bambumbile
Senior Member
- Aug 30, 2009
- 109
- 0
Tatizo hapa ni kuwa Mwenyekiti mwenye alikuwa hakimu katika mahakama ambazo tunasema court of no law.
Hakuna sheria ya Diwani kumfukuza diwani mwenzake, hapo jamaa kachemka sana.
Mahenge kachaguliwa na wananchi na ndio hao watakaomuondoa lakini hawezi kufukuzwa na mtu yeyote yule zaidi ya kusimamishwa na baraza la madiwani wenzake. Anasimamishwa na baraza la madiwani na sio kufukuzwa, sasa huyu jamaa ni sheria gani anazotumia hadi kuandika barua ya kijinga kama hiyo?
Mahenge amempiga bao Mwakyembe, ndio maana Mbunge anatumia kila rafu kumharibia jamaa lakini kashindwa.
Gwamaka,
Lakini huenda pia Mwenyekiti wa Halmashauri aliamua yeye mwenyewe. Uongozi wa wilaya unashughulikia hili jambo na mpaka sasa ni wazi mwenyekiti kakiuka sheria. Kama ulivyoandika, hao mahakimu wa zamani wanajifanya wanajua sheria kumbe sivyo.
Inabidi kuwa waangalifu maana kama yeye kafanya kosa na wao wasifanye makosa ya kumsimamisha mwenyekiti. Inabidi kupunguza joto hapa Kyela maana limezidi mno.