HALI ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Mwanza si shwali baada ya aliyekuwa Diwani wa
Kata ya Mkuyuni, Charles Lugo (Fashion), na
wanachama zaidi ya 100 kujiunga na Chama cha
Wananchi (CUF). Anaandik Moses Mseti, Mwanza
(endelea).
Tukio hilo linakuja ikiwa ni mwendelezo wa wimbi
la wanachama wa CCM kuhamia upinzani hususani
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA.
Diwani na wanachama hao
kutoka matawi mbalimbali ya
CCM, walieleza chanzo na
sababu za kutimkia CUF, kuwa
chama hicho kimetawaliwa na
vitendo vya rushwa, chuki na
undugu kitendo
kinachosababisha kukosekana
kwa demokrasia ya kweli.
Wamesema viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya
chini hadi Taifa, wamekuwa wakitumia rushwa
kushika madaraka na kusababisha watu ambao ni
wazalendo wenye nia dhabiti ya kuwatumikia
wananchi kukosa haki hiyo.
Wanachama hao wakiongozwa na diwani huyo,
walipokelewa leo na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
CUF, Karume Jeremiah, wakati wa mkutano wa
hadhara uliofanyika eneo la Chakechake,
Nyamagana.
Akizungumzia tamko la wao kujiengua CCM na
kujiunga CUF, Fashion amesema wamefikia hatua
hiyo kutokana na kuchoshwa na vitendo alivyodai
vya rushwa kwenye uchaguzi, uonevu na hila na
kukosekana kwa demokrasia.
Tumetoka CCM kwa sababu ya wizi wa waziwazi
katika uchaguzi, wanafunga magori ya mkono
watu wakiwa wanaona, sasa tumekuja huku
upinzani. Lazima tuwashughulikea mpaka
waachane na wizi wao.
Niliwania udiwani kwa mara nyingine tena, hila
na tamaa ya CCM walinikata jina kwa sababu
nilikuwa napingana nao, walipolazimisha fedha za
miradi ya wananchi tuzitumie kwa mambo ya
chama, amesema Fashion.
Kwa upande wake, Jeremiah amesema kutokana na
CCM kushindwa kuwatumikia wananchi ipasavyo,
sasa umefika wakati wakaipisha UKAWA kuingia
`magogoni` ili kutatua kero za watanzania.
................
.
KILAZA