Diwani Kata ya Kyela Matatani Kufuatia Kuanzishwa Mamlaka ya Mji Mdogo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani Kata ya Kyela Matatani Kufuatia Kuanzishwa Mamlaka ya Mji Mdogo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KILITIME, Nov 17, 2009.

 1. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tarehe 13 nov 2009 ndio tarehe iliyoandikwa barua na M/KITI WA HARMASHAURI YA WILAYA YA KYELA kwenda kwa diwani wa Kyela Mh Mahenge maarufu kwa jina la MAKETE/HALF LONDON nakala kwa tamisemi dodoma, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi wa wilaya, afisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji mdogo wa Kyela, katibu wa ccm.

  Kuwa kuwepo kwa mamlaka ya mji mdogo ktk oneo la kata ya Kyela mjini kunapelekea kata ya kyela isitambulike tena kwa maana kata hiyo kwa sasa imefutika hivyo diwani,wenyeviti wa vijiji kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa ya 1982 kifungu no.45(1) cha kushangaza ni namna nzima zoezi lilivyoendeshwa ni dhairi limegubikwa na mazingira ya visasi na kukomoana yaanI ukimwaga ugali mi ntamwaga mboga duh yaan sasa tunakoelekea si kwema Mwakyembe unayaona haya tunaujua uhusiano wako na makete si mzur

  Wakazi wa Kyela tunaomba usimamizi wako na maelakezo yako tunazijua kazi na umuhim wa diwan huyu naogopa kufananisha ya richmond na posho mbili picha kama hiyo ipo kivingine hapa wilayani upeo wangu ktk sheria si mpana lakini sitoshelezwi na hatua zilizochukuliwa ingawa nna maswala kadhaa ya kujiuliza nisaidien kuujua ukweli na hatua stahili!

  Tchao Kilitime!!
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kilitime,

  Unaweza fanyia editing hii taarifa ili iweze someka walau vizuri! Zingatia matumizi ya herufi kubwa na vituo. Nimejaribu kuisoma nikaishiwa pumzi. Hata ukiweka paragraphs itasaidia sisi wengine slow learners.

  Asante
   
 3. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kwa kifupi sana diwan hana kazi kwa " kuwepo kwa mamlaka ya mji mdogo ktk eneo la kata ya kyela mjini, kunapelekea halmashauri ya kyela ikome kuwa na mamlaka ya moja kwa moja kupitia kwa diwan wa kata hiyo"

  imesema sehemu ya barua hiyo imeendelea kueleza kua "kutokana na kufutika kwa kata vijiji navyo vimefutika na wenyeviti wake pia wamefutika na diwani wa kata husika pia naye amefutika (amekoma kuwa diwani) Hio ndio tafsiri ya sahihi ya sheria"

  hiyo ni sehemu tu ya barua hiyo kinachonitatiza ni namna ilivyosisitiza kua ndio tafsiri sahihi ya sheria naomba nielimishwe zaidi ktk hatua zilizostahili na mifano halisi ya sehemu zingine au ndo ule usemi wa

  ukimwaga mboga sisi tutamwaga ugali?
   
 4. E

  Engineer JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Wakuu,

  Mbona sijalisikia hili? Wacha nifuatilie nione kuna nini. Yaani Kyela kuwa mji mdogo ina maana hakutakuwa na diwani wa kata ya Kyela?

  Mheshimiwa Mahenge hawaelewani kabisa na Mwakyembe. Mwenyekiti wa Halmashauri ni mtu wa mbunge.

  Muhimu hapa kabla ya kulaumu ni kuangalia sheria inasemaje. Vinginevyo hawa watu wanataka kuleta matatizo.

  Huyo Mwenyekiti wa halmashauri mwenyewe hata udiwani hana nafasi ya kurudi tena.

  Hii Kyela yetu wanaiyumbisha sana.
   
 5. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mwakalinga na washabiki wake ndio wanayumbisha Kyela. Otherwise Kyela iko poa tu na kipunga tunavuna kama tunarrrria vile.
   
 6. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Jamani hizi siasa ni za watu binafsi au?? mbona wananichanganya hapa????

  hivi kuleta maendeleo kati eneo lahitaji tena siasa kwa watendaji??? au inahitaji kuchapa kazi na siasa kando, Hii ni dalili mbaya sana na uchochezi mbaya sana kuta fuka moshi hapo si muda mrefu nawambieni angalieni 2010 mtajionea kunawatu watakimbia kata au maeneo yao waliyo yaomba ktk chaguzi zilizopita kwaajiri ya utendaji mbovu wao wa kazi

  Poleni sana watu wa kyela

   
 7. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Sasa mnataka kuniambia Mwakyembe ndo kaunda Halmashauri ya Mji mdogo au? siyo TAMISEMI. Kama ni kweli kata yenu imekuwa Mji mdogo hilo ni swala la kufurahia, sasa mnalita vita kwa kulinda kibarua cha diwani wenu! yaani mnataka wananchi wakose heshma yao ya kuwa mji mdogo na kupata Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi pamoja na wakuu wa idara na watalaam wengine kwasababu ya huyo diwani? kweli nyie mmechoka, au mnaelimu gani wakuu?
   
 8. E

  Engineer JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi siasa za visasi Kyela ni balaa tupu. Nimefuatilia na kuongea na wahusika. Kilichotokea mbunge alikua hapa wiki jana na akamshauri huyo mtu wake kwamba aandike barua ya kumfuta Mahenge udiwani wa kata ya Kyela mjini kwasababu sasa Kyela imekuwa mji mdogo.

  Mwenyekiti na yeye bila kuangalia sheria inasemaje na bila kushauriana na madiwani wenzake, akaandika hiyo barua.

  Mheshimiwa Mahenge ni mfuasi namba moja wa Mwakalinga na pia anakumbukwa kwa juhudi kubwa alizofanya kusimamia ujenzi wa shule za sekondari Kyela. Yeye kwa madiwani ndiye ana uwezo mkubwa, hivyo anafanya mambo mengi kwa kujitolea. Kwa wanaoijua Kyela, yeye ni mmiliki wa guest houses mbalimbali hapa mjini.

  Madiwani wanakusanya signatures ili zifike theluthi mbili na wanataka kuyitisha kikao cha madiwani na kumfukuza kazi huyo Mwenyekiti. Mpaka leo madiwani 11 kati ya 21 wameweka sahihi zao na wanasema kesho namba itatimia.

  Katika madiwani 21, mbunge anaungwa mkono na madiwani kama watano tu akiwemo huyo diwani Kisugujila pamoja na mama watatu wa kuteuliwa na diwani mwingine wa kuchaguliwa.

  Halmashauri ya CCM wilaya pia inaandaa kikao kushughulikia mzozo huu.

  Mimi sijui sheria na tunawaomba wenye kujua sheria za miji midogo mutuelemishe. Ila nimeambiwa mji mdogo kama Tunduma una diwani wake na pia kuna mifano ya miji mingine na kwamba sheria waliyotumia kuandika hiyo barua haina maana hiyo.

  Tutawahabarisha zaidi vita hii itafika wapi. Ila nina uhakika uamuzi huu una uhusiano na uchaguzi wa mwakani na mpambano kati ya Mwakalinga na Mwakyembe.

  Watu hawataki majimbo yao yaguswe.
   
 9. E

  Engineer JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa mahenge ndiye aliongoza juhudi za Kyela kuwa mji mdogo. Kinachoongelewa hapa ni je sheria inafuatwa au inapindishwa kwa ajili ya vita vya kisiasa?

  Hivi kweli ni utawala bora kumwandikia barua kama hiyo diwani na kusambaza sehemu zote bila hata kuongea na yeye kwanza? Huu ni uongozi wa aina gani? Hata kama sheria itasema hivyo, ilitakiwa wamwite Mahenge kwanza na ikiwezekana hata kumuaga.

  Wasomi wa sheria wanaiharibu Kyela.

   
 10. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Technically inapindishwa mbaya na ni siasa duni zisizo na fikra kamili. hapo ni kufirisika kifikra 100%

  Na kama ni siasa hajui ni siasi fitna na sio siasa uchumi na maendeleo,

  Utawalaaaaaaa!!!!!! utawala gani kuhalibu maendeleo ya kata ndio utawala uende ivyo what's wrong with we black africans??? jamani hatumwogopi MUNGU????? au Hamjui kuna KUZALIWA NA KUFA KESHO au wadhani ukifa utaenda na huo utajiri sijui siasa zako kwa MUNGU??????

  me nadhani ukiwa ktk siasa na uongozi ukapata ni kuhudumia jamii, fanikisha maendeleo, jenga heshima na mengineyo ya msingi ndio ingawa twajuwa wewe ni binadamu kuna kuteleza ila isiwe makusudi sasa


   
 11. E

  Engineer JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kesho kimeitishwa kikao cha kamati ya maadili ya halmashauri na wamempa Mwenyekiti mpaka kesho awe amemwaomba msamaha mheshimiwa Mahenge, vinginevyo yeye ndiye atasimamishwa wakisubiri kikao cha madiwani.

  Hizi siasa za fitna za Afrika ndio zinatumaliza na tutaendelea kuwa maskini. Kibaya zaidi zinafanywa na wasomi ambao ndio walitakiwa wawe nuru ya mambo mapya ya maana.
   
 12. m

  magoli Member

  #12
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 14, 2009
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  .

  Mkuu jethro,
  Mbona haueleweki?Umeandika nini sasa hapa?
   
 13. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #13
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Vipi bwana mkubwa, tunaomba updates za huko Kyela, mambo yamekwendaje?
   
 14. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #14
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sijapata kabisa kinachoendelea huko kwa Mhishimiwa Dkt Mwakyembe!
   
 15. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #15
  Nov 18, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  aanayetakiwa kuandika barua hiyo ni mkurugenzi iweje mwenyekiti wa halmashauri kujipa madaraka ya kuandika barua hiyo.kwa sababu hiyo ndio shaka ya kuhusika kwa Dr mwekyembe kunakuja kwani mahenge ni hasimu wa DR na mwenyekiti wa halmashauri ni mfuasi wa DR.
   
 16. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #16
  Nov 19, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa vipi nini kinaendelea huko tukuyu wanaseme mheshimiwa mbunge mwakyembe amekwenda jimbon hebu tueleze kinachoendelea huko mkuu
   
 17. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #17
  Nov 19, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  .... Nasikia mh Mahenge amemtaka mwenyekiti wa almashauri amwombe msamahaa!
  je Mkiti ametii??
  uliahid kutujulisha zaid nini kinaendelea huko Kyela nasikia Mh Mwakyembe yuko huko Jimbon je ni kweli na inahusiana na tatizo hili ua ni safari zake za kawaida za jimboni??
  Je hadi sasa mbunge ametoa msimamo gani ukizingatia yeye ni mwalimu wa sheria?? hata PCCB wanajua naomba mtupatie tafsiri sahihi ya sheria iliyotumika kumwachisha diwan huyu 1982 kifungu no 45(1)'sheria ya serikali za mitaa ya
   
 18. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #18
  Nov 19, 2009
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  habari nilizozipata hivi punde nasikia wananchi wa kata ya kyela wanataka kuandamana kuipinga hiyo barua! hivi sasa naambiwa mheshimiwa dawani anapita kwa wenyeviti kuhamasisha maandamano hayo! vp mbona umekaa kimya sana
  wakati huu sisi tunakutegemea sana kwa kutujulisha kinachoendelea huko!
   
 19. E

  Engineer JF-Expert Member

  #19
  Nov 19, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kilitime,

  Hapa vurugu tupu na wacha tuone mwisho wake utakuwaje.

  Sikuandika jana kwasababu hata mimi yamenikuta, nimechongewa kwenye uongozi wa wilaya kwamba namwandika vibaya mbunge JF.

  Eti mbunge amepewa IP ya computer ninayotumia na uongozi wa JF. Hiyo ni JF where we dare to speak openly!

  Wote tunaotumia hiyo kompyuta ya kazini tuliwekwa kitimoto ila hawana ushahidi ni nani. Nitawajulisheni zaidi baadaye. Watu wanashindwa kufuatilia maendeleo, kazi ni kufuatilia wale ambao wanapingana nao kimawazo. Engineer hayumbishwi na mtu yeyote.

  Kuna vikao vingi bado vinaendelea. Mwenyekiti amekataa kuomba msamaha ingawaje sasa ni kama anakubali tafsiri yake ya hiyo sheria ilikuwa na makosa.

  Leo siku ya tatu watu hawafanyi kazi na wanaongelea mgogoro huo tu.

  Nikipata maelezo zaidi nitawajulisheni. Wacha nilinde kibarua changu kwanza.
   
 20. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #20
  Nov 19, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Pole sana. Mbombo ngafu.
   
Loading...