Diwani wa CHADEMA anena - Matatizo ya ugumu wa maisha HAYANIHUSU

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
Kama kiongozi sipendi kuwa mnafiki. Matatizo yangu sio matatizo ya watanzania wengi. Na matatizo ya watanzania wengi sio matatizo yangu. Sipandi daladala. Silali njaa. Watoto wangu hawaathiriki na migomo iwe ya mabasi, walimu au madaktari. Kufilisika kwa mifuko ya jamii hakunishtui.

Ujambazi haunisumbui sana kwa sababu ni silaha, nina walinzi, nina electric fence. Majirani zangu pia wanvyo vyote. Bei za sokoni hazinipi shida kwa sababu nanunua mahitaji yangu Supermarket. Barabara mbovu hazinikeri sana maana naendesha VX yenye air suspension! Foleni sio shida gari yangu in AC!

JE ni sababu gani kama kiongozi inayonifanya nitoke povu kujidai naumizwa na matatizo ya watanzania? Ni kwa nini watanzania hawaoni uongo na unafiki wa viongozi wao? Kwa nini wanakubali tunawadanganya mchana kweupe?

Msando Alberto - Diwani CDM kata ya Mabogini, Moshi Vijijini
 
Mwenye akili timamu wata mwelewa aliimanisha nini...
 
Sometimes Yes sometimes No!
Wewe unavyo, lakini shangazi, wadogo zako, Wajomba na mabinamu zako huko kijijini wana shida kama kawi!

Hamaanishi kwamba anajivunia kuwa na navyo kama kweli anavyo bali anafikisha ujumbe wa Watanzania ambao masikio yetu yamejaa nta na macho yetu yana upofu kama tumemwagiwa acid
 
El Toro, kwa nafasi yako ningetumaini ungekuwa wa mwisho kupotosha. Ila sishangai umeamua kuwasilisha kipande tu ambacho unajua kitapeleka hisia tofauti.

Kipande hiki hujakiweka:

@ Chacha. Nimekulia Kijiji cha Chekereni, Kata ya Mabogini. Nimesoma shule ya Msingi Chekereni. Uongozi pekee niliona na ninaoamini nastahili ni kuwa Diwani wa Kata ya Mabogini au Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Chekereni/Mjumbe wa Halmashauri. Sio ubunge wala uwaziri. Sababu kuu ni kwamba naamini nina jukumu la kuisaidia jamii yangu kupiga hatua za maendeleo. Ni kwa sababu ni wanajamii hao hao kwa njia moja au nyingine wamenisaidia kufika hapa nilipo leo hii. Naamini kwamba kwa kuwa kiongozi ngazi ya chini naweza nikawa sehemu ya msingi wa maendeleo ya Taifa letu.

Lakini nasisitiza kuhoji unafiki wetu viongozi (iwe CCM au CHADEMA) kujidai kwamba tunayajua matatizo ya wananchi kuliko wananchi wenyewe. Ni kwa sababu hatuishi maisha ya mwananchi wa kawaida ndio maana kila siku matatizo hayaishi. Ni wabunge wangapi watoto wao wanasoma shule za kata? Kwenye Kata yangu hakuna mtoto wa kiongozi hata mmoja anasoma. Hakuna mtoto au mke wa kiongozi anatibiwa Zahanati ya Mtakuja au Mabogini!

Hicho ndicho ninachokisema na haitanisababisha nikae kimya kwa sababu mimi ni Diwani kupitia CHADEMA (kumbuka mimi sio Diwani wa CHADEMA). Ni Diwani wa Wananchi wa Kata ya Mabogini.
 
Back
Top Bottom