
hapo kazi ipo!!! vitisho kila kukisha, kwan hilo gari T203 BKW mmiliki wake ni nani?km unafahamu,
 
Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,938
Mzee wa rula bado sijakusoma vizuri;
-Waliotekwa walipandishwa kwenye gari ya watekaji ama gari ya waliotekwa?
-Unaweza kutoa ufafanuzi wa jinsi tukio lilivyotokea hasa pale Nanyaro alipokamata steering na watekaji wenzake na dereva wakakimbia. Huyo Boniface aliyekuwa na mh. Diwani alikuwa wapi wakati huo?
 
Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,938
Kwanza siyo Crashwise ambaye umemzoea kuwa ni mnazi wa CDM! Unachobisha ni ni hapo? Watekaji walikuwa wane na jamaa walikuwa wawili dereva ambaye kwa mujibu wa Nanyaro mwenyewe ni baunsa hivyo alivyoona gari linaekea porini aliamua kumdhibiti kwanza Nanyaro ambae kiumbo ni mdogo na kisha kumtupa nje kwa kushirikiana na wenzake. Umeelewa au bado unapinga mazingira ya wao kuepuka dhahama hiyo? Elewa hii story siyo ya kutunga kama story za Erick Shigongo kule globalpublishers.

Mkuu sasa nimekupata baada ya kuuona ufafanuzi wako.

Hizi ni dalili kwamba siku ya leo ni lazima makamanda wajipange vizuri zaidi kiulinzi na kiusalama kwani chochote chaweza kutokea kabla ya kesho.

Hawa magamba kwa kushirikiana na mungiki yao na wing C (polisi) wanaweza wakawatengenezea zengwe ili makamanda wasiwepo wakati wa upigaji na uhesabuji wa kura.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom